Wakuu, hasa kwa Wanaume tunaowapa wake zetu mitaji, leo nimepata wazo...nahitaji ushauri kidogo.
Mke wangu ni mjasiriamali, tokea nimemuoa yeye ni mtu wa biashara.
Kipindi cha maandalizi ya harusi yetu, aliweka pesa nyingi sana kwenye maandalizi ya sendoff yake.
Tunaingia kwenye ndoa mtaji wake ukiwa hoi.
Ikabidi nitoe kama 13M hivi kupush mtaji ili awe stable, offcoz biashara ikasimama poa, nikapata janga kidogo 2016 baada tu ya uchaguzi wa 2015 (kazi zangu zikasimama)
Most of biashara zake ndio zikawa zinapush life, naanza kurecover 2017 narudi job, biashara zake zikawa zimedorora sana nikahisi mimi ndio chanzo...anyway nilivyorudi tu job, nikakopa bank nikampa 12M pamoja na kutoa mahitaji yote ya home. Lazima kila mwezi niweke 600k home...(exclude ada za watoto).
2020 wakawa wanajenga kwao japo alifanya kimya kimya, ila nilijua yeye na Dada yake waliwajengea wazazi wao...so business ika drop(walifanya kitu kikubwa kuliko uwezo)
Malalamiko yakaanza tena, anyway kwasababu madeal yangu yalikuwa poa nikamjaza tena 10M kupush mtaji...in most cases biashara yake inamhudumia mwenyewe kwangu ni poa, hela ya nywele, nguo zake n.k huwa anafanya mwenyewe...
This time amekuja tena na wazo lakuomba kuongezewa mtaji, abadilishe na kuongeza biashara.
Na mimi nina maeneo yangu nataka kuyajenga sasa...
Nimemwambia nimkopeshe 25M ila ajue atairejesha, na njia atakayotumia ni mimi kutokutoa matumizi ya ndani, ile 600k atoe yeye kama marejesho...kakataa, kwasababu huko nyuma sikufanya hivyo...
Maisha yanabadilika umri unakwenda na bado sijafanya uwekezaji ninaoutaka!
Hapo nakosea? Je, maamuzi yangu ni sahihi au nakosea?