Nataka nichukue mkopo ninunue mabasi ya mikoani

Hizo ni tamaa na sio wazo la biashara
Anza na kidogo ulichonacho Kwanza ndio ufike mbali
Mkopo wanachukua baada ya kuona biashara inaenda vizuri na sio kuanza na mkopo
Ila kila la kheri
 
Hata bei ya mabasi hajui
Nina rafiki wa mabasi ya mkoani mengi sana, na kila akiuza ya zamani ili aingize mapya lazima aagize kwa mkopo ambao huwa ananishirikisha karibu kila jambo hadi gharama ya basi moja hadi inakanyaga barabarani sio chini ya hiyo pesa kwaiyo kijana kama anaona milioni 500 ajaribu aone....ila kwa iyo pesa pia anaweza nunua tandem 3 nahisi mpaka anakamilisha kila kitu iyo pesa itakuwa imefanya jambo kubwa na chuma zitaanza kazi
 
Do you have collaterals and competitive business plan, since bankers are not risk takers

Je unadhamana na andiko shindani la mpango wa biashara
 
Vip kuhusu dhamana?
 
Ni kweli kwa Bongo hawaamini ktk Idea za Watu .niliwahi kumsikia E. Shigongo wakati anaanza biashara yake ya magazeti yake Udaku, akawa hana mtaji, akampelekea mzee mmoj rafiki yake hiyo Idea walau amkopeshe kiasi fulani cha Pesa. Yule mzee hakumuamini, akampiga tarehe, lakini baadae akaja kumkopesha ile hela.

Yule mzee,angekuwa mjanja, angemwambianamuuzie share ktk hiyo biashara. Ila makunaliano yalikuwa ni kukopeshana.

Leo hii huyo Mzee japo hata simjui, lakini lazima atakuwa anasimulia, kuwa amewahi kumsaidia E.Shigongo wakati anajitafuta.
 
Toa mfano wa mkopo wa 10 au 5m ?na treasury bill ni benk yoyote inachukua. Mfano unawezanukawa naa hisa au utt exim wakachukua mkopo
 
Sio kikoba wala upatu🤣🤣🤣🤣
Yeye anadhani mikopo nikama maji unaenda kuchota mtoni ama bombani, elimu yake haija msaidia, itoshe kusema ana tatizo gorofani amekuja kwenye jukwa hilli kwa utani
 
Ushauri wangu tafuta kwanza experience ya biashara ya vyombo vya moto

Ni zaidi ya unavyoona barabarani


Anza hata TATA kakope africaries huko ujipime uwezo



Afu pia huwezi kopesheka pesa zote hizo kama sio mfanya biashara na huna dhamana
 
Kununua mabasi hio si idea mkuu, hio kila mtu anaweza fanya au i afabywa na watu wengi, tu
 
BOT wanatoa mikopo kwa watu binafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…