Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Natamani kuwa Mwanasiasa lakini moyo wangu umegoma kabisa!
Nikitazama runinga, nikisoma magazeti, au kushuhudia mijadala ya kisiasa, kuna sauti inaniambia: "Laiti na mimi ningekuwa mwanasiasa!" Kwa mbali, siasa inaonekana ni nafasi ya heshima, ushawishi na fursa. Ni njia ya kuwahudumia watu, kupigania wanyonge, na kushiriki katika ujenzi wa taifa. Wanasiasa wanapata nafasi ya kusikika, kuheshimiwa, na mara nyingine kunufaika kiuchumi na kijamii. Wanakutana na viongozi wa mataifa mengine, wana sauti bungeni, na majina yao huandikwa katika vitabu vya historia.
Lakini kadiri unavyokaribia uwanja wa siasa, ndivyo taswira inavyoanza kuonekana tofauti. Siasa ni shamba lenye miiba mingi: fitina, chuki, kashfa zisizoisha, usaliti kutoka kwa waliokaribiana nawe, na mashinikizo ya kila aina. Kuna wanaopoteza utu wao wakijaribu “kusurvive” ndani ya mfumo, na wengine hulazimika kuchafua mikono yao kwa gharama ya uadilifu. Wengine huingia katika ndoto za kuleta mabadiliko, lakini baadaye wanaonekana kama sehemu ya tatizo walilopanga kulimaliza. Kuna wanaozushiwa mambo ya uongo na kushambuliwa mitandaoni, na wengine huachwa na familia zao kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa. Na wengine wanaipigania keki miaka nenda rudi, lakini wanajikuta wamerudi mavumbini kabla ya kuionja keki. Mwee, tabu yote ya nini hii.
Nikitafakari hayo moyo wangu unaniambia: "Kaa pembeni mwanangu." Kweli heri nikae pembeni, niwaombee tu viongozi wetu Mungu awape hekima zaidi. Heri niombee amani na maridhiano badala ya kujiingiza mahali ambapo sihasa.
Nashangaa sasa hivi kila mtu ni mwanasiasa hata kama hapati mshahara wa siasa zake. Waliokimbia masomo ya siasa, wamejiingiza kwenye siasa. Mtu akianzisha chaneli tu ya Youtube, anaongea kama mwanasiasa aliyebobea. Kwanini? Moyo wangu mimi umegoma. Unaniambia sio lazima wote tuwe ndani ya ulingo wa siasa ili kulisaidia taifa. Tunaweza kuijenga nchi kupitia taaluma zetu, huduma zetu, upendo wetu kwa jirani, na maombi yetu kwa taifa.
Narudia tena kusema: moyo wangu umegoma kuwa mwanasiasa, lakini haujagoma kuiombea nchi na viongozi wake kama maandiko yanenavyo:
1 Timotheo 2:1-4
"Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu..."