Wisdom
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 492
- 122
Kama wewe ni msomaji wa Biblia mapambano ya hivyo yalishafanyika.Ukipita sehemu za wanamaombi utasikia wakiutuma moto (wanapiga faya) kwenda kwa shetani, mapepo, wachawi na waganga.
Ukiingia kwenye makanisa yao utakuta watu wamepagawa na mapepo, mapepo yanasema naungua, naungua, usinichome, natoka.
Kuna watu wanasema huko makanisani kuna maigizo na hizo kelele haziakisi ukweli wowote. Sasa kuondoa ubishi, nimeona nije na pambano la wazi ambalo walokole watapambana wa waganga tuone ni kundi gani lina nguvu zaidi.
Mipango inaendelea, mtajulishwa ni lini na wapi pambano litafanyika, na Zawadi zitakuwa ni zipi kwa washindi.
1. Musa na Haruni VS Janess na Jembres (wale wachawi wa Farao) na Musa na Haruni walishinda
2. Elia VS wachawi wa Baali
Upande mmoja kulikuwa na wachawi na waganga 890 na upande mmoja Nabii Elia na mechi iliishakwa Elia nabii wa Mungu kuibuka kidedea
3. Daniel VS wachawi wa Babeli
Mfalme aliota ndoto na akaisahau akawaita wachawi na waganga wake wote na kuwaambia kwanza wamkumbushe ndoto alafu wamuambie tafsiri yake wakashindwa akaletwa Daniel akamkumbusha ndoto na kumpa tafsiri sahihi
4. Yusufu VS Wachawi wa Misri
Farao aliota ndoto na ikamsumbua akawaita wachawi wote Misri na kuwaambia wamuambie maanana tafsiri ya ndoto ile na wakashindwa lakini Yusufu akaletwa kutoka gerezani na kutafsiri ile ndoto kisha kutoa solution ya nini kifanyike