Natakakusoma hesabu chuo kikuu bila kupitia form iv

MKUU ACHA KABISA ILE KITU PURE MATH usipime ondoa wazo hilo
 
Mkuu amekwambia BED in MATH muurumie mwenzio tuliopita tumeyaona bana inabd haende kufundsha Math hata form six huyo akimaliza . hapo ni PURE Math
 
Mkuu amekwambia BED in MATH muurumie mwenzio tuliopita tumeyaona bana inabd haende kufundsha Math hata form six huyo akimaliza . hapo ni PURE Math
Naelewa mkuu ila wahenga walisema penye nia pana njia. Kama vipi anaweza kukomaa ila ndio hivyo juhudi za ziada zinahitajika.

Ila mimi siamini kama hesabu ni ngumu. Ni msingi mbovu tu kwa wanafunzi wengi.Ulishawahi kujiuliza kwa nini nchi Asia wanafunzi wengi sana wanajua hesabu kuliko nchi zetu za Afrika?
 
MKUU ACHA KABISA ILE KITU PURE MATH usipime ondoa wazo hilo

Duh! Haahaaa amakweli kbmk umenipa donge zima zima itabidi nilimeze hivyo hivyo bila kupepesa macho.
 

Ni kweli nilizianda hizo juhudi za ziada kwani hata mi akilini naijua pure si mchezo,ila tatizo linakuja kwenye suala ulilosema kuwa waalimu wetu wanaojua hilo somo jinsi wananavyojiona! Hapo ndo ishu.
 
Mkuu math ngumu imebeba sheria ndani yk anae jua math manake anajua sheria hizo, ili kuzimasta inahitaji mda ndomana kuna pre request mfano huwezi kusoma Differential EQN kama hujajua integration na differntn. Hivyo ikipigwa hiyo tuna integrate na ku differnt juu kwa juu sasa kaz kwa yule asiye jua yaan ataumia ELIMU KWAKE ITAKU MATESO KUNA STATISTIC KULE BANA WEEE taumia huyu haloo ataumia
 
sasa muda unatofautiana kuna watu wanatumia muda mfupi tu kumaster hizo kanuni na unaweza kukuta huyu ni mmoja wapo. Math kawaida sana, watu mnawaogopesha sana wanafunzi. Yaani hesabu ni kati ya masomo ambayo unaweza kuambiwa kuna test muda wowote halafu hushtuki maana kanuni ni zilezile. Halafu hakuna kuonewa kule, ukipatia umepatia na ukikosa umekosa. Very straightforward!! Ndio maana mimi naona ni rahisi tu kama ukifuata utaratibu mzuri wa kukomaa nazo.
 
HIKI ni spesho kesi kule wamesha andaliwa mazingira ya kufundshwa A to Z
hongera sana wote waliokushauri hawana uelewa mzuri ST. JOSEPH UNIVERSITY WANATOA BACHELOR OF EDUCATION WITH MATHEMATICS KWA WALIO MALIZA FORM FOUR NA KUPATA C KWENYE HESABU....CHECK WEBSITE YAO
 
hakuna bana inabd aambiwe ukweli ajue ingekua rahc km unavyosema A za math olevo zisingepotea advance najua zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi wanao soma PCM vipaji wana A za za olevel yakija ya advance nenda necta ukaone isotoshe pale UDSM (Coet) kakataliwa mtu kusoma engineering sababu YEYE kasoma BAM tu
 
Mkuu mimi ni mhitimu wa Bsc. Mathematics. Si kweli kuwa hesabu za form six na chuo hazina tofauti sana. Kule ni deep sana. Nikupe mfano, kwenye complex number tulikuwa na lecture sessions 15 ila kwenye session ya kwanza tulimaliza complex ya six, zilizobaki balaa, tuli integrate mpaka complex number!! Kuna topology, functional analysis, ambazo hazipo six. Elimu ya form six ni muhimu sana. Bila form six asijidanganye kufanya maths chuo kikuu.
 
kama umejipanga kapige usiogope kk ila nakushauri uchague serikalini

Serikalini chuo gani atapata bila six? Cha kumshauri dogo ni kuomba St. Joseph. Pale kwa waliomaliza form four wanapiga degree miaka mitano( of which miwili ni ile ya six). Ila vyuo vya serikali hata mature age hawaruhusu kozi zenye maths na science
 
waambie bana wasimpotoshe mwenzao engineering math tuliyopiga Coet pale udsm ilikua ishu yaan olevel aambui bana utatokea wap kwanza kukomaa sawa lkn c kivile bana
 
waambie bana wasimpotoshe mwenzao engineering math tuliyopiga Coet pale udsm ilikua ishu yaan olevel aambui bana utatokea wap kwanza kukomaa sawa lkn c kivile bana
Sasa kwani yeye anaenda kusoma Math ya Coet??? Acheni kumtisha bwana, mimi nimesoma pure na chuo nimekula namba sana tu bado sijaona ugumu wowote.
 
Nimesoma BED SCIENCE Mwenge Univeristy, Physics & Mathematics (2012), hutoweza kusoma hesabu chuo kikuu kama hujasoma pure a'level,Nakushauri uking'ang'ania utajuta kuzalia, kuna kitu kinaitwa differential eqn,complex number, ni hatari, zile za a'level ni cha mtoto kabisaaaa, pls ucjalibu kwa ushauri zaid mrjulius86@gmail.com
 

mkuu pole sana, kama unahamu ya kusoma digree ya hesabu kweli nakushauri uanze kidato cha sita, la sivyo utarudi nyumbani mwenyewe bila kuambiwa!
 
usituongopee bwana wee alafu hujui uhusiano wa coet na Math kwanza, kwan yy ataenda kusoma hesabu za kutoka mbinguni? Ile math ya coet ni kama option lkn hawezi vp yule anaeenda kusoma afundishe wenzake Math?
Sasa kwani yeye anaenda kusoma Math ya Coet??? Acheni kumtisha bwana, mimi nimesoma pure na chuo nimekula namba sana tu bado sijaona ugumu wowote.
 
usituongopee bwana wee alafu hujui uhusiano wa coet na Math kwanza, kwan yy ataenda kusoma hesabu za kutoka mbinguni? Ile math ya coet ni kama option lkn hawezi vp yule anaeenda kusoma afundishe wenzake Math?
Sijaongopa sehemu yeyote. Sijasema najua uhusiano wa Coet na Math na pia nilisema kule juu sijui aina ya Math inayofundishwa BAED ila pia nilisema kama ni pure basi jitihada za ziada zinahitajika. Sioni umuhimu wa kulumbana hapa kwa sababu wewe kama unaona hesabu ni ngumu hiyo ni juu yako huwezi kulazimisha na mimi nione hesabu ngumu!!! chukulia unakutana na mtu anakwambia kuimba ni rahisi sana kwa kuwa yeye anaweza na anaamini hivyo halafu wewe uanze kumbishia eti ni ngumu hivi atakuelewa. FYI mwaka niliomaliza mimi A-level niliongoza kwenye Advanced Mathematics Bongo nzima so go figure na nimesoma hesabu kwenye nchi ambazo hesabu ni kama chai tu.
 

Ndugu yangu wala usijaribu.Utaweza mikiki ya akina Prof.Masenge sijui bado yupo au hapana??Maana hata kama advance ulipata A hapo unaenya na hesabu zake za double integral na calculac we atu ty
 
Mkuu, mimi nimesoma hesabu chuo kikuu. Kikubwa ni kwamba, hesabu inahitaji strong base. For sure, hawezi kusoma zile kama hajapita six. Ila nilishauri akasome St. Joseph, miaka mitano kwa mhitimu wa form four(of which two years ni zile za advance)
 

Ila angekuwa amesoma walau Additional Maths O'level, atleast ingesaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…