Natamani aende kwao tu....

Natamani aende kwao tu....

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Yani full tafrani home, ana wiki ya pili sasa yani nimeshamchoka huyu ndugu, kafika home kututembelea lakini full kutupangia ratiba za kuamka , leo kaamka mapema kaanza kutia makelele amkeni amkeni

Usafi mtafanya SAA ngapi? Wakati sisi tuna ratiba zetu za usafi, kila mtu akiamka ana kazi yake ya kufanya. Hadi jinsi ya kuvaa nguo anatupangia,yeye muislam anataka wote tuvae minguo mirefu kha hapana!!! kwakweli natamani aondoke ata kesho ana kazi ya kusemana tu, hadi kufatilia jikoni jinsi unavyopika..."

Jana kaniita akidai ana shida anataka tuzungumze nikamwambia sawa, mada yenyewe sasa ni kuhusu mavazi yangu ety nisivae suruali" Leo nimevaa sketi ndefu ananambia napenda uwe unavaa hivi kila siku!!! kwani mimi ni mtawa wa st fransis.
 
Yani full tafrani home,kuna ndugu kafika home kututembelea lakini full kutupangia ratiba,za kuamka hadi jinsi ya kuvaa nguo kwakweli natamani aondoke ata kesho ana kazi ya kusemana tu, hadi kufatilia jikoni jinsi unavyopika.......
Mmemdekeza mchaneni au niite mimi, kwani kaleta nini ambacho nyie hamna ?tuanzie hapo!
 
Itakuwa huyo ni bibi yako mzaa baba au mama...amekuja na kugundulika hapo kuna malezi ya hovyo! Hamfamyi kazi,wavivu, mnavaa nusu uchi..mko huru sasa bibi ameamua kunyoosha.

Alafu wewe ndie utakuja kuwa mke wa mtu!
 
Mwanaume huamka saa 10 alfajiri anatoka nje anafanya mazoezi ya mwili kisha usafi wa nyumba, saa 11 anafanya usafi wa mwili na 11:30 anatoka kwenda kazini ikiwa pamoja na biashara.

Mwanaume aliyekamilika havai vimodo, vijora au vikuku, inawezekana ndivyo mlikuwa mkivaa ndiyo sababu kaamua kuwarudisha relini, mshukuru sana badala ya kumleta huku tukutetee.
 
Mwanaume huamka saa 10 alfajiri anatoka nje anafanya mazoezi ya mwili kisha usafi wa nyumba, saa 11 anafanya usafi wa mwili na 11:30 anatoka kwenda kazini ikiwa pamoja na biashara...
Wanawake wenyewe waoga hawa ndio wa kuamka saa kumi kweli?
 
Back
Top Bottom