Nataka nijifunze uchawi, niwaadhibu wezi wa mali ya umma, maana CCM inakumbatia wizi kupitia ofisi ya DPP

Nataka nijifunze uchawi, niwaadhibu wezi wa mali ya umma, maana CCM inakumbatia wizi kupitia ofisi ya DPP

Myebusi Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2022
Posts
671
Reaction score
1,543
Sio huu uchawi feki wa Mshana Jr, nataka uchawi wa kuwaadhibù wote wenye dharau na mashauzi nchini.

Naanza na wale waliochota mahela ya umma na uchafu wao umeorodheshwa kwenye CAG report.

Siwatoi mabusha, nawamaliza kwa mateso makali.

DPP ni nani hadi anawakumbatia wezi wasichunguzwe na Takukuru?

Katiba ya mwaka 1977 ni mwiba mchungu kwa mlalahoi. Katiba imetengeneza tabaka la wanaokula neema ya nchi na wasio na tumaini.

Bila kuua hawa wezi wanaolindwa na mfumo wa CCM nchi haiwezi kwenda.
 
1681240100237.jpg
 
Sio huu uchawi feki wa Mshana Jr, nataka uchawi wa kuwaadhibù wote wenye dharau na mashauzi nchini.

Naanza na wale waliochota mahela ya umma na uchafu wao umeorodheshwa kwenye CAG report.

Siwatoi mabusha, nawamaliza kwa mateso makali.

DPP ni nani hadi anawakumbatia wezi wasichunguzwe na Takukuru?

Katiba ya mwaka 1977 ni mwiba mchungu kwa mlalahoi. Katiba imetengeneza tabaka la wanaokula neema ya nchi na wasio na tumaini.

Bila kuua hawa wezi wanaolindwa na mfumo wa CCM nchi haiwezi kwenda.
Naunga mkono hoja yako.. hii ndio dawa pekee iliyobaki njia zingine zote hazina matokeo.. hawa wanaoiba pesa za uma ni kuwaua tu kimya kimya..
 
Hata serikali ingeweza kutengeneza kikosi cha siri kuwamaliza wezi wa mali za umma. Nchi nyingi zenye adili, hufanya hivyo kuwaadilisha raia wake
Tanzania bado imelala.. ila hali hii ikizidi taifa la Tanzania litaangamia kwasababu ya tamaa ya hawa wezi wa mali za uma... hivi unaiba pesa zote hizo ili ukazifanyie nini, kwa faida ya nani ikiwa unaowaibia unazidi kuwadidimiza kwenye lindi la umaskini wa kutupwa.. nafikiri ifike mahala tufundishane adabu juu ya matumizi sahihi ya mali za umma.
 
Tanzania bado imelala.. ila hali hii ikizidi taifa la Tanzania litaangamia kwasababu ya tamaa ya hawa wezi wa mali za uma... hivi unaiba pesa zote hizo ili ukazifanyie nini, kwa faida ya nani ikiwa unaowaibia unazidi kuwadidimiza kwenye lindi la umaskini wa kutupwa.. nafikiri ifike mahala tufundishane adabu juu ya matumizi sahihi ya mali za umma.
Wanaenda kuficha nje. Mabenki ya nje yanazikopesha na kutengeneza faida
 
Unadhani rahisi rahisi hao jamaa huko ndo walikolalia yan huwez kalia kiti ofisini bila kupitia huko
 
Haaahaa unajidanganya.. Kama unaweza uzidi wa kano Nigeria na milima ya himalayas sawa
 
Vipi wewe ukidondoka? Mfumo unarudi kulekule.

Dawa ya mafisadi na wezi wa mali za umma ni nguvu ya umma kuwaondoa. Watanzania wengi bado hawana elimu na walioelimika wameshagawanywa (divide and rule).

Ipo siku nguvu ya umma itaamua. Kizazi cha miaka ya 2010s ndicho kitaleta mabadiloko.
 
Hao mafisadi ni hatari sana kwenye kuzindikwa .

Mbaya zaidi wanawaomba viongozi wa dini wawaombee mema

Hawa ingewezekana kama viongozi wa dini zote wangekua ni watu waadilifu wanaochukizwa na umaskini wa watanzania wengi kutokana na wachache kukwapua Mali za umma Kwa Kasi kubwa sana.

Mtu ANAIBA fedha za umma anakwenda Kununua Kiwanja Kwa Bei ya sh. Bil. 1. Cha nyumba ya kuishi na sio ya biashara.

Kama viongozi wa dini na machifu wa jadi na waganga wa jadi wangekataa kuwazindika na kuwaombea Dua njema wezi hakika Mungu angewaazibu na familia zao wote.

Mfano Shekhe mkuu, maaskofu, mapadri, waganga wa jadi ,machifu n. k. Wakiitwa kwenye Uzinduzi au hafla jambo la kwanza ingekua ni kuomba Dua zinazotamka uhalali na uadilifu wa viongozi uwe ni tunu ya Taifa letu na baraka Kwa vizazi vyetu wote.
Mungu atuepushe na viongozi wasio waadilifu . Mwenyezi Mungu asimame kuwatetea maskini ,wajane,yatima na Vijana wanaojiingiza kwenye vitendo vibaya kutokana na Umaskini unaosababishwa na wale waliopewa nafasi za ukuu kugauka na kuwa kama mbwa mwitu wakali dhidi ya Mali za Watanzania wote ambaza Mungu aliziumba Mwenyewe.

Mungu Muumba aliyeumba Mali asili nyingi Kwa ajili ya Watanzania wote na wachache wakapewa nafasi ya kuzisimamia ama Kwa kujuana au upendeleo wowote lakini wamekua juu ya Mali za umma basi wasipotenda haki kuzisimamia Kwa manufaa ya wengi basi nguvu za Mungu zisizoshindwa na yeyote zikawaadhibu wao na vizazi vyao ili iwe ni fundisho kuu Kwa vizazi vyote .

Mungu wa haki na Muumba wa vyote aheshimike katika haki na wema . Ajulikane katika haki na kweli, Mungu Muumba kama alivyowainua wakuu na wenye madaraka ili wasimamie haki na kuepukana na dhulma basi akawashushe mpaka chini wale wanaodhuluma Mali za umma na watu wengi kuishi maisha ya dhiki huku wao wakila na kusasa na kutupia mbwa wao wanaowafuga na kuwapa maisha makuu kuliko binadamu wenzao.
Kama vile Mungu alivyomwambia yule Tajiri aliyelimbikiza Mali Kwa dhulma na kuiambia nafsi yake kuwa Sasa umejijazia Mali pumzika ule na uifurahishe nafsa yako Kwa anasa za kila aina mana nina Mali za kutosha ,"Usiku wa Leo Malaika wanakuja kuchukua roho yako", iwe kwao pia wale wanaoiba Mali za umma walitegemea kuishi maisha ya Raha na amani na furaha. Usiku wa Leo Malaika wakasimame malangoni mwao kuzichukua roho zao.

Hakika watanzania wakifunga na kuomba Dua yoyote ya kuwatakia mema au mabaya wale wanaosababisha wanadamu wengi kuishi maisha ya dhiki kwenye Rasilimali alizoziumba yeye hakika Mungu atajibu.

Tatizo tumekua muda wote tukiwaombea Afya njema , ulinzi, usalama , na zaidi Kuna matamko ya kuwatakia maisha marefu ili Wazidi kututawala . Kumba maombi yetu yalipaswa yawe na Condition ya kuwa watutawale Kwa haki na kuepukana na ufisadi ,dhulma ,rushwa na wizi kwani ni vikwazo Kwa wanadamu wote walioumbwa na Mungu ili wafurahiye uumbaji wake na sio kulalamika kutokana na kunyimwa haki zao.

Kuwaombea mema viongozi waovu ni kuwasaidia kupata mazindiko na kuendelea kuiba Mali za umma Kwa Raha zao bila kujali mana Mungu hua anajibu maombi kama watu wanavyoomba . Mungu anatushanga mana hatujui mema na mabaya.
Ni kama Mtoto wako anapovunja glass mara ya kwanza ukamkemea ,akavunja themosi ukamchapa au ukamkemea vikali zaidi basi ni rahisi sana kuacha na kuwa makini mana atajua kuwa anachofanya ni kosa .
Hali kadhalika Kwa watawala wanapoiba Mali za umma tukawachekea na kubaki kuwapigia magoti kuwaomba misaada na kuwaombea Dua njema na afya njema hakika wanaendelea kufanya hayo hayo mana nafsi zao zinapata faraja.

Tunaweza tukawatafta viongozi wa dini zote waadilifu sana . Wasio na makandokando mabaya na wenye sifa njema , tukawatafuta machifu wa jadi wanye uwezo wa kutambika mvua ikanyesha. Tukatoa sadaka au michango kila mahali ikapatikana kama bil. 1. yaani watu mil.1 kila mmoja akatoa Elfu Moja tuu. Kisha tukawapa kila msoma Dua sh. Mil. 1. Wakafanya kazi hiyo kwa siku 21 yaani wiki tatu mfululizo. Waislam wakasoma Albadiri na wakristo wakasoma zaburi zinazoendana na kuwalaani watawala wanaomuasi Mungu katika nafasi walizopewa kusimamia vile alivyoviumba Mungu.
Wanyama pori hawakuumbwa na CCM Wala Familia za watu Fulani .
Mlima Kilimanjaro unaingiza mabilioni lakini haukuumbwa na CCM Wala watu Fulani na familia na marafiki zao.
Ardhi kubwa ya Tanzania haikuumbwa na Rais Wala familia ya marafiki zake Wala CCM .
Mito na misitu havikuumbwa na CCM Wala makada wake wanaojiona kuwa wao ndio wanaoamua nani awe juu na nani awe chini na nani aibe bila kuulizwa na nani Akiiba hata kuku aozee Gerezani.
Madini ,gesi, mafuta havikuumbwa na CCM Wala watawala waliopata utawala ama kihalali au Kwa dhulma lakini hawakuviumba Bali ni Mali ya Mwenyezi Mungu Muumba wa kila kitu na wao ni wasimamizi waliopata nafasi ya kuvisimamia Kwa haki ili wanadamu wasiomnung'unikie Mungu.
Wananchi wote hawakuumbwa na CCM(wakiwemo wale makada wanaosema CCM Ina wenyewe na wenyewe ni Sisi) Wala watawala Bali wote wakeumbwa na Mungu hivyo wanapaswa kutenda yake yanayomfurahisha Muumbaji wa vyote.
Jua , Mwezi, nyota, mvua, hewa ya oksijeni vyote hivyo sio Mali ya CCM Wala Chadema ya walamba asali Bali ni Mali ya Mungu Muumbaji wa vyote .
Hakika Mungu anapenda kuona Taifa likisimama katika hukumu za haki na serikali na watawala wakiwaadhibu Wahalifu wote bila kupindisha SHERIA . Vinginevyo Mungu Mwenyewe atasimama na watu wake kuwaadhibu waovu wote Kwa ghadhabu kubwa sana na wengi wataumia na kupote kabisa pamoja na vizazi vyao mana ili Mungu aogopwe na kuheshimiwa.
 
Back
Top Bottom