Natamani kupenda tena

unajua kama una kitu special kwa mwanaume anayetaka mtu wa kuishi nae hawezi kukuacha kirahisi haijarishi ni umbali kiasi gani,lakini tofauti na hapo tutakula bata tu ila atakuwa anakuchora tu akitaka kuoa lazima ule kibuti cha kimyakimya
Sio lazima iwe hivyo always, haujawahi ona mwanaume/mwanamke anaweza kukuacha kwa kukuona haufai alafu akajirudi kwa magoti baada ya kugundua yo the best!!

Sio kwamba kwa kuwa kwenu wanaume basi mmekamilika 100%,lasivyo kusingekuwa na matatizo ktk ndoa maana mngekuwa mnachagua the best.
 
Mamii wewe bado haujawa tayari kupenda, jipe muda kwanza. Inaelekea bado una majeraha ya mahusiano yako yalopita. Usijilazimishe, haya mambo huwa yanatokea tu.
 
kila binadamu ana mapungufu yake hilo halipingiki lakini uvumilivu wa mtu na mtu ni tofauti,mfano unaweza kuwa unakunywa pombe mwingine akaona ni sawa tu na akaweza kuvumila lakini kwa mwingine hilo ni kosa ambalo halivumiliki,wanawake wengi kizazi hiki cha karne ya 21 wengi wenu hamjuii nini maana ya mahusiano lbda kama kula bata tu,ubabe mbele kwa mbele,kabla ujalaumu au kusononeka jiangalie mwenyewe kwanza waweza uliza hata watu waliokaribu yako watakwambia mapungufu yako kama wewe ni mtu wa kujichanganya ,lakini kama ndio wale wabinafsi nakijisikia sahau
 
Vya kuchagua vipo vingi,

Wengine wanataka wanaume wenye swagger, au pesa au smart au mtafutaji au mpole ila mradi kila mtu na vigezo vyake.
Mimi basi sijajua napendaga nini.
 
unajua kama una kitu special kwa mwanaume anayetaka mtu wa kuishi nae hawezi kukuacha kirahisi haijarishi ni umbali kiasi gani,lakini tofauti na hapo tutakula bata tu ila atakuwa anakuchora tu akitaka kuoa lazima ule kibuti cha kimyakimya
Kila mtu ana kitu special kwa mtu alie tayari kukipata hicho kitu. lakini unaweza ukawa na kila kitu mtu anakitaka ila akawa na sababu nyingine zitakazokatisha mahusiano yenu mfano kabila, dini etc..
 
Sinaga vigezo hata. Mwanzoni nilikua najua napenda wanaume weusi wanaofuga nywele ila nilikuja kufall in love na mwanaume mweupe na ananyoa. So yes sina choice yeyote nitakaempenda nimempenda moyo ti uridhie.
Ndo maana nilikuuliza umri,
Maana bado una matamanio ya mpaka awe na six pack na kiduku,
Walau ukifika ata miaka 35, utakuwa tayar kwa mahusiano.
 
Hakuna binadamu asiechagua. Usingekuwa unachagua usingrfungua huu uzi ungebeba yoyote alieanza kukutokea.
Mimi napenda na siamini sana kwenye kujifunza kumpenda mtu ndiyo sababu hata mtu awe smart vipi, awe na hela awe handsome kama moyo haujaridhia siwezi kuwa nae. Ningekua nina vigezo na naweza kupenda haraka ningekua nishapata muda tu..
 
...mpende alokuzalisha!
..wataka mtwisha nani zigo la malezi!
.#pambana_na_hali_yako_tu!
 
Ex bf wangu ambae ilibidi tuachane kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu ananilalamikia kila siku kuwa anajuta kwa uamuzi aliochukua anatamani yasingetokea yaliyotokea huwa namwambia tu ni maamuzi aliyochukua ayaishi mimi sipo tena. Ningekua sikua mwema asingepoteza muda na mimi. Kuna vitu haviepukiki hata kama uwe na tabia kama malaika vikitokea vimetokea.
 
Mamii wewe bado haujawa tayari kupenda, jipe muda kwanza. Inaelekea bado una majeraha ya mahusiano yako yalopita. Usijilazimishe, haya mambo huwa yanatokea tu.
Sawa mamii.. ngoja niendelee kujipa muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…