Nashukuru mkuu kwa ushauri wako,hata kama nikijituma vilivyo haita saidia?
si kwamba nakukatisha tamaa..ila unadhani ukifika darasani ukaambiwa differential equations, complex number, trigonometric ratios, integrals, differentiation je utapata kitu? na je ni chuo gani wataweza kukusajili? na kama ulikua unapenda maths kwa nini hukuendelea advance????
ndugu yangu ukifika chuoni jua hesabu haitakua ile ya form 4...chuoni ni pure mathematics tu!! na sio kwamba nakukatisha tamaa ila huo ndio ukweli, anyway labda waje wengine wanaojua zaidi hasa jinsi mtu ambaye hasoma maths advance akaenda kusomea degree ya hesabu chuoni!!
Mkuu nashukuru sana na nazidi kupokea maoni yenu,kuhusu majibu ya maswali yako ni hivi;Huko kwenye diploma umesoma hesabu? Kama hujasoma, msingi wako wa hesabu sio mzuri sana kiasi cha kuweza kuhimili mikiki ya chuo kwa ufanisi. Ila kama umeamua unaweza, kinachotakiwa ni juhudi na pia kumbuka hesabu ni mazoezi zaidi, kwa hiyo ukifika chuo inabidi uhakikishe haipiti siku hujafanya hesabu.
Kwa upande mwingine umeshajiuliza unataka kusoma hesabu ili iweje? Yaani ukishasoma halafu ndio inakuwaje? What is your ambition in life?
Habari zenu wana JF naombeni ushauri;nahitaji kusomea BED in mathematics ila sijasomea hesabu form 6, nimesoma o-leval nilipata C ya hesabu kwani nilikuwa naipenda sana hesabu mpaka leo bado naipenda,ila watu wananishauri kwamba nisisubutu kusomea hesabu chuo kikuu kwani ni ngumu. Nina diploma ya Human Resource Mgm(1st class) nilitokea moja kwa moja frm 4 sikupitia frm 6,ila nimepania kusoma kwa juhuudi hiyo hesabu.Naombeni ushauri wenu wa aina yeyote nitaupokea kwa masomo ya degree hususani yenye hesabu nitafurahi zaidi.
Nawasilisha.
Yaani ukishasoma halafu ndio inakuwaje? What is your ambition in life?
Mantiki nzima ya mada hii nadhani ingejikita kwenye maswali haya. Anataka kusoma HISABATI ili awe nani?
Form six!!!! Hesabu ya form six na chuo hazina tofaut sana ila tofaut ni jinsi mhadhiri na mwalimu wanavyofundisha. Form six wanaelewesha sababu wanaamini hakuna anaejua chochote kwenye topic husika lakini chuo wanapitiapitia juu juu wakiamini wote walisoma form six hivyo ni marudio tu...
Fanya usome ya form six ili iwe rahisi chuo otherwise utateseka sana na utaishia kupata makarai (C) au supplementary kabisa.