Hiki ni mojawapo ya kifo cha furaha nilichowahi kushuhudia ...! Mzee Mwasapile almaarufu kama Babu wa Loliondo ametwaliwa kutoka maisha haya.. Mwendo ameumaliza salama ... Kwa amani na kwa furaha... Alimuishi Kristo Yesu akamtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa
Maneno ya
Mambo ya rohoni ufahamika kwa njia ya roho. Ni wale walio na Roho wa Mungu ndio wanaweza kuyajua mambo ya rohoni.
Siyo watu wote wanaosema, Bwana, Bwana ni watumishi wa Bwana Yesu Kristo wa kweli na haki. Ninyi huangalia mambo kwa jinsi ya mwili. Mmepotoka.
Kitendo cha huyu mzee na dawa yake ya kikombe unafikiri ulikuwa ni mpango wa Bwana Yesu Kristo?
Mwenyezi Mungu hakuwa na mkono wake ktk uongo ule; Na kama haukuwepo, basi, kazi ile ilitoka upande wa pili wa Yule Mwovu.
Mtume Paulo ktk kitabu cha Timotheo, mwanae ktk imani, anatuasa kuwa watauwa na kutosheka na hali tuliyonayo ni jambo lenye manufaa kubwa; kwa sababu, hapa duniani tulikuja uchi na tutaondoka vivyo hivyo uchi kama mzee huyu alivyoondoka.
Anaendelea kutufundisha kuwa, kupenda pesa ndiyo shina la maovu yote tuyashuhudiayo hapa Duniani.
Kwa jumla, "kikombe cha Babu" ulikuwa mpango uliotengenezwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na shetani-ibilisi ili kuwaingiza ktk maagano ya kishetani na kisha kuwaua ili awavune kuzimu.