Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

Unawapataje hao watanzania Apo earport maana mie sijawaona pale jk nataka niende cantona fear mwezi wa nne

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nakushauri uende china kwasababu vitu ni bei nafuu sana na utapata idea ya vtu vingne pia

mimi naish huku ila sio guangzhou so nilipata nafasi ya kwenda kutembea guangzhou mwaka jana mwanzon

vitu vya kuwasaidia kwa experience na uelewa wangu kama atakae kuwa anajua zaid atanisahihisha

ticket mm za bei nafuu kabisa huwa nakata STA travels posta karibu na shule ya mtendeni jengo moja na Takims safaris n tours

hapo huwa napata ticket kuanzia laki 7 na ktu one way ya kwenda guangzhou ila ukate mwez kabla


kwa guangzhou inategemea sasa kama unakwenda kwaajili ya canton fair nakushauri ukae (wansheng wei) ni karibu sana na Canton na kama unataka kukaa mbal na maeneo waafrika waliojazana ...hio sehemu ni nafuu kwa hostels sio hoteli lkn hostels ni nzur sana ....anyway since ni mgeni hio sehemu inaweza ikawa mtihan kdogo hivyo waweza kaa (sanyuanli ) hapa kuna hoteli nying na za bei ya chini sana utapata chumba hadi cha elfu ishirini na ktu kupanda ila hadhi ya chumba ni kulingana na hela unayoilipia ...advantage ya hapa upo karibu na soko la nywele ..vipodoz ..na nguo ..walking distance na migahawa ya kiafrika ...pia soko la cm halipo mbali


kuna xiaobei ...hii ni kama posta ya guangzhou pia unaweza pata hotel nzur za kuanzia elfu 50 hv 40 kupanda ...advantage upo karibu na masoko


sasa basi una save vipi gharama zisizo za msingi

cha kwanza ...uwe na mwenyej ...wapo watu wanafanya io kaz ya kutembeza watu masokoni ila kwa experience yangu Wazanzibari wana bei ndogo sana kuliko wabongo ....mm nlimlipa mzenj elfu 70 kwa siku 3 kunitembeza masokon wakat wabongo wanataka hadi dollar 100 kwa siku

ishu ya pili ...ya kusave pesa guangzhou ni kununua chakula kwenye migahawa ya wachina (waislamu ) halal restaurants chakula ni close na chetu na nikizur kwa bei chee ...starting price ni elfu 4 hv wakat restaurant za kiafrika vyakula sahan had elfu 30 huko inafika

njia nyingne ya kusave hela guangzhou punguza matumiz ya taxi ...usafr wa gharama ndogo ni Treni ya underground (metro ) hii hadi airport mpaka hotel unayokwenda unaweza unganisha ukalilipa buku 3 au nne na ni umbali tuseme kimara mpaka mbagala hv wakat umbali huo taxi unalipa hadi elfu 60 hv

kingne chochote unachotaman kununua hakikisha upo kwenye soko sahihi ndio utapata bei nzur usione tu kiduka kinauza cm ukadhan ni bei nzur hapana nenda kwenye soko halisi la hio bidhaa utapata bei nzur

kingine ukifika sokon take your time zunguka kabla kufanya maamuz maana bei ni tofaut na wauzaj ni weng sana ...ukipanda taxi hakikisha unatoa pesa kamili .maana madereva taxi huwa wanatoa chenj hela feki sometimes ....usimwamini mtu na mizigo yako ..matapel weng hata waafrika



mtaj huo 20m unatosha kabisa just go kila lakheri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu na huko china kuna kupunguziana bei madukani ukilia??
 
Na Mimi nipm namba naitaji kwenda mwezi wa 4 nifanyie wepesi tafadhari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nishawhi kuwasmbia mods waiboreshe jf waweke option ya sauti ila kuna mbwa mmoja akaropoka akauliza unataka voice note we kasuku?

Mods hawakuboresha mana walijua utatusi kwa sauti kama unavotusi kwa maandishi(mbwa mmoja)...
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nadhani huyu atakuwa ni mwalimu wa mwandiko, anasahihisha matumizi ya L na R
Yan watanzania tuna shida sana ndugu yangu
 
Mi naongezea apande ethiopian airline na wakati wa kurudi ashuke nairobi apande basi za dar atasave karibu laki 500.
Kama umekata go and return unawezaje kusave hiyo?
 
D
Dollar 100 ni kwa siku zote atakazo kaa?
 
hii post yakufanyia lamination
 
Mungu akubariki sana
 
benjamathayo,
Umesoma hadi darasa la ngapi wewe? Unashindwa kutofautisha matumizi ya L na R, hizo pesa si utaenda kupoteza tu huko?
Nenda kariakoo pale wenye maduka makubwa kaulize elimu kama utamkuta ata mwenye phd uje humu usimulie, nenda mwanza, kahama, mbeya, tunduma kaone watu walivyo na mawe alaf kaulize elimu yao uone...
Tafuta pesa uone kama wenye hyo elimu hawajaanza kujikomba komba kwangu kwa mapambio.
 
Tangu lini wenye elimu wakawa na hela
kuna kitabu kinaitwa
"Why A student work for C student 🤣😂
 
Tangu lini wenye elimu wakawa na hela
kuna kitabu kinaitwa
"Why A student work for C student [emoji1787][emoji23]
asilimia kubwa wakulima wenye plantaions hapa TZ hawana elimu kabisa au kama wanazo basi za kuunga unga, wenye viwanda na biashara kubwa mijin na vijijin elimu zao ni za kuunga unga na soletape au hawana kabisa ila wenye elimu wanaenda kuomba vibarua na kazi kwao...
Elimu ni nzur sana ila ukianza kujitamba kwa elimu yako utaonekana mpuuz fanya tu research matajir wa mtaan kwako kaulize elimu zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…