Amen!Ukisoma Biblia na kuongozwa na Roho mtakatifu,
Una Elimu yote ya kukusaidia kuwa mwanasiasa Bora ikiwa uko ndani ya field hiyo.
Daudi was a king, politician,
Daniel was a politician,
Joseph was a politician,
King Solomon was a politician,
The Book of Judges, Kings 1&2, Samwel 1&2, Yeremia, nk nk
Ni siasa na uongozi zile,
Mifumo ya kidunia wamecopy Biblia na kujiweka Katika siasa wakiingia hila pia.
Sasa wa Giza hawataki muingie humo maana wanajua mna maarifa ya juu kuwazidi.
Mimi nimo humu kuhakikisha nauleta Ufalme wa Mungu Katika nchi YANGU Tanzania.
Watawale viongozi wenye hofu ya Mungu wanaochukia wizi wa kura na dhulma Ili haki itawale.
Na imekuwa. Amen
Issue siyo kula hela!!! Issue ni KUMTUMIKIA MUNGU katika uwanja wa siasa!Mtumishi acha kuingiwa na tamaa itakayo kusababishia madhara makubwa. Hapo hapo ulipo panatosha.
Kula hela inayotokana hawa watu wajinga na wanaopenda miujiza feki. Waambie tu unafufua wafu, viwete wanatembea, unaponya magonjwa yote yasiyo na tiba ikiwemo kansa na ukimwi, waambie una vitu vyenye upako (mfano maji, sabuni, udongo, chumvi, mafuta, nk) na hakikisha unawauzia kwa bei kubwa! Na usisahau kuisifia ccm.
Rabonn na ElishaAmen!
Nilitaka kumwambia dada Setfree maneno haya haya! Nashukuru Mungu umemwambia vizuri zaidi!
Mi nadhani kila tunachofanya, kiliwekwa kifanyike kwa ajili ya utukufu wa Mungu!!Rabonn na Elisha
mmenifanya nipekue Maandiko upya. Nimegundua kuwa ni kweli katika Agano la Kale kulikuwa na watumishi waliokuwa na nafasi za kisiasa kama Daudi, Daniel, na Yusufu. Lakini katika Agano Jipya, nimepekua sijaona hata mwanafunzi mmoja wa Yesu aliyekuwa mwanasiasa. Wala Yesu hakuwaita kutoka kwenye nyadhifa za kisiasa. Aliwaita wavuvi, wakusanya ushuru, na watu wa kawaida, sio watawala. Hata Simoni Zelote ambaye alikuwa mwanaharakati, aliacha siasa alipomfuata Yesu.
Hii inanionyesha kuwa huduma ya Yesu haikulenga mambo ya siasa, bali ilijikita katika kubadili mioyo ya watu. Kwa hoja hiyo sasa moyo wangu sio tu umegoma kuwa mwanasiasa bali hata nafsi na roho yangu vyote vimekubaliana kwamba sipaswi kuwa mwanasiasa.
Kwenye siasa watu wanatumikia matumbo yao. Hakuna watoto wa Mungu wa kuwahudumia kwenye siasa.Issue siyo kula hela!!! Issue ni KUMTUMIKIA MUNGU katika uwanja wa siasa!
Anachotaka yeye ni kuwahudumia watoto wa Mungu kupitia siasa ya kweli, haki na uwazi akimwakilisha Mungu aliye hai!!