Natamani kujua kinachosababisha umasikini kwa vijana wasomi

Barugize

Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
43
Reaction score
22
Habari za Muda huu wana JamiiForums.

Mimi ni kijana mjasiliamali kwa muda wa mika 10, kuna mambo huwa najiuliza kila siku nikiwa peke yangu sasa leo nimona ni changie na wana JamiiForums wenzangu.

Suala la Umasikini na Utajiri.

Kwanini vijana wengi hususani Wasomi ndio wanao hangaika sana kwenye masuala ya Uchumi, fedha na itajiri.

Utamkuta kijana mwenye umri wa miaka 28 hadi 39 ana shinda sana ya kifedha ili hali ni Msomi na ukute amesoma masomo ya Uchumi, Biashara lakini unamkuta anahangaika sana kifedha.

Pia, nikijaribu kuchunguza Vija wenye Rika kama hilo wasio wasomi naona wanamashi mazuri na wana endasha magari, wana nyumba zao na wanasomesha watoto wao shule nzuri.

Je, Shule zina sababisha vijana kuwa tengemezi kwenye suala la Utafutaji au au kuna tatizo gani?

Pia, kuna hii tabia ya Wasomi kupenda kufanya Biashara: Tatizo linakuja kwamba wasomi wengi wana taka kuanza bishara yenye mtaji mkubwa, utakuta kijana anakwambia nikipata milioni 10 naweza fanya biashara.

Naombini ufafanuzi kwanini wasomi wengi wanajikuta kwenye wimbi la umaskini kuliko walio ishia Darasa la Saba?

"JAMANI NIMEAMUA KUANDIKA TU"
"UTANI KWA WASOMI WENZANGU"
 
Umeuliza swali zuri sana Ila ili kujibu hili swali mtu inabidi awe ametulia sana maana zitashuka paragraphs za kutosha hio essay yake ni ndefu sana km proposal ya kugombea mkopo bank, nitakupa jibu dogo TU sababu ni UNYONYAJI
 
Wanawasaka wakuwafaa kwa usiku mmoja hawawaoni
Usifanye mchezo bro zebidi toto mwendo wa pini
Kosa kumuachia dakika moja cross kumi

Lakini si ma-hardcore, mwendo wa chama sado
Tuendelee jirushe mchezo uishe bado
 
Matarajio makubwa.

Hii ndo changamoto yenyewe, ukiondoa hii utaishi maisha yako hatua kwa hatua..mafanikio mwachie Mungu pambana kwa nguvu na wakati wako. Usipokua na matarajio makubwa sana huwezi kujiona unafeli sana .... kuepuka mitandao ya kijamii pia, mana ndimo zitokako chemichemi za kuona hufanikiwi kwakua wenzio unaona wanaishi maisha ya matarajio yako,hii inaua sana spirit ya utafutaji
 
Haya mambo ni huku africa tu huwezi kukuta ulaya na America kuna hizi vitu..
Jibu ni mfumo wetu wa maisha unakataa mfumo wetu wa elimu. Tujishahishe..!
 
matarajio makubwa.

Hii ndo changamoto yenyewe, ukiondoa hii utaishi maisha yako hatua kwa hatua..mafanikio mwachie Mungu pambana kwa nguvu na wakati wako. Usipokua na matarajio makubwa sana huwezi kujiona unafeli sana .... kuepuka mitandao ya kijamii pia, mana ndimo zitokako chemichemi za kuona hufanikiwi kwakua wenzio unaona wanaishi maisha ya matarajio yako,hii inaua sana spirit ya utafutaji
Nikuulize swali mkuu, Serikali mtu analipwa hadi million 25/30 kwa mwezi Ila anafanya machakato ya kukwiba billions within a month, unadhani ni nini kilichopo nyuma ya yeye kufanya hivyo?
 
Sababu kubwa ni kutokua na elimu ya ujasiliamali wengi tunatoka masomoni na mentality ya kuajiriwa then tukifika kitaa Mambo yanakua ndivyo sivyo na hii inapelekea kujaribu biashara mbalimbali lakini nazo wengi wetu tunaanguka kwa kukosa Ile elimu ya ujasiliamali
 
Habari za Muda huu wana JamiiForums.

Mimi ni kijana mjasiliamali kwa muda wa mika 10, kuna mambo huwa najiuliza kila siku nikiwa peke yangu sasa leo nimona ni changie na wana JamiiForums wenzangu.

Suala la Umasikini na Utajiri.

Kwanini vijana wengi hususani Wasomi ndio wanao hangaika sana kwenye masuala ya Uchumi, fedha na itajiri.

Utamkuta kijana mwenye umri wa miaka 28 hadi 39 ana shinda sana ya kifedha ili hali ni Msomi na ukute amesoma masomo ya Uchumi, Biashara lakini unamkuta anahangaika sana kifedha.

Pia, nikijaribu kuchunguza Vija wenye Rika kama hilo wasio wasomi naona wanamashi mazuri na wana endasha magari, wana nyumba zao na wanasomesha watoto wao shule nzuri.

Je, Shule zina sababisha vijana kuwa tengemezi kwenye suala la Utafutaji au au kuna tatizo gani?

Pia, kuna hii tabia ya Wasomi kupenda kufanya Biashara: Tatizo linakuja kwamba wasomi wengi wana taka kuanza bishara yenye mtaji mkubwa, utakuta kijana anakwambia nikipata milioni 10 naweza fanya biashara.

Naombini ufafanuzi kwanini wasomi wengi wanajikuta kwenye wimbi la umaskini kuliko walio ishia Darasa la Saba?

"JAMANI NIMEAMUA KUANDIKA TU"
"UTANI KWA WASOMI WENZANGU"
Kusoma siyo shida,shida ni kaunadili ulichosoma kiwe hela
 
Sababu kubwa ni kutokua na elimu ya ujasiliamali wengi tunatoka masomoni na mentality ya kuajiriwa then tukifika kitaa Mambo yanakua ndivyo sivyo na hii inapelekea kujaribu biashara mbalimbali lakini nazo wengi wetu tunaanguka kwa kukosa Ile elimu ya ujasiliamali
Kweli kabisa

Tuwaige Uganda kwa kuinclude somo la ujasiriamali katika mfumo wa elimu toka elimu ya awali hadi chuo
 
  • Thanks
Reactions: gim
Uvivu tu na kutokujaribu....mitaji tunayo ila uvivu wa kimwili na kiakili...
 
Kweli kabisa

Tuwaige Uganda kwa kuinclude somo la ujasiriamali katika mfumo wa elimu toka elimu ya awali hadi chuo
Kwa Tanzania hii sidhani Kama inawezekana tumeshindwa kuviendesha vyuo vya ufundi tutaweza kuweka mtaala wa ujasiliamali?
 
Back
Top Bottom