Habari za saa wajumbe wangu,
Kuna ndoto ambayo nimeona na nikaamka usiku wa kuamkia jana kwamba viongozi wetu wa dini hasa hasa jamaa zetu wa Rome wanashiriki kumshauri mzee zaidi ya 75%.
Si vibaya kupewa ushauri wa kiroho kutiwa moyo namna ya kuwahudumia watu wako, lakini je kuna ukweli na uhalali ndani yake? Hakuna haramu kweli?
Yawezekana kabisa kabisa kwa yanayoendelea, kuvurugwa kwa uchaguzi, kura kuibwa, watu kuuawa na wengine kuteswa na kupigwa hawa viongozi wa dini wapo kimya wanaona sawa. Wanamtia mzee moyo bila kutazama kuwa hali si shwari. Kama sivyo kwanini hawa viongozi wa dini wamekaa kimya? Maovu hawataonja?
Ni Mungu yupi wanamwakilisha katika utumishi wao?
Hizi damu zilizomwagika katika uchaguzi huu kwanini mikono yao isiwe imechangia huko?
Ni ndoto lakini naendelea kutafakari, tuenda ikawa na maono ndani yake. Viongozi wa dini laana hii haitawaacha salama nawaambieni.