Natamani kuwa na mwisho mwema kama Babu wa Loliondo

Kwamba tiba zetu ziliponya watu kwa imani waliyokua nayo. Si ndivyo unamaanisha hapa
Kwenye uponyaji kuna mambo mawili imani na tiba sahihi..! Imani huharakisha uponyaji.. State of mind..na I man I Ina vipengele vitatu
Imani juu ya dawa
Imani juu ya mtoa dawa/tabibu
Imani juu ya mazingira
Mwili una asilimia za natural healing, dawa husaidia tu huo mchakato wa uponyaji...
Na kwenye magonjwa na tiba, si kila ugonjwa ni wa kunywa dawa, mengine ni mind stated..!
Na si kila dawa iwe ya asili ama ya kizungu itatibu ugonjwa husika kwa mafanikio tarajiwa.. State of mind na Bali ya mwili ya huchangia sana kwenye uponyaji negatively or positively
IMANI ndio msingi wa kitu chochote...!
 
Hata mimi. Hapa nipo natafuta kakitu ka kuwavuruga wabongo waingie kingi kuwa ni tiba au suluhisho la jambo fulani. Nitaiweka kama marehemu babu huyo. Yani huwezi kuthibitisha kama ni miyeyusho au la. Ukihoji sana nakwambia nimeoteshwa, wewe imani yako tu ndo itakuponya. Kw astaili hii lazima nitakufa nikiwa na furaha. Sitokosa pesa ya pweza na al-kasusu. Sema sijui kwa Mungu nako nitachomoa au atanitaiti, ndo sijui.
Sema sijui kwa Mungu nako nitachomoa au atanitaiti, ndo sijui.[emoji3064][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Inasemekana aliamini ataitibia delta akapiga panda, imani ikakatiza uhai wake.

Ufu 14:13

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.[emoji1547][emoji1533][emoji1545]
 
Wengine walipona kwa imani na huo ndio muktadha wa kikombe...na illikuwa ni lazima ujushushe.. Ukienda pale na ukuu na sifa zako kikombe lazima kikukalishe.. Ama ukatumia ujanja ujanja hila na ubabe kufika mbele ya babu kikombe kiligeuka mma tuu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]jamaa umenipa burudani hapa! Kweli huduma ya kiimani ni kuamini huku ukijishusha na kunyenyekea pasipo hata chembe ya unafiki.

Umenikumbusha enzi hizo shuleni tulivyokuwa tunapita kibabe hadi mbele ya mgawa uji /msosi. Akizubaa tunajichotea wenyewe.
 
Mambo ya rohoni ufahamika kwa njia ya roho. Ni wale walio na Roho wa Mungu ndio wanaweza kuyajua mambo ya rohoni.
Siyo watu wote wanaosema, Bwana, Bwana ni watumishi wa Bwana Yesu Kristo wa kweli na haki. Ninyi huangalia mambo kwa jinsi ya mwili. Mmepotoka.

Kitendo cha huyu mzee na dawa yake ya kikombe unafikiri ulikuwa ni mpango wa Bwana Yesu Kristo?
Mwenyezi Mungu hakuwa na mkono wake ktk uongo ule; Na kama haukuwepo, basi, kazi ile ilitoka upande wa pili wa Yule Mwovu.
Mtume Paulo ktk kitabu cha Timotheo, mwanae ktk imani, anatuasa kuwa watauwa na kutosheka na hali tuliyonayo ni jambo lenye manufaa kubwa; kwa sababu, hapa duniani tulikuja uchi na tutaondoka vivyo hivyo uchi kama mzee huyu alivyoondoka.

Anaendelea kutufundisha kuwa, kupenda pesa ndiyo shina la maovu yote tuyashuhudiayo hapa Duniani.
Kwa jumla, "kikombe cha Babu" ulikuwa mpango uliotengenezwa na kuratibiwa kwa umakini mkubwa na shetani-ibilisi ili kuwaingiza ktk maagano ya kishetani na kisha kuwaua ili awavune kuzimu.
Kwahiyo wewe ni wa rohoni, na umeliona lile tukio kuwa la shetani. ...itakuwa siku za mwisho, nitawamwagia watu wote roho wangu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]jamaa umenipa burudani hapa! Kweli huduma ya kiimani ni kuamini huku ukijishusha na kunyenyekea pasipo hata chembe ya unafiki.

Umenikumbusha enzi hizo shuleni tulivyokuwa tunapita kibabe hadi mbele ya mgawa uji /msosi. Akizubaa tunajichotea wenyewe.
Hahahaha Ila siku akikulia timing akakupata umekwishaa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hiki ni mojawapo ya kifo cha furaha nilichowahi kushuhudia ...! Mzee Mwaisapile almaarufu kama Babu wa Loliondo ametwaliwa kutoka maisha haya.. Mwendo ameumaliza salama ... Kwa amani na kwa furaha... Alimuishi Kristo Yesu akamtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa

Maneno ya Mungu yanasema maisha ya mwanadamu ni miaka 70 na ukiwa na nguvu ni miaka 80, baada ya hapo unaishi miaka ya bakshish...Naamini mzee Mwaisapile kaishi na ya ziada

Hakuwahi kujulikana popote katika kazi yake ya utumishi wa kiroho kwenye imani yake ya Kikristo kupitia kanisa la Kilutheri..alihubiri na kutumika kwenye madhabahu ya Mungu mpaka anastaafu akiwa hana kitu chochote cha thamani cha kidunia zaidi ya kibanda cha nyasi alichokiita nyumba yake. Lakini hakuwahi kulalamika popote wala kumlalamikia yeyote

Mungu anaona yote ... Naye akamwambia.. Kwakuwa umenitumikia kwa uaminifu NITAUSHIBISHA MEMA UZEE WAKO! Mara paap! Kikombe hicho
Hakujitangaza popote iwe mitandaoni, kwenye vyombo vya habari ama kutembea na maspika ALITANGAZWA kwa sauti iliyoenda mbali sana
Hakuhangaika kutafuta wasaidizi na watenda kazi..! WALIKUJA wenyewe..
Hakuhangaika kuleta WALINZI wala kuwalipa POSHO watu walijitolea

Watu wakamiminika Loliondo toka pande zote za dunia kwenda Loliondo kupata kikombe cha babu kinachoponya magonjwa mbalimbali...Habari zake zikavuma na kutangazwa mpaka na vyombo vikubwa vya habari duniani

Akawa balozi mzuri aliyeitangaza Tanzania na Loliondo kwa uzuri baada ya eneo hilo kugubikwa na migogoro na kashfa zilizosababishwa na wanasiasa WAROHO wa mali
Wanasiasa na viongozi mbalimbali wa nchi yetu hawakuwa nyuma kwenye kwenda kupata kikombe cha Babu..Mungu akaushibisha mema uzee wa babu..Mchungaji mstaafu Mwaisapile..!

Lililo kubwa na la ajabu hakutoza fedha kubwa kwenye tiba yake ya kikombe! Alitoza mia tano tuu/500 na katika hiyo yeye alichukua mia mbili tuu/200 nyingine zikaenda kwa watenda kazi na wasaidizi wake.. Na wote walitumikia kwa uaminifu mkubwa..!
Tiba ile ilikuwa na maajabu mengi
Kupitia hiyo tiba utalii ukaongezeka
Kupitia hiyo tiba Tanzania ikazidi kujitangaza kimataifa
Kupitia hiyo tiba watu wakafanya sana biashara
Kupitia hiyo tiba watu wengi wakapona maradhi yao, wengine walikufa njiani na wengine hawakupona.. Kwakuwa kila kitu kina pande mbili
Kupitia hiyo tiba tuliwaona manabii na mitume wengi katika rangi zao halisi..Wivu ukawajaa na kuanza kumshambulia babu kwa kila hali..LAKINI KAMWE HAKUJIBIZANA NAO..Alimuachia Mungu aseme nao...

Atazikwa mazishi ya kawaida kabisa. Mwili wake hautataabishwa huku na kule wala hautanuka.. Atazikwa akiwa fresh kabisa bila kuanza kuoza akiwa bado duniani..pengine hatakumbukwa duniani lakini anayo nafasi yake mbinguni siku ya kiama...
Apumzike kwa amani mtumishi mwema na mwaminifu wa Mungu.. Natamani kuwa na mwisho mema kama yeye[emoji848]

[emoji2827]Mungu nisaidie[emoji1545][emoji1545][emoji1545]

giphy.gif

Mungu atamuona na kumlipa kwa UTAPELI wa kutuaminisha KIKOMBE FEKI CHA DAWA.
wengi ndugu na jamaa wakapoteza MAISHA
Baadae Kikombe kikachukuliwa na SHETANI alie kianzisha kikaingia GIZANI mpaka leo. Baada ya mavuno waliokusudia kuvuna kupitia matatizo na dhiki za wagonjwa wa UKIMWI NA KISUKRI.
 
Basi Yesu akawaambia asiye na mawaa awe wa kwanza kurusha jiwe...
 
Mungu atamuona na kumlipa kwa UTAPELI wa kutuaminisha KIKOMBE FEKI CHA DAWA.
wengi ndugu na jamaa wakapoteza MAISHA
Baadae Kikombe kikachukuliwa na SHETANI alie kianzisha kikaingia GIZANI mpaka leo. Baada ya mavuno waliokusudia kuvuna kupitia matatizo na dhiki za wagonjwa wa UKIMWI NA KISUKRI.
Eneo niishilo walitoka mamia ya watu wakaenda kunywa kikombe. Hadi leo ni wazima. Kuna ndugu yangu wa karibu sana alikua na kifafa kila mwezi anaanguka. Baada ya kikombe anWezamaliza mwaka/miaka bila hata dalili. Ila akinywa kilevi tu imo
 
Kwahiyo wewe ni wa rohoni, na umeliona lile tukio kuwa la shetani. ...itakuwa siku za mwisho, nitawamwagia watu wote roho wangu.
Hakika ndugu, kama ulivyosema, Ni kweli na uko sahihi, ... mimi ni wa rohoni na ndiyo maana mambo ya Kikombe cha Babu tulioneshwa na Roho wa Mungu mapemaa na hatukunyamaza kimya bali tuliwaonya watu kukiepuka.
 
Hiki ni mojawapo ya kifo cha furaha nilichowahi kushuhudia ...! Mzee Mwaisapile almaarufu kama Babu wa Loliondo ametwaliwa kutoka maisha haya.. Mwendo ameumaliza salama ... Kwa amani na kwa furaha... Alimuishi Kristo Yesu akamtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa

Maneno ya Mungu yanasema maisha ya mwanadamu ni miaka 70 na ukiwa na nguvu ni miaka 80, baada ya hapo unaishi miaka ya bakshish...Naamini mzee Mwaisapile kaishi na ya ziada

Hakuwahi kujulikana popote katika kazi yake ya utumishi wa kiroho kwenye imani yake ya Kikristo kupitia kanisa la Kilutheri..alihubiri na kutumika kwenye madhabahu ya Mungu mpaka anastaafu akiwa hana kitu chochote cha thamani cha kidunia zaidi ya kibanda cha nyasi alichokiita nyumba yake. Lakini hakuwahi kulalamika popote wala kumlalamikia yeyote

Mungu anaona yote ... Naye akamwambia.. Kwakuwa umenitumikia kwa uaminifu NITAUSHIBISHA MEMA UZEE WAKO! Mara paap! Kikombe hicho
Hakujitangaza popote iwe mitandaoni, kwenye vyombo vya habari ama kutembea na maspika ALITANGAZWA kwa sauti iliyoenda mbali sana
Hakuhangaika kutafuta wasaidizi na watenda kazi..! WALIKUJA wenyewe..
Hakuhangaika kuleta WALINZI wala kuwalipa POSHO watu walijitolea

Watu wakamiminika Loliondo toka pande zote za dunia kwenda Loliondo kupata kikombe cha babu kinachoponya magonjwa mbalimbali...Habari zake zikavuma na kutangazwa mpaka na vyombo vikubwa vya habari duniani

Akawa balozi mzuri aliyeitangaza Tanzania na Loliondo kwa uzuri baada ya eneo hilo kugubikwa na migogoro na kashfa zilizosababishwa na wanasiasa WAROHO wa mali
Wanasiasa na viongozi mbalimbali wa nchi yetu hawakuwa nyuma kwenye kwenda kupata kikombe cha Babu..Mungu akaushibisha mema uzee wa babu..Mchungaji mstaafu Mwaisapile..!

Lililo kubwa na la ajabu hakutoza fedha kubwa kwenye tiba yake ya kikombe! Alitoza mia tano tuu/500 na katika hiyo yeye alichukua mia mbili tuu/200 nyingine zikaenda kwa watenda kazi na wasaidizi wake.. Na wote walitumikia kwa uaminifu mkubwa..!
Tiba ile ilikuwa na maajabu mengi
Kupitia hiyo tiba utalii ukaongezeka
Kupitia hiyo tiba Tanzania ikazidi kujitangaza kimataifa
Kupitia hiyo tiba watu wakafanya sana biashara
Kupitia hiyo tiba watu wengi wakapona maradhi yao, wengine walikufa njiani na wengine hawakupona.. Kwakuwa kila kitu kina pande mbili
Kupitia hiyo tiba tuliwaona manabii na mitume wengi katika rangi zao halisi..Wivu ukawajaa na kuanza kumshambulia babu kwa kila hali..LAKINI KAMWE HAKUJIBIZANA NAO..Alimuachia Mungu aseme nao...

Atazikwa mazishi ya kawaida kabisa. Mwili wake hautataabishwa huku na kule wala hautanuka.. Atazikwa akiwa fresh kabisa bila kuanza kuoza akiwa bado duniani..pengine hatakumbukwa duniani lakini anayo nafasi yake mbinguni siku ya kiama...
Apumzike kwa amani mtumishi mwema na mwaminifu wa Mungu.. Natamani kuwa na mwisho mema kama yeye[emoji848]

[emoji2827]Mungu nisaidie[emoji1545][emoji1545][emoji1545]

giphy.gif

Unadhani alikuwa na mwisho mwema wakati ametapeli na kuumiza wengi kwa uchoyo wake?
 
Hivi leo hii unaweza kusifia tena hichi ulichoandika?

Watu wametapeliwa,wamekufa pia wamepoteza vingi vyao

Kikombe kinatibu eee?
 
Back
Top Bottom