KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Ukipita sehemu za wanamaombi utasikia wakiutuma moto (wanapiga faya) kwenda kwa shetani, mapepo, wachawi na waganga.
Ukiingia kwenye makanisa yao utakuta watu wamepagawa na mapepo, mapepo yanasema naungua, naungua, usinichome, natoka.
Kuna watu wanasema huko makanisani kuna maigizo na hizo kelele haziakisi ukweli wowote. Sasa kuondoa ubishi, nimeona nije na pambano la wazi ambalo walokole watapambana wa waganga tuone ni kundi gani lina nguvu zaidi.
Mipango inaendelea, mtajulishwa ni lini na wapi pambano litafanyika, na Zawadi zitakuwa ni zipi kwa washindi.