Natamani kuwa Mwanasiasa lakini moyo wangu umegoma kabisa!

Natamani kuwa Mwanasiasa lakini moyo wangu umegoma kabisa!

Ukisoma Biblia na kuongozwa na Roho mtakatifu,

Una Elimu yote ya kukusaidia kuwa mwanasiasa Bora ikiwa uko ndani ya field hiyo.

Daudi was a king, politician,

Daniel was a politician,

Joseph was a politician,

King Solomon was a politician,

The Book of Judges, Kings 1&2, Samwel 1&2, Yeremia, nk nk

Ni siasa na uongozi zile,

Mifumo ya kidunia wamecopy Biblia na kujiweka Katika siasa wakiingia hila pia.

Sasa wa Giza hawataki muingie humo maana wanajua mna maarifa ya juu kuwazidi.

Mimi nimo humu kuhakikisha nauleta Ufalme wa Mungu Katika nchi YANGU Tanzania.

Watawale viongozi wenye hofu ya Mungu wanaochukia wizi wa kura na dhulma Ili haki itawale.

Na imekuwa. Amen
Amen!

Nilitaka kumwambia dada Setfree maneno haya haya! Nashukuru Mungu umemwambia vizuri zaidi!
 
Mtumishi acha kuingiwa na tamaa itakayo kusababishia madhara makubwa. Hapo hapo ulipo panatosha.

Kula hela inayotokana hawa watu wajinga na wanaopenda miujiza feki. Waambie tu unafufua wafu, viwete wanatembea, unaponya magonjwa yote yasiyo na tiba ikiwemo kansa na ukimwi, waambie una vitu vyenye upako (mfano maji, sabuni, udongo, chumvi, mafuta, nk) na hakikisha unawauzia kwa bei kubwa! Na usisahau kuisifia ccm.
Issue siyo kula hela!!! Issue ni KUMTUMIKIA MUNGU katika uwanja wa siasa!

Anachotaka yeye ni kuwahudumia watoto wa Mungu kupitia siasa ya kweli, haki na uwazi akimwakilisha Mungu aliye hai!!
 
Amen!

Nilitaka kumwambia dada Setfree maneno haya haya! Nashukuru Mungu umemwambia vizuri zaidi!
Rabonn na Elisha
mmenifanya nipekue Maandiko upya. Nimegundua kuwa ni kweli katika Agano la Kale kulikuwa na watumishi waliokuwa na nafasi za kisiasa kama Daudi, Daniel, na Yusufu. Lakini katika Agano Jipya, nimepekua sijaona hata mwanafunzi mmoja wa Yesu aliyekuwa mwanasiasa. Wala Yesu hakuwaita kutoka kwenye nyadhifa za kisiasa. Aliwaita wavuvi, wakusanya ushuru, na watu wa kawaida, sio watawala. Hata Simoni Zelote ambaye alikuwa mwanaharakati, aliacha siasa alipomfuata Yesu.

Hii inanionyesha kuwa huduma ya Yesu haikulenga mambo ya siasa, bali ilijikita katika kubadili mioyo ya watu. Kwa hoja hiyo sasa moyo wangu sio tu umegoma kuwa mwanasiasa bali hata nafsi na roho yangu vyote vimekubaliana kwamba sipaswi kuwa mwanasiasa.
 
Mi nadhani kila tunachofanya, kiliwekwa kifanyike kwa ajili ya utukufu wa Mungu!!

Kwa kifupi, dhumuni kuu la maisha yetu hapa duniani ni KUMTUKUZA MUNGU! So, kila tunachofanya ni lazima kiwe kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hata siasa iliwekwa ifanyike kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Kama watu hawatamuona Mungu katika siasa zetu hizo basi ni si-HASA na siyo siasa!

Kama ni mfanyibiashara, fanya kwa ajili ya utukufu wa Mungu! Huko madukani na masokoni tunauziwa bidhaa chafu nyingine kutoka kuzimu (unaweza kufikiri ni kiatu kwa macho ya nyama na kumbe sivyo!!!) so, ni jukumu la wakristo safi kuingia sokoni na kuwauzia watoto wa Mungu bidhaa safi kiroho na kimwili!

Kadhalika katika siasa, kuna viongozi wengi kutoka kuzimu na shetani amewatumia kutimiza kusudi la kuzimu. Lakini tungepata viongozi wazuri wakristo wenye kutumikia kusudi la Mungu, hakika tungekuwa na nchi nzuri sana! Usingesikia habari za watu kutekwa na kuuwawa! Usingesikia habari za ushoga na ufisadi! Usingesikia habari za ombaomba na mimba za utotoni nk

Tunahitaji watoto wa Mungu kama wewe ndani ya ulingo wa siasa kutumikia kusudi la Mungu! Tumewaachia wana wa giza kutawala na mambo hayaendi vizuri!

Ni wakati wa watoto wa Mungu KUMILIKI NA KUTAWALA!!
 
Issue siyo kula hela!!! Issue ni KUMTUMIKIA MUNGU katika uwanja wa siasa!

Anachotaka yeye ni kuwahudumia watoto wa Mungu kupitia siasa ya kweli, haki na uwazi akimwakilisha Mungu aliye hai!!
Kwenye siasa watu wanatumikia matumbo yao. Hakuna watoto wa Mungu wa kuwahudumia kwenye siasa.
 
Back
Top Bottom