Nataka nikanunue bodaboda mjini, nizingatie yapi nisije kuuziwa mbuzi kwenye gunia?

Biashar ya pkpk nimefanya mpaka sitaman,,mara kashikwa na trafik anakuambiaa na akikuambiaa week ikifika atakupa kidogoo ,,pkpk moja nmetoaa kwa mkatabaa wa mwakaa ,kamaliza mwaka nikawa namdai kama hela ya week 24 ,,mpaka sasa ni kama mwaka na miez sabaa ,bado namdai lak nne hapo majanga yakimkuta hakup ,inafka kipnd anakuambia mtoto wake mgonjwa kila tatzo likitokea anakuambiaa

shushushu VIP
 
Hkkisha wanakupa
Kadi ya pkpk..inakuaga ktk jina la kampuni au hapo uliponunulia
So ukipewa hkksha kesho yake unaenda tra kubDilisha jina ili iwe na jina lako bnfsi
Thn hkksha unakata insurance either ndogo au kubwa
Yapo makampn mengi ila kwa uchche ni reliance, bumaco etc
Thn kama huko kwenu kuna umoja wa bodaboda na wanatoza ada ya uanachama thn ni vzr ulipie na huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran bro, ila huko kubadilisha jina wanatoza bei gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi kwa upande wangu hii biashara ya bodaboda achananayo kabisa.Hutapata pesa na kikubwa utakachoambulia ni patupu.Katika biashara kichaa hapa Tz ni kununua bodaboda ukampa mtu ili utegemee akuletee pesa.Sikushauri ila ukitaka kununua zingatia unapata kadi ya pkpk ,risiti ya efd na ifanyie matengenezo ya awali kwa matumizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umechanua vizuri,Ila umesahau kua baada ya mapato hayo ya mwaka mzima still bodaboda inakua Mali yako,ambapo kama ulibahatika kudum nayo 1 yr ukiiuza pia faida inaongezeka maradufu,
Ila,tahadhari iwepo kwenye loss pia,hv ni vyombo vya moto,kuna kuibiwa,kuna ajali n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ukimaliza Kuinunua hakikisha pia Chenji itakayobaki basi unajinunulia Jeneza lako zuri tu kwani tayari Tiketi maalum ya kukufanya ungie humo Jenezani umeshaipata Mkuu.
 
Kama ungegeukia kilimo Mkuu ndani ya miezi mitatu unakua mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Biashara ya kichaaa iyo. Wakulima wengi hawajatoka kimaisha, unamshauri akalime tumia akili.
Kama wewe kilimo kimekulipa onyesha vitu ulivyo vipata kupitia kilimo.
Mnachukulia kilimo kama kazi ya kukaa kwenye kiyoyozi
 
Maelezo ktk paragraph ya mwisho ndio itakuwa anguko lako. Mungu aepushe. Hawa jamaa wa bodaboda Si wa kuwapa Uhuru huo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nimependa sana mchanganuo wako...vipi kwahiyo pesa unaweza mshauri afanye biashara gani nje ya bodaboda
Kama ataweza. Kama ataweza. Msimu Huu wa mavuno, anunue mahindi na kuyahifadhi mpk January or February. Kipindi hicho njaa huwa imetamalaki na price huwa ni mara mbili au zaidi ya bei alonunulia. Soko kwa kipindi hicho sio tatizo.

Changamoto ni sehemu ya kuhifadhi na dawa za kuyasitiri mahindi dhidi ya wadudu.

Kwa vijiji vya Mpwapwa, maeneo ya Gairo na Kibaigwa, 2.4 m anapata Si chini ya gunia 40.

Mwaka Jana, January to March, gunia la Mahindi lilifika mpk Tshs 140,000.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simpo tu badala ya kuweka 2.4 zote kwenye pikipiki moja mpya gawa mzigo katikati tafuta boxa used mbili jwa watu nunua izo na uhakika utapata faida mara mbili,

mi naamini chombo cha moto ni matunzo kinaweza kudumu miaka mia hata kama ni used

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri sana mkuu nimejifunza kitu
 
Milioni 2. Pamoja na vibali au inakuwaje? Na jee? Ulaji wa mafuta upoje ukilinganisha na BM 150 Boxer-150
Pamoja na vibali mkuu,ila wewe itabidi ukabadilishe jina la mmiliki yani liwe lako kwa sh 37,000 pia ulaji wa mafuta TVS-124.7cc, boxer 150cc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bodaboda inamlipa yule anayeinunua nakuifanyia biaahara mwenyewe,kitendo chakumkabidhi mtu aitumie awe anakuletea pesa ni majanga,huwa kunakua usumbufu hovyohovyo na pesa haipatikani.


Mimi niliwahinunua hiyo bodaboda aina ya SANLG,kwakweli ilinitesa sana,mara niambiwe boss nimekamatwa na trafiki,mara mvua imenizuia kufanya kazi,mara nini,hela hamna kabisa,wiki hii unapewa pesa,wiki ijayo hupati.

Sasa hivi mwezi ujao nanunua bodaboda nyingine lakini ntaifanyia kazi mwenyewe eneo la chuo cha UDOM kwakuhakikisha nakua na wateja wangu permanent 50,wengi wao akina dada wale wavivu wakwenda kufuata chips au vyakula vingine sehemu moja inaitwa kwa WAJAS,nina uhakika nitakua nalala na sio chini ya 30,000/= na ntakua nafanya kazi siku saba za wiki.Ninao uhakika wakufikisha si chini ya laki nane au tisa kwa mwezi kwasababu ya idadi ya wateja nitakaokua nao pale.

MUNGU nisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…