Nataka nijue kusoma Quaran

Gaidi mvaa kanzu fupi anapojifanya mkristo.
 
Qur'an ya Kiswahili ina nyongeza ya Shehe Abdallah Saleh Farsy. Maneno yote kwenye mabano hayapo kwenye original Qur'an ya kiarabu.
 
Hongera sana mkuu, Nikupe moyo juu ya hilo. Binafsi kabla sijakuwa Muslim nilikuwa na imani mbaya sana juu ya hii dini, Nilianza kuifatilia kwa undani zaidi hadi nafika kidato cha 5 nikajikuta rasimi naipenda sana na kuamua kuwa Muslim. Hadi sasa nmeweza kujifunza mwengi sana na nmehifadhi baadhi ya Aya bila hata kutafuta mwalimu wala kwenda madarasa.

Ushauri wangu ni kwamba kama una nafasi ya kutosha weka juhudi ya kutaka kujifunza na adhimia kujifunza, pia tafuta mwl akuelekeze, Ndan ya miez 3 utakuwa mbali sana.
 
Qur'an ya Kiswahili ina nyongeza ya Shehe Abdallah Saleh Farsy. Maneno yote kwenye mabano hayapo kwenye original Qur'an ya kiarabu.
Tafsiri ya Qur'ani ni pana sana ndyo mana akasema hivyo kwa lengo la kuweka sawa.

Mfano akisema

هي (hiya ) kwa maana ya yeye lakini ni yeye mwanamke.

Hivyo anaweza tafsiri kama YEYE (mwanamke) hapo huwezi sema katia nyongeza kwa sababu bado neno la kwenye mabano linarudi katika maana ya neno husika,hakuna kuongeza hapo...

Kiarabu ina maana pana sana.

Mfano kuna aya zimeanza na amri ya قل QUL (SEMA) lakini hapo anakusudiwa aseme huyo aloteremshiwa Quran ambaye ni mtume muhammad sala na salama ziwe juu yake.

Hivyo akiandia hivi

قل kwa maana ya "sema(ewe muhammad) hapo hakuna nyongeza kwa sababu ni katika mlango wa kulifasiri neno hilo kwa upana wake..
 
Download Quran app kwenye Google play.uisome na uifuate.soma pia Bible hasa vitabu vya kiunabii agano jipya na pia zingatia mafundisho ya yesu maana nu mwalimu Bora njia kweli na uzima
 
Nakuomba tu usome Biblia maana koran ni summary ya Biblia.
 
Kwa maeneo aliyopo sina uenyeji nako labda nifanye mpango niwasiliana na Baadhi ya wanafunzi wa maeneo hayo kama atakuwa tayari ni mpe namba za walioko huko wakamuelekeze sehemu salama ya kusoma.

Naogopa asije akasoma kisha baada ya mwaka anakuja kusema waru wavae mabomu wakajiripue kuua makafiri.

Hizi fikra hizi nazipiga vita kukicha ndyo maana napenda akajifunze sehemu salama.

Nakumbuka kuna sehemu nilikuwa nasoma elimu ya hadithi basi kuna haduthi moja bhana inasema

الدنيا سجن المؤمن وجنة الكافر dunia ni jela kwa muumini na dunia ni pepo kwa kafiri.

Basi yule mfundishaji akasema "si mnaona leooo waislamu wanateswa,lazima tulipe kisasi,mashekhe wanafungwa n.k"

Nikasema huyu atanivisha mabomu siku sio nyingii...nikasepa zangu mie
Mwelekeze mtoa mada wapi atajifunza Quran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…