Hebu tiririka kwa kirefu tujue tunakusaidiaje?
1.Hela ulizipata wapi
2.Bank ilikupa sababu gani za kuzitoa hizo hela?
3.kwa kosa gani ulifungwa?
4.Why USD na sio TSH?
5.Unataka kupewa msaada gani humu jf?
Tiririka kwa kuyajibu hayo maswali niliyokuuliza ili tujue wapi pa kuanzia.
Namiliki lodge yakulaza wageni kisiwan znz, so nikajiingiza kwenye system ya booking.com ili niweze kurahisishia wageni kutoka angle zote za dunia kufanya booking kwa urahisi sana, nikafungua bank acc na wakanipa ile POS machine na wateja wakawa wanafanya booking from all over the world, ikawa ndani ya muda mchache nimepiga pesa nzuri maisha yakawa safi, sasa baadhi ya wafanyakazi wa bank sio waaminifu walipoona pesa ni nyingi, wakazuia account yangu...
Nilipo kuwa hapa dsm bila kujua nilienda kutoa pesa ikawa nashindwa pata huduma ikanibidi niingie ndani pale HQ ya bank kuulizia mbona siwezi kutoa pesa na acc yangu inapesa...nimekaa naeleza tatizo langu...mara ikapigwa simu wakaja baadhi ya wafanya kazi wa pale pale bank ambao mm nawajua coz hiko kimachine ninachotumia ndio walinikabidh wao, wakaniambia niingie ndani, nikaingia wakaniuliza kwann unaiibia bank...nikawaambia mbona sijafanya wizi wowote ule na kama pesa booking zote c munaziona, so nani nimemuibia after that wakavuta simu kinyemela kuwatwangia polisi wakaja kunibeba kutokea pale bank bila maaelezo hadi msinbazi, pale napo nikaambiwa nimewaibia bank...
Nikawaeleza kama nilivyowaeleza hapo awali watu wa bank...sasa nilichokuja kugundua wale wafanya kazi walikula njama na polisi, wahakikishe sichomoki na niende jela baada ya hapo watoe pesa wagawane, wakafanikiwa kwa asilimia chache sana coz sikufungwa ila nilikaa bahabusu kwa muda wote huo nikawa natokea gerezani kwenda kusikiliza kesi yangu mahakamani nikapambana nipate zamana nitoke gerezani kwa muda wote huo nikapata dhamana sasa hivi natokea home kwenda kusikiliza kesi yangu, na ushahidi kwa upande wao wameshatoa kama nimewaibia ila ushahidi wenyewe haujitoshelezi wameshindwa kumleta mtu yoyote yule aliyeibiwa na mm, na mimi kwa upande wangu nimeshajitetea tayari so next month naenda kusikiliza hukumu itakuwaje, ila chakushangaza pesa zilizopo kwenye acc walikwara zote kwakuhisi sitoweza toka tena...
Ila chakushangaza kwann case kama nimeiibia bank case wafungue wafanyakazi wa kawaida na sio mwanasheria wa bank, na bank kama bank haijui kama kuna case inaendelea mahakamani kuhusu kuibiwa kwa pesa...Hivyo sasa nilikuwa nasubilia case hii yao iishe ndio nifungue yangu but naona imechukua muda mwingi sana haijaisha hadi hivi sasa....nikapata wazo niishtaki bank moja kwa moja kwa nn imetoa pesa zangu bila ya ridhaa yangu....sasa ndio najiuliza hapa na nataka kusikia kutoka kwenu hii issue imekaaje hapa...
NOTE: Bank haina taarifa kama inacase na mimi zaidi ya wale wale wafanya kazi na nimejitahidi kuonana na MD wao wale jamaaa wanafanya kila aina ya nia nisionane nae na wamefanikiwa kwenye hilo coz kila nikienda nionane na MD wananizuia wanataka niwaeleze wao kwanza nini shida wakishindwa ndio iende kwa MD...natumai umenielewa coz mimi kwenye kueleza majambo najihisi sio mfasaha sana