Nataka na nina Nia ya Kuwa Tajiri Nipeni Mawaidha yenu!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Kheri iwe pamoja nanyi ndugu zangu!
Mimi ni kijana Mwenye umri 20s nina ndoto na nia ya kuwa Tajiri(Financialy), Nahitaji kuwa Tajiri yaani kuwa na Pesa ndio Furaha yangu....sihitaji kingine zaidi ya Pesa....Nahitaji kuwa Tajiri.

katika shughuli zangu ninazozifanya mara kwa mara naambulia pesa ya kawaida ya kubadilishia mboga...Hali ambayo siridhiki nayo.

Yaani nataka kuwa Tajiri Haswa ile ukifika mtaani waseme Flani naye ni Tajiri wa Huu Mtaa.

Nimewaza sana nikafikia uamuzi wa kutumia Nguvu za Giza maana kila niliyejaribu kuzungumza naye amejaribu kunisihi kwamba ukitaka kuwa tajiri lazima shetani awe na ukaribu na wewe.

Nimejaribu kufuatilia story za Matajiri wengi nimeona wao pia wameegemea sana upande wa Nguvu za Giza sina uhakika kama wapo au hawapo ambao wanategemea nguvu za Mungu.

Sasa ndugu ambao kidogo Mna idea ziwe hizo za Nguvu za Giza au kama kuna Njia Nyingine tofauti nipeni Mawaidha yenu ili Nifanikishe lengo langu.

Asanteni.
 
How To Become A Billionaire (Seriously)
 
Soma link hiyo. Pia je wewe unejiajiri au umeajiriwa? Unafanyashughuli gani? Je unafanya uwekezaji wowote? Kwani kama umeajiriwa kuwa tajiri sahau kuwa tajiri labda kipato cha kati tu. Kama umejiajiri basi upo kwenye njia sahihi ya kuwa milionea kuelekea bilionea. Ni ngumu kuwa hivyo unavyotaka ila ni inawezekana.
 
Nguvu za giza zitakufanya usiufaidi utajiri wako! Kuna masharti utapewa ambayo yatakufanya uishi km mtumwa maisha yako yote. Pia usishangae kafara za watu wako wa karibu ambao ungependa waufaidi utajiri wako zikihusika
 
Nguvu za giza zitakufanya usiufaidi utajiri wako! Kuna masharti utapewa ambayo yatakufanya uishi km mtumwa maisha yako yote. Pia usishangae kafara za watu wako wa karibu ambao ungependa waufaidi utajiri wako zikihusika
Toa Hii ides vizuri tafadhali boss
 
Nguvu za giza zitakufanya usiufaidi utajiri wako! Kuna masharti utapewa ambayo yatakufanya uishi km mtumwa maisha yako yote. Pia usishangae kafara za watu wako wa karibu ambao ungependa waufaidi utajiri wako zikihusika
Toa Hii ides vizuri tafadhali boss
 
Ili uwe tajiri Fanya yafuatayo∆1.andaa mpango wa muda mfupi wa kuendeshea maisha yako ya kila siku. 2.andaa mpango wa muda mrefu wa muda mrefu wa kiuchumi ongeza elimu yako ya uzalishaji iwe ile iliyo rasmi au isiyorasimi.wekeza vitu vyenye faida kauanzia miaka mitano na kuendelea wekeza katika biashara kwakuanza kwa kidogo ilikuapata uzoefu wa biashara wekeza katika kilimo cha miti ya matunda kule kijijini kwenu.hayo ni baadhi tu ya mambo yatakayo kufanya uwe napesa.na akili ya kuambiwa changanya na za kwako.
 
Je umeajiriwa? Je umejoajiri? Je unatamani tu kuwatajiri na hauko tayari kufanya mambo yatayokupa utajiri. Kwanza nisema mimi binafsi siamin kama utajiri unauhusiano na nguvu za giza. Kama unaimani na nguvu za giza basi sidhani kama utapata huo utajiri na kama utapata hautikuwa na amani na huo utajiri wako.
 
Duh elim elim elim
Ungesoma tu bila kuandika pia ni jambo la busara sana. Wanasema ukitaka kuona au kuelewa uwezo wa kufikir wa mtu basi mpe nafasi ya kuongea au mpe karatasi na kalamu aandike. Kwani mtu akiandika au kuongea anaonesha uelewa au ujinga wako hadharani.
 
Unataka utajiri serious au unabwabwaja tu? Kama upo serious njoo PM....I will give you the real techniques. Thanks
 
Unaposema utajiri unataka uwe na kiasi gani cha pesa? Unatakaufikie hicho kiwango lini?
 
Kama una mama au baba wa kumuweka store?nitafute nkupeleka...tafuta hela ya mganga na pumba za kumlisha mzazi wako akiwa store...
 
Better idea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…