Natamani kupaza sauti kuhusu uonevu huu ila...

Niandike hapa historia ya mgonjwa, huoni naacha vielelezo vya kunitrace na kesho naokotwa kwenye kiroba? Kuna zama huko kwa wenzetu watu walikuwa wanaweka habari kama hizi kwenye chupa na kutupa mbali ili miaka mingi ijayo watu wasome yaliyotokea!
 
Hicho kiwanda kinaitwaje na kipo wapi? Ukishindwa kukitaja wewe utakuwa ni muongo na mchonganishi.
 
Hicho kiwanda kinaitwaje na kipo wapi? Ukishindwa kukitaja wewe utakuwa ni muongo na mchonganishi.
Mkuu ingekuwa Dar ambapo kuna health facilities nyingi ingekuwa nafuu kulinda usalama wangu, hapa nilipo kuna vituo vya kutolea huduma za afya 3 tu, watuhumiwa hao ambao wengi wanatetewa na watanzania wenzetu wenye pesa na madaraka ni rahisi kujua ni kituo gani kilitoa taarifa ya mama huyo, ila pia enzi hizi mh, angalau kuna kipindi watoa taarifa walikuwa wanakabidhiwa kwenye vyombo vya usalama viwalinde!

Wananchi wakisimama pamoja hata Jeshi linatii, watanzania tumegawanywa kwa mafungu.mno..
 
FUNGUKA MKUUKIWANDA GANI, KIKO WAPI.N.K!..KAMA HUWEZI KWENDA POLISI AMA DAWATI HUSIIKA HATA KUWEKA HAPA KILA KITU UNAOGOPA?
Hakuna watu wanao tumikisha watanzania kinyanyasaji kama wachina, wachina ni makatili sana na hawajali utu.
 
Mkuu mbona ameweka wazi hapo juu kwamba ukijifanya unapenda haki siku zako zinahesabika za kuishi ndiyo maana kaamua kuleta humu yaani katupa jiwe gizani
 
Sasa inasaidia nini kuleta hapa hiyo story nusu nusu? Funguka ni wapi ili wenye kazi zao waanze kazi mara moja?
 
PM details za hao manyang'au tusaidiane kulifanyia kazi hilo la wachei

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Nakupongeza kwa kuumia kwa utu wako, barikiwa sana kwa namna ulivyoguswa. Egos za baadhi usikwazike nazo ni upeo finyu
 
uchumi wakati
 
Kiukweli kwenye nchi hii Uzalendo wa sisi wenyewe ni Ndito hebu ona Waliomleta wanamuibia maana mama amepewa Laki mbili ili ije kumsaidia wale nao wanaichukuwa watanzania wenzio hao alafu wewe unataka kuongea juu ya huyo mama bora ulivyoogopa mwenzangu upo sawa.
Maana sisi wenyewe ndio tunauwana unajua unaweza ukazani unamsaidia mtu kumbe yeye akaja kukugeuka ukashangaa basi achana nao.
 
Ulikosea kwenye ku frame story kabla ya kuileta humu... Nenda takukuru au kwa watu wa usalama wape hii ishu
 
Ulikosea kwenye ku frame story kabla ya kuileta humu... Nenda takukuru au kwa watu wa usalama wape hii ishu
Zamani kidogo wakati nimeajiliwa sijafahamu vizuri kuhusu hii nchi nilikuwa na akili kama zako, mwisho wa mwezi mmoja nikakuta makato kwenye mshahara wangu ambayo sikujua ni ya nini, kuangalia kumbe Chama flani cha wafanyakazi, nikaenda ofisini kwao tena ofisi ya Mkoa nikawauliza kwanini wanakata pesa wakati sikuwahi kuomba uanachama na sikujaza fomu yoyote ya kuridhia makato? boss alijibu kwa kaejeli na dharau kibao hadi nikaamua kwenda Takukuru....hadi leo bado nakatwa hiyo hela na sijawahi kuomba uanachama, ila kila Mei Mosi huwa napewa tisheti na kofia!

Kuhusu habari ya huyu mama ambayo kwakweli imeninyima usingizi leo (mama na kichhanga chake walikuja wananuka harufu ya bidhaa za kiwnda hicho!) kuna member wa hapa JF kanipa mbinu ya kumsaidia huyu mama na Mimi kubaki salama...Asante sana mwana JF ambaye hukutaka nikutaje hapa jukwaani, Mungu akujalie maisha marefu ili watu wengine wajifunze wema kutoka kwako!
 
Naomba msaada wa kuwaambia mods waondoe uzi huu...
Paw pls!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…