Nataka Nifanye hii Biashara, Wazoefu Tusaidiane

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Niaje wakuu.. Kuna Hii Biashara ya Vibanda vya Movie naona ina return nzuri asee.. 30K per Day kawaida sana. Nimeipenda kwani ina mtaji mdogo lakini pia ni ngumu kuleta Hasara na pia rahisi kufanya.

Sasa mie nataka niweke Goli hilo liwe la kuuzia Movies, Miziki, vitu kama Flash na accessories ndongo ndogo za kielekroniki.

Pia nifanye huduma ya SOFTWARE na Hardware technology.. kama kuflash simu na kuweka softwares na Windows 🪟.

Mungu akijalia niweke na KiMpesa na kama Mtaji Ukikua niuze na Simu kabisa Hapo.

Hii ni Plan yangu Mpaka sasa..

Kwenu nyinyi wazoefu naombeni mnipe mwanga maana mie ndo naanza.

Asanteni..
 
Weka.

Humu Tanzania kuna shughuli zinaonekana ni ndogo sana ila zinaingiza hela kiurahisi unapata hela ya kula.
Yeah.. ndio Target yangu kubwa.. kazi huwa napata za contract.. zikiisha unaweza sota pesa zikikata..
 
Mi namshauri afungue goli la kupaka kucha wadada. Kama lile la yule jamaa wa kimara mwisho njia panda ya bunyokwa wa kujiita sijui Athanas.

Mda wote jamaaa ana mafuriko ya kina dada ofisini kwake.

Biashara zinazogusa wanawake zinalipa

Hahahaaaaa aisee ile sehemu inaniuma manake nilianza kuifukuzia mara paaap namkuta jamaa.
 
Mkuu biashara ya movie inataka sehemu za uswazi sana na hizo kazi nyingine kama umezingatia hilo hongera ila soma hata veta short course masuala ya electronics unaweza chonga na mkuu wa chuo na usiende kusoma ila ada lazima kulipa ukipata cheti itakusaidia kwa wateja wasumbufu kuna watu wajuaji sana unaweza kwenda polisi ukiharibu simu ya mtu,
Ilishanitokea pale mikumi ndo naanza kazi mteja kaleta simu inawaka imetumbukia kwenye maji kuifungua na kusafisha haiwaki mteja akanimaindi sana mhindi fulan akaenda polisi kwenda wakaniuliza umesomea nikajibu ndio nikaonesha cheti msala ukaisha kumtengenezea jamaa simu hadi iwake ila alitaka nimnunulie mpya
 
Asante sana mkuu.. umenipa Akili Safi ya Nyongeza..
 
Achana na ma muvi kachukue kozi ya kutengeneza simu halafu fungua office classic utapiga hela mpaka uchanganyikiwe.
Ukipata wateja 10 tu kwa siku 100,000 haikukosi,si unajua kwenye ufundi simu hata MTU awe mjanja vipi ukimwambia kiasi Fulani cha hela abishi.
 
Mkuu samahani,
Naomba unipe Abc za coz za ufundi simu kwa maana ada na muda wa coz.
 
Mkuu nimesoma pale veta electronics kozi fupi ilikuwa 240000 miezi mitatu hiyo inahusu vifaa vyote vya umeme ikiwemo simu,radio,TV,inverter na matakataka yote kama hayo hiyo ada ilikuwa 2014 ila kama hujui kabisa ukirudi penda kwenda kwa mafundi wa mtaani utakuwa vizuri zaid imenipa manufaa mengi hii kazi sema nimeacha kutokana na kuona mchongo wa nje ya elimu ila mtu akijichanganya nafanya bila ya kusahau kuwa mtundu na software
 
Vpnotes mlizotumiaga unazo bado?
 
Back
Top Bottom