Nataka niache kazi niende Dar es salaam kuendesha boda yangu

Nataka niache kazi niende Dar es salaam kuendesha boda yangu

Wakuu hamjambo??

Niende Moja kwa moja kwenye mada...Mimi nipo Kanda ya ziwa nilikuwa nafanya kazi sehemu kwa bahati nzuri nilijikusanya kwa mshahara wa 400,000 nikafanikiwa kununua pikipiki

Nataka kuacha kazi hii ya ualimu niende Dar kuendesha boda hasa bolt...make naona kama nachelewa kutafuta maisha... mshahara haunitoshi kabisa..

Hivyo wadau mlipo Dar na mnaondesha boda uko Dar baishara hii ipoje...make lengo langu nataka nipate 30,000 kwa mwezi...

Karibuni wadau kwa ushauri...nimechoka kuajiriwa pia nilivyokosa hizi kazi za ualimu za serikali ndo nimekata tamaa kbs
Karibu Sana ila kabla hujaacha KAZI usisahau kuwa diesel imepanda bei
Pia kwa malengo yako hayo ya faida ya elfu 30 daily uje umejiandaa kabisa kufanya makazi yako juu ya pikipiki
Na mwisho wadada, wadada, wadada
 
Back
Top Bottom