Nataka nimchome kwa ndugu zake

Sasa mchumba wako analiwa na ww unachekelea? Au na wewe unataka kuukalia
 
Usiwe sababu ya kuvunja undugu wa watu, dhima yake ni kubwa sana kwa Mungu. Huyo binti si mkeo, usimuonee uchungu kiasi hicho. Shukuru Mungu umejua tabia zake mapema kabla kumfanya mke. Kama anaweza kulala na mume wa dada yake hatoshindwa kulala na kaka yako. Piga chini.

Kumbuka ukisanua unachojua athari haitokuwa kwake tu. Utavunja udugu wake na dada yake, utavunja ndoa ya dada yake na mumewe na pengine kuleta mtafaruku katika familia nzima. Sasa huoni kuwa utakuwa unaadhibu wasiokuwa na hatia.

Za mwizi daima ni 40, kama dada yake anajua kuna kukutana baina yake na shemeji yake basi ni swala la muda tu atawakamata na hapo hutokuwa na lawama yeyote hata wakiuana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ