Natamani kupaza sauti kuhusu uonevu huu ila...

Natamani kupaza sauti kuhusu uonevu huu ila...

Bila shaka hii ni chai ya jioni. Haiwezekani health worker ashindwe hata kuandika historia ya mgonjwa. Na pia haelewi/ameshindwa kusimamia muongozo wa kazi yake. Ameleta contradiction tupu mfano huyo mama alishindwa vipi kuhudhuria clinic kwa miezi yote 9?, alikuwa na mkataba wa aina gani?, alipata uchungu wa ghafla? Maswali ni mengi mengi
Niandike hapa historia ya mgonjwa, huoni naacha vielelezo vya kunitrace na kesho naokotwa kwenye kiroba? Kuna zama huko kwa wenzetu watu walikuwa wanaweka habari kama hizi kwenye chupa na kutupa mbali ili miaka mingi ijayo watu wasome yaliyotokea!
 
Hicho kiwanda kinaitwaje na kipo wapi? Ukishindwa kukitaja wewe utakuwa ni muongo na mchonganishi.
 
Taja jina la kiwanda kesho huyu mama awaibukie
JamiiForums136820583.jpeg
 
Hicho kiwanda kinaitwaje na kipo wapi? Ukishindwa kukitaja wewe utakuwa ni muongo na mchonganishi.
Mkuu ingekuwa Dar ambapo kuna health facilities nyingi ingekuwa nafuu kulinda usalama wangu, hapa nilipo kuna vituo vya kutolea huduma za afya 3 tu, watuhumiwa hao ambao wengi wanatetewa na watanzania wenzetu wenye pesa na madaraka ni rahisi kujua ni kituo gani kilitoa taarifa ya mama huyo, ila pia enzi hizi mh, angalau kuna kipindi watoa taarifa walikuwa wanakabidhiwa kwenye vyombo vya usalama viwalinde!

Wananchi wakisimama pamoja hata Jeshi linatii, watanzania tumegawanywa kwa mafungu.mno..
 
FUNGUKA MKUUKIWANDA GANI, KIKO WAPI.N.K!..KAMA HUWEZI KWENDA POLISI AMA DAWATI HUSIIKA HATA KUWEKA HAPA KILA KITU UNAOGOPA?
Hakuna watu wanao tumikisha watanzania kinyanyasaji kama wachina, wachina ni makatili sana na hawajali utu.
 
Kuna matatizo ya kimfumo kwenye maswala ya safeguarding; sio kwenye afya sehemu nyingi tu zinazohusika na social services.

Health worker, walimu, ustawi wa jamii na taasisi zingine zinazotoa huduma za jamii hao wafanyakazi ni askari wa mbele kwa serikali kwenye kusimamia sheria, kupambana kupunguza maswala ya unyanyasaji kinyume na sheria na kadhalika.

Nchi za wenzetu frontline workers wana sign mkataba wa duty of care kuripoti mambo ambayo watakayoona ‘ndivyo sivyo’ ni jukumu lao na sehemu zingine unashitakiwa for negligence usipofanya ivyo mtu akapata madhara wakati wewe ulikuwa na information ambazo ukuzitoa watu wachunguze na kuchukua hatua.

Mtu anakutana na mjamzito anaona kabisa process zake za kumpatia huduma hazikuwa sahihi kutokana na restrictions za mwajiri wake ambazo ni kinyume cha sheria badala ya kupeleka concerns kwa wahusika anakuja hapa kulalamika sasa hayo matatizo yataisha vipi kama wenye mamlaka awapelekewi habari na watu wanaoshuhudia ili kuchunguza na kuchukua hatua.
Mkuu mbona ameweka wazi hapo juu kwamba ukijifanya unapenda haki siku zako zinahesabika za kuishi ndiyo maana kaamua kuleta humu yaani katupa jiwe gizani
 
Sasa inasaidia nini kuleta hapa hiyo story nusu nusu? Funguka ni wapi ili wenye kazi zao waanze kazi mara moja?
 
Nipo kibaruani mchana wa leo (nimerudi kazini awamu ya sita baada kama nilivyohaidi), nimempokea mama na kichanga chake ambaye amejifungulia kazini kwenye kiwanda cha Mchina (sehemu sitaitaja) ila ni mazingira mabaya kujifungulia binadamu, mama hana kadi ya kliniki na bahati nzuri alikuja kuanza kliniki ijumaa saa kumi akakuta huduma zimeishafungwa (jiulize ilikuwaje mama aanze kliniki na mimba kubwa karibia na kujifungua, hii haihitaji akili kubwa bila shaka hakuna ruhusa kazini) kwahiyo zile huduma kama vipimo vya wingi wadamu, magonjwa ya zinaa na ukimwi nk. na hivyo maisha ya huyu mtoto yapo hatarini!

Jamaa waliomsindikiza kwenye tax huyu mama ni wanaume watatu hakuna jisia ya kike! Walipofika wakahudumiwa wakataka kulipia staff aliyekuwepo akasema huduma za mama na mtoto ni bure, na hapo waksema wanazo 200,000/ mchina kawapa kwa ajili ya matibabu ya huyu mama na wakasema anahitaji risiti, wakauliza kama tunaweza kufanya mbinu ili risiti ipatikane .....kwa ufupi hatukuwapa risiti na badala yake yule mama alipewa sh.40,000 hela iliyobaki wasema wanaenda kutafta namna ya kupata risiti...tuachane na mambo ya pesa maana mimi sio lengo langu la kuleta uzi hapa JF,

Kitendo cha huyu mama kutohudhulia kliniki, kujifungulia kazini, nk kinaleta picha ya kuwepo na manyanyaso kwenye hiki kiwanda, nilitamani huyu mama awe mfano kwa akina mama na watu wote wanaoteswa na kunyimwa haki zao makazini...nilitamani kuripoti unyama huu ila....HII NCHI WAPENDA HAKI HAWATAKIWI KABISA, ukiangalia kesi za wenye pesa kama wale wezi wa mafuta Kigamboni ambapo serikali wapo kimya, nk nikijifanya kuingia anga za hawa wachina wanaoshirikiana na watanzania wenzangu yanaweza kunikuta ya kunikuta na kubaki peke yangu na historia isinikumbuke!
Tuendelee kuangalia pingamizi lililowekwa kwa Diamond Platnumz aondolewe kwenye tuzo za BET maana hiki ndicho waliowengi miongoni mwetu tunaweza sana!

PM details za hao manyang'au tusaidiane kulifanyia kazi hilo la wachei

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Nakupongeza kwa kuumia kwa utu wako, barikiwa sana kwa namna ulivyoguswa. Egos za baadhi usikwazike nazo ni upeo finyu
 
Nipo kibaruani mchana wa leo (nimerudi kazini awamu ya sita baada kama nilivyohaidi), nimempokea mama na kichanga chake ambaye amejifungulia kazini kwenye kiwanda cha Mchina (sehemu sitaitaja) ila ni mazingira mabaya kujifungulia binadamu, mama hana kadi ya kliniki na bahati nzuri alikuja kuanza kliniki ijumaa saa kumi akakuta huduma zimeishafungwa (jiulize ilikuwaje mama aanze kliniki na mimba kubwa karibia na kujifungua, hii haihitaji akili kubwa bila shaka hakuna ruhusa kazini) kwahiyo zile huduma kama vipimo vya wingi wadamu, magonjwa ya zinaa na ukimwi nk. na hivyo maisha ya huyu mtoto yapo hatarini!

Jamaa waliomsindikiza kwenye tax huyu mama ni wanaume watatu hakuna jisia ya kike! Walipofika wakahudumiwa wakataka kulipia staff aliyekuwepo akasema huduma za mama na mtoto ni bure, na hapo waksema wanazo 200,000/ mchina kawapa kwa ajili ya matibabu ya huyu mama na wakasema anahitaji risiti, wakauliza kama tunaweza kufanya mbinu ili risiti ipatikane .....kwa ufupi hatukuwapa risiti na badala yake yule mama alipewa sh.40,000 hela iliyobaki wasema wanaenda kutafta namna ya kupata risiti...tuachane na mambo ya pesa maana mimi sio lengo langu la kuleta uzi hapa JF,

Kitendo cha huyu mama kutohudhulia kliniki, kujifungulia kazini, nk kinaleta picha ya kuwepo na manyanyaso kwenye hiki kiwanda, nilitamani huyu mama awe mfano kwa akina mama na watu wote wanaoteswa na kunyimwa haki zao makazini...nilitamani kuripoti unyama huu ila....HII NCHI WAPENDA HAKI HAWATAKIWI KABISA, ukiangalia kesi za wenye pesa kama wale wezi wa mafuta Kigamboni ambapo serikali wapo kimya, nk nikijifanya kuingia anga za hawa wachina wanaoshirikiana na watanzania wenzangu yanaweza kunikuta ya kunikuta na kubaki peke yangu na historia isinikumbuke!
Tuendelee kuangalia pingamizi lililowekwa kwa Diamond Platnumz aondolewe kwenye tuzo za BET maana hiki ndicho waliowengi miongoni mwetu tunaweza sana!

uchumi wakati
 
Kiukweli kwenye nchi hii Uzalendo wa sisi wenyewe ni Ndito hebu ona Waliomleta wanamuibia maana mama amepewa Laki mbili ili ije kumsaidia wale nao wanaichukuwa watanzania wenzio hao alafu wewe unataka kuongea juu ya huyo mama bora ulivyoogopa mwenzangu upo sawa.
Maana sisi wenyewe ndio tunauwana unajua unaweza ukazani unamsaidia mtu kumbe yeye akaja kukugeuka ukashangaa basi achana nao.
 
Mkuu ingekuwa Dar ambapo kuna health facilities nyingi ingekuwa nafuu kulinda usalama wangu, hapa nilipo kuna vituo vya kutolea huduma za afya 3 tu, watuhumiwa hao ambao wengi wanatetewa na watanzania wenzetu wenye pesa na madaraka ni rahisi kujua ni kituo gani kilitoa taarifa ya mama huyo, ila pia enzi hizi mh, angalau kuna kipindi watoa taarifa walikuwa wanakabidhiwa kwenye vyombo vya usalama viwalinde!

Wananchi wakisimama pamoja hata Jeshi linatii, watanzania tumegawanywa kwa mafungu.mno..
Ulikosea kwenye ku frame story kabla ya kuileta humu... Nenda takukuru au kwa watu wa usalama wape hii ishu
 
Ulikosea kwenye ku frame story kabla ya kuileta humu... Nenda takukuru au kwa watu wa usalama wape hii ishu
Zamani kidogo wakati nimeajiliwa sijafahamu vizuri kuhusu hii nchi nilikuwa na akili kama zako, mwisho wa mwezi mmoja nikakuta makato kwenye mshahara wangu ambayo sikujua ni ya nini, kuangalia kumbe Chama flani cha wafanyakazi, nikaenda ofisini kwao tena ofisi ya Mkoa nikawauliza kwanini wanakata pesa wakati sikuwahi kuomba uanachama na sikujaza fomu yoyote ya kuridhia makato? boss alijibu kwa kaejeli na dharau kibao hadi nikaamua kwenda Takukuru....hadi leo bado nakatwa hiyo hela na sijawahi kuomba uanachama, ila kila Mei Mosi huwa napewa tisheti na kofia!

Kuhusu habari ya huyu mama ambayo kwakweli imeninyima usingizi leo (mama na kichhanga chake walikuja wananuka harufu ya bidhaa za kiwnda hicho!) kuna member wa hapa JF kanipa mbinu ya kumsaidia huyu mama na Mimi kubaki salama...Asante sana mwana JF ambaye hukutaka nikutaje hapa jukwaani, Mungu akujalie maisha marefu ili watu wengine wajifunze wema kutoka kwako!
 
Naomba msaada wa kuwaambia mods waondoe uzi huu...
Paw pls!
 
Back
Top Bottom