Nina mchumba wangu ambae sasa tuna miaka mitatu nikiwa nae ila mienendo yake inaanza kunitia wasiwasi sana na kuna vitu nimeshabaini kwake.
1. Kuna shemeji yake ambaye kamuoa dada yake mkubwa anamtaka na wana mawasiliano ya karibu hadi kamtumia kiasi cha pesa mara kadhaa jumla haiwezi kupungua laki mbili na wanakutana mara kadhaa na huwa haniambii mpaka nijue kwa jitihada zangu au mpaka dada yake amtukane kuhusu swala la kukutana na mme wake bila taarifa yeye kupata maana nahisi kama kahack simu ya mumewe.
2. Mara zote nikimuuliza kuhusu ili jambo anakua mkali sana na kufanya kama vile mimi simuamini ilihali anasema ukweli na mambo mengine mengi ambayo yananifanya nimchome kwa ndugu zake.
NB: Kuna mambo ambayo mimi nayajua mengi na nikimwambia dada yake lazima tu apo litokee jambo kubwa sasa nawaza apa nimchome ili kila mtu akose kila kitu maana mimi hilo nilikua nalisamehe ila bado kuna la ex wake kwaio nataka nimchome naombeni ushauri wenu wakuu.