lukubuzo Samsis
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 2,920
- 3,388
Gaidi mvaa kanzu fupi anapojifanya mkristo.
Heshima kwenu wakuu, mimi ni kijana (miaka 26) mkristo ambaye hivi karibuni nimefatilia kiundani sana dini ya uislamu na nimetokea kuikubali sana.
Moja ya sababu zilizofanya niipende dini hii ni kwamba lugha inayotumika ni ile halisia iliyotumika kuandika hii quaran, Napenda sana napokua kwenye dini nisome kwa maandiko orijino, kusiwe na kitu ambacho kimeongezewa wala kupunguziwa, wala kutafsiriwa. Kuna makosa madogo katika tafsiri ya lugha iliyotumika kwenye maandiko ya kihebrania ya biblia mfano biblia zetu zilizotafsiriwa zimeandika mama yake Yesu alikua ni bikra na ndicho wengi huamini ila biblia orijino ya kihebrania imeandika kwamba mama yake yesu alikua ni mwanamke mdogo anaeweza kuzaa, Kwa vile hapa Tanzania ni nadra sana kukuta madarasa ya kibrania Ningejaribu mbali kujua kihebrania ila jitihada zingegonga mwamba kwa sababu nilifatilia kwamba kwamba huko israel dini ya ukristo ni asilimia 2 tu wanaoiabudu tangu ilioruhusiwa mwa juzi (2016) ambapo wengi huabudu judaism na uislamu.
Ukristo ni dini nzuri tu ambayo imenilea mpaka hapa nilipo na kila napopata tatizo mungu amekuwa msaada sana kwangu nikiwa katika dini ya ukristo, Sitasema kwamba dini ya ukristo sio nzuri, LA HASHAAA!!!,
Zipo sababu nyingi mno zinaonifnya nihamie kwenye uislamu kutoka ukristo ambazo nikiziweka wazi patatokea malumbano yasiyo na mwisho.
Kwa sasa familia na ndugu zangu wote ni wakristo na sitapenda kuhama ghafla, nataka nipate mwanga wa elimu ya kiislamu kwa kusoma kiarabu ili nispate shida kusoma quarani.
NAOMBENI MNISHAURI MAMBO MUHIMU KUHUSU ELIMU YA LUGHA YA KIARABU ITAKAYONISAIDIA KUSOMA QURAN, NI VITU VIPI INABIDI NIJIFUNZE ILI NAPOANZA KUSOMA QUARAN NA KUINGIA RASMU KATIKA DINI YA UISLAMU NISIPATE TAABU.