Nataka niende Chato nikaiombe msamaha familia ya Hayati Magufuli

Nenda bwanaaa usitutishe
20231112_185139.jpg
 
Mtu aliyeweza kuishi mjini wakati wa Magu basi hakuna hali ya uchumi itakayomshinda , na hata hayati mwenyewe alisema .

Mimi pia nilipata changamoto ila nilijaribu shamba na mjini na hatimaye nikarudi kwenye reli.

Pambana na maisha bila kujali ni nani anatawala.

Maisha siyo rahisi haswa kwa mwanaume. Usikate tamaa!
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau hata tulichokisomea kwa sababu tuliamua kufanya mambo mengine nje na elimu zetu ili maisha yaende.

Kiukweli alipokufa magufuli mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana waliofurahi sana, nakumbuka siku hiyo walipotangaza kifo cha magufuli mida ya saa sita usiku.

Mimi nilibubujikwa machozi ya furaha nikiamini kuwa sasa na mimi nakwenda kulamba asali, kwa sababu yule aliekuwa anazibana sector binafsi na kubana kutoa ajira serikalini ametangulia kwa hiyo mambo yatakuwa mtelezo.

Sio siri kwa sasa mambo ndio yamekuwa magumu zaidi huwezi kupata kitu mpaka utoe chochote sio tamisemi wala wizarani sio utumishi wala sector binafsi mambo ni magumu zaidi ya jana.

Hata angekuwepo mpaka sasa ungeendelea kuteseka tu. Ajira haikua sera yake yule Bwana. Ni afadhali ya sasa. Nawajua washikaji kibao waliopata ajira straight baada ya kumaliza chuo bila kutoa hata senti kumi. Mlilie Mungu wako akufungulie njia. Kulilia kaburi ni sawa na kutambika mizimu. Kaburi la Magufuli halitoi ajira. Acha kudeka! Hakuna wa kukuhurumia usipofikiria nje ya Box
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau hata tulichokisomea kwa sababu tuliamua kufanya mambo mengine nje na elimu zetu ili maisha yaende.

Kiukweli alipokufa magufuli mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana waliofurahi sana, nakumbuka siku hiyo walipotangaza kifo cha magufuli mida ya saa sita usiku.

Mimi nilibubujikwa machozi ya furaha nikiamini kuwa sasa na mimi nakwenda kulamba asali, kwa sababu yule aliekuwa anazibana sector binafsi na kubana kutoa ajira serikalini ametangulia kwa hiyo mambo yatakuwa mtelezo.

Sio siri kwa sasa mambo ndio yamekuwa magumu zaidi huwezi kupata kitu mpaka utoe chochote sio tamisemi wala wizarani sio utumishi wala sector binafsi mambo ni magumu zaidi ya jana.
Unatakiwa uikatae ccm!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mwizi mzuri, anayeiba kuku, kiatu, ndara na anayevunja na kuiba gari tv, wote majizi,
Maghu,alizuia wengine wasiibe, sukuma gang ndio walikuwa majizi, mjomba alikuwa boss hazina,shemeji ndio mkandsrasi wa tamisemi, waliopinga wakakutana na kamba za kunyongea za vijana wa makumbusho!
Kulikuwa hakuna uadirifu, watu walikuwa, na hofu.
Angenyonga wezi lakini na ye ye asiibe na genge lake, tungekuwa mbali, ishu ya makinikia, alituingiza mkenge, kesi tumeshindwa, tu nalipa fidia Hao mabeberu, ukienda umwambie, aliowapiga risasi walikuwa wanasema ukweli kuhusu mikataba, na ye ye aombe msamaha,
System yake haikuwa mbaya yote, nchi za Afrika, hatuhitaji wa bunge 250! Wizara 30! Wakuu wa mikoa, wilaya, na upuuzi mwingine, kila halamsshauri kuna kenge wanaitwa maofisa biashara wa wilaya, na maofisa utamaduni!
Mambo ya biashara waaxhiwe TRA,
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau hata tulichokisomea kwa sababu tuliamua kufanya mambo mengine nje na elimu zetu ili maisha yaende.

Kiukweli alipokufa magufuli mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana waliofurahi sana, nakumbuka siku hiyo walipotangaza kifo cha magufuli mida ya saa sita usiku.

Mimi nilibubujikwa machozi ya furaha nikiamini kuwa sasa na mimi nakwenda kulamba asali, kwa sababu yule aliekuwa anazibana sector binafsi na kubana kutoa ajira serikalini ametangulia kwa hiyo mambo yatakuwa mtelezo.

Sio siri kwa sasa mambo ndio yamekuwa magumu zaidi huwezi kupata kitu mpaka utoe chochote sio tamisemi wala wizarani sio utumishi wala sector binafsi mambo ni magumu zaidi ya jana.
Kama unaenda kwa sababu ya hiyo basi ni uamuzi wa ovyo

Hakuna raisi yoyote ambaye anaweza kurekebisha tatizo la ajira

Shida kubwa ipo kwenye mfumo mbovu wa elimu, kibaya zaidi unazalisha watu wengi zaidi kupitia BRN

Hata wasio na uwezo wanafika chuo kikuu

Idadi kubwa ya wasomi (wengi uchwara) ukijumlisha mfumo mbovu wa elimu = unemployment
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau hata tulichokisomea kwa sababu tuliamua kufanya mambo mengine nje na elimu zetu ili maisha yaende.

Kiukweli alipokufa magufuli mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana waliofurahi sana, nakumbuka siku hiyo walipotangaza kifo cha magufuli mida ya saa sita usiku.

Mimi nilibubujikwa machozi ya furaha nikiamini kuwa sasa na mimi nakwenda kulamba asali, kwa sababu yule aliekuwa anazibana sector binafsi na kubana kutoa ajira serikalini ametangulia kwa hiyo mambo yatakuwa mtelezo.

Sio siri kwa sasa mambo ndio yamekuwa magumu zaidi huwezi kupata kitu mpaka utoe chochote sio tamisemi wala wizarani sio utumishi wala sector binafsi mambo ni magumu zaidi ya jana.
Endelea kuchapika.....
 
Back
Top Bottom