Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!
Mkuu kwanza pole sana aisee, hapo mwanamke huna, ingekuwa ndo mimi ningeshaacha lisereleke tu,
 
Sijui kwann niliumbwa kwa akili ya kuchunguza... Ningekua mm kwanza ningekua nmeshachunguza uhalali wa hiyo kazi, wiki tatu , hapokei simu ,nkazi gan?? Kaenda na akina nan..kwann huongei nahao akina nanani.

Ningechunguza kiasi kwamba ningegundua kua,yupo kwa huyo mwanaume alokua anamuomba hela usiku wa manane.


AMINI AMIN NAKUAMBIA ,HAPA DUNIAN MAHITAJI MAKUBWA ANAYOTAKA MWANAUME TOKA KWA MKEWE NI
[emoji117]HESHIMA HESHIMAAA
[emoji117]SEX


....... Inawezekana kabisa , wee unakoswa yote hayo. Au unapata sex lkn unakoswa eshima ,au vyote kwapamoja kwa wakat mmoja.

Huyo dem inawezekana kwao ndo mtoto wa kwanza( Wanakuaga ni Matatizo).



SERIOUS,,USIPOKUA MWANAUME, UTAKUFA SIKU SIO ZAKO.


Kitendo cha mke wako, kutopokea simu, anakuta missed call lkn hakujulish .......... Kwangu angekua kanipa sababu ya kuachana naye.

Ni dharau za kiwango cha Kimataifa.
Umenena vyema mkuu
 
Nimeyapima kwa mizani kubwa nimeona hayabebeki. Achana nae mapema tu kabla hujajiangamiza kwa maradhi yasiyoambukiza na ya kuambukiza pia.

Mimi nimesomesha mke na nimemuacha na sasa naishi kwa amani.
 
Usipofanya maamuzi magumu mtagawana Majengo ya serikali. Ni ama wewe utaenda JELA au Yeye Ataenda MOCHWARI. Nadhani umenielewa. Ndoa yenu imefikia Point of No return otherwise Ipo siku Mmoja atazikwa na mwingine ataozea jela.



Nakushauri Fanya maamuzi magumu.
 
A
Sijui kwann niliumbwa kwa akili ya kuchunguza... Ningekua mm kwanza ningekua nmeshachunguza uhalali wa hiyo kazi, wiki tatu , hapokei simu ,nkazi gan?? Kaenda na akina nan..kwann huongei nahao akina nanani.

Ningechunguza kiasi kwamba ningegundua kua,yupo kwa huyo mwanaume alokua anamuomba hela usiku wa manane.


AMINI AMIN NAKUAMBIA ,HAPA DUNIAN MAHITAJI MAKUBWA ANAYOTAKA MWANAUME TOKA KWA MKEWE NI
[emoji117]HESHIMA HESHIMAAA
[emoji117]SEX


....... Inawezekana kabisa , wee unakoswa yote hayo. Au unapata sex lkn unakoswa eshima ,au vyote kwapamoja kwa wakat mmoja.

Huyo dem inawezekana kwao ndo mtoto wa kwanza( Wanakuaga ni Matatizo).



SERIOUS,,USIPOKUA MWANAUME, UTAKUFA SIKU SIO ZAKO.


Kitendo cha mke wako, kutopokea simu, anakuta missed call lkn hakujulish .......... Kwangu angekua kanipa sababu ya kuachana naye.

Ni dharau za kiwango cha Kimataifa.
AKija wakacheki afya wezakuta ameenda kutafuta ada.
 
Kama unampenda mkeo jikaze mumsomeshe bwashee wako. Toa ushirikiano ndio mzigo wako huo .
 
Ndoa ndoa ndoa....ama Kushi na mke kuishi na mke kuishi na mke!
Mitihani saana.

Kuna wakati najihisi napata tabu za maisha kwa sababu niliwahi kuzaa na mwanamke.
Ukishazaa naye anakupeleka atakavyo mpaka ukome,bahati mbaya uwe na moyo wa huruma kama mimi! Utajuta.
Sema sasa hivi,nimekuwa jasiri... Hafurukuti
 
Mim mwenyew nataka kuachia ngazi na nikiachana nae sioi tena maisha yangu yote hawa viumbe kuishi nae unahitaji kua na moyo waziada sio huu wanyama tuliopewa na Mmuumba
Hahaaa yaan imebidi nicheke tu mkuu, wakati ni mambo sirias
 
Mimi ni mwanamke ila km usemayo kweli muache asije kukuletea ngoma bure.
Huyo kashindikana na familia yake nao wajinga kutetea uovu wa mtoto wao!
Hilo ni kweli kabisa kuna familia zinasapoti ujinga Wa watoto wao bila kuangalia mazara anayoweza kupata Mtoto wao,mim nimepiga chini mke kisa kama hiki alafu ndugu wanasaport umalaya Wa ndugu yao .sijui kwnn dunia umekua hivi single mama Na single baba watatawala sana kizazi hiki.
 
pole sana mkuu..duh..hapo naona tatizo ni moja kuu..
hakuna anayesali kati yenu wote...amini nakwambia piga goti tu ...
shetani kaingia, ni Maombi tu hapo , hakuna namna.
 
Tatizo lako ulioa 'ili msaidiane majukumu' yaani ulidhani mke atapunguza umasikini wako"
Unavunja ndoa kisa mke hatoi hela? Hebu fikiria upya assume ni mama wa nyumbani hudumia familia yako na mtoto uone hai ndugu wanaompa kichwa watafikia wapi.
 
Pole ndugu, ndoa ni gereza la hiari, ndio maana inaitwa "kufunga pingu" ukifungwa pingu unakuwa hauko huru, naona kama umechagua pingu isiyo zaiz yako
[emoji85] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kwenye ndoa kila mtu na mziki wake, sauti yake na ala yake [emoji23] [emoji23] [emoji23] dunia simama nishuke mie
 
Back
Top Bottom