Natamani kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani ajengewe sanamu

Natamani kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani ajengewe sanamu

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Naandika haya nikijinasibu kutokuegemea kwenye dini yeyote au zozote zilizo katika dunia yetu hii pendwa ndogo sana inayoitwa Earth.Nimesema dunia yetu ni ndogo sana maana ni kama punje tu dhidi ya sayari zingine zilizo angani kama Jupiter.Dunia ni kama punje ya mtama dhidi ya mpira wa basket ball kwa Jupiter na Jua letu.Mungu akiamua kuiangamiza ni sekunde chache.

Namuunga mkono sana kiongozi wa nchi ya Quatar kwa jina la Tamim bin Hamad Al Thani kwa msimamo wake kwenye kombe la dunia kutokutaka mambo ya kimagharibi yasiyofaa kuingizwa nchini kwake.Kwa kawaida mgeni ukikaribishwa popote hata kwa rafiki yako huwezi kwenda na sheria zako ni vyema ufuate kanuni na masharti ya unapokwenda.

Nchi za magharibi zimekuwa na tabia mbaya sana kujaribu kueneza tamaduni zao ambazo haizifai kabisa katika nchini zingine na kujaribu kuzilamisha kuzisambaza katika nchi zingine kwa nguvu mfano mapenzi ya jinsia moja,wanaume kusuka nywele,kuvaa hereni kwa wanaume,wanawake kuvaa suruali mbano,kuvuta bangi.

Tabia hizi ni chafu mno kibaya zaidi nchi za Africa tumekuwa tukizi copy kuona kwamba ndio tamaduni bora.Wakati mwingine na mara nyingi wanatumia kigezo za usawa wa kijinsia kupenyeza mambo ya machafu vijana wetu siku hizi wameharibika sana.

Kibaya zaidi siku hizi kuna dada zetu wanakwenda kanisani wamevaa mavazi yasiyo na staha kabisa vimini vyenye mpasuko bahati nzuri kwa wenzetu waislam hili halipo.

Nchi za magharibi wana mpango wa kupenyeza mambo ya kumpinga kristo kwa kupitia Freemason.Makanisa siku hizi mengi yamegeuka kuwa sehemu ya biashara siku hizi kuna manabii hata wanawake badala ya kumcha mungu yote haya yanashabikiwa na nchi za magharibi kwa nchi za kiarabu kwa kweli hakuna upuuzi kama huu na ndio maana wana misimamo mikali sana tunawaona washamba lakini wanafanya kile wanachokiamini kiko sawa.Kuna mpango unaitwa new worl order ambao shetani ndio kinara wa kuleta mambo yote haya machafu yote haya yanaletwa na nchi za magharibi.

Pombe inakatazwa uwanjani kwa vile ni nchi ya Kiarabu ni kosa lakini Ufaransa na Ureno kuna sheria ya kutokutumia kileo wawapo uwanjani.

Namuunga mkono kiongozi huyo na nchi zetu na nchi zingine tunatakiwa tuwe na misimamo yetu.Cha kujiuliza mbona nchi za magharibi wao hawaigi tamaduni zetu za kiafrika bali tunaona zao ni nzuri ambapo ni za hovyo mno hata mungu hapendi hizo tamaduni.

Nimeamua kuweka picha mbili za kiongozi huyo moja akiwa amevaa kutokana na tamaduni za dini yake na ingine akiwa amevaa suti na tai akiwa kwenye mkutano huko Ujerumani nimeweka picha hiyo nikiwa na maana suti ni kweli ni vazi la kimagharibi lakini ni vazi la heshima ndio maana waarabu wanalivaa sio watu wafikirie waarabu ni kanzu tu na barakashia.

emir.JPG
quatar.JPG
 
Mambo ya mtu kujengewa sana ni kinyume na Uislamu,kama pongezi basi anastahili kwa mazuri yake.
 
Back
Top Bottom