Nataka niunde chama ambacho kitawaenzi hayati Baba wa Taifa JK Nyerere na hayati JP Magufuli

Nataka niunde chama ambacho kitawaenzi hayati Baba wa Taifa JK Nyerere na hayati JP Magufuli

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Baada ya kuona wanaodhihaki kazi nzuri aliyoifanya Hayati JP Maguli iliwemo miradi mikubwa ,kutufikisha uchumi wa kati ,kutatua shida za wanyonge waliyokuwa wamedhulumiwa haki zao,kupambana na rushwa nk nataka wazalendo tuunde chama ambacho misingi yake itakuwa ya uzalendo uliyoonyeshwa na Hayati Baba wa taifa JK Nyerere na Hayati JP Magufuli.

Chama hiki kitapamabana na CCM mafisadi wanaojaribu kuonyesha kuwa Hayati JP Magufuli hakufanya kitu (wanabweka baada ya Simba kufa) na upinzani uchwara uliyekosa ajenda na kudandia kushabikia kifo cha JPM.

Wazendo naomba jina la chama hicho kipya tafadhali.
 
Unapoteza muda tafuta kazi ya maana ufanye! Wengi tunakubali kuna mazuri mengi Hayati JPM amelifanyia Taifa hili kama vile viongozi waliomtangulia.

Ila ukweli ni kwamba kuna mambo mengi pia ya hovyo Hayati JPM alifanya katika uongozi wake ambayo ni lazima yarekebishwe kwa ustawi wa Taifa letu!
 
Hao unao taka kuwaanzishia chama hawafanani kwa chochote kile

Nidhambikubwa sana kumuweka magufuli na nyerere kundi moja hiyo ni dhambi kubwa sana sana sana
 
Wazalendo ndio akina nani? Si ni kila mwanaCCM tuliambiwa ndiye mzalendo wa nchi hii na yeyote asiye mwanaCCM ni msaliti asiyepaswa kuishi? Kwani hakuna wanaCCM?
 
Usiunde chama maana chama ni jina watu ndio mtaji..... unaweza tumia vyama vilivyopo kufanikisha hilo
 
Back
Top Bottom