Natamani kuwa na mwisho mwema kama Babu wa Loliondo

Rest in peace mzee wakikombe.
Umeniachia funzo sana..kamwe nisikate tamaa kwasababu yaumri,
Unaeza kukosa kwenye ujana ukapata uzeeni kikubwa akiri nakujituma. [emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 
"Hatakumbukwa sana hapa duniani, ila mbinguni ana nafasi yake' Wewe ni nani mpaka ya babu wa Loliondo na Mungu wake uyajue? Acheni kupotosha watu.
 
Ok.
Pamoja na yote, alidhihirisha jinsi Wanyakyusa walivyo katika ubora wao. Yupo mwenzake alitumia imani ya aina hiyo kupukutisha watu wa ukanda huohuo,,,
Mwisho wa mtu tumwachie Mwenyezi MUNGU
 
Kwamba bado kuna watu mnaamini kile kikombe ni tiba?

I swear Tz tuna shida bado. Ndiyo sababu unaona mvutano mkubwa juu ya chanjo kwakua Tz elimu haijasambaa kote ndiyo maana wajinga bado wengi.
 
Kwamba bado kuna watu mnaamini kile kikombe ni tiba?

I swear Tz tuna shida bado. Ndiyo sababu unaona mvutano mkubwa juu ya chanjo kwakua Tz elimu haijasambaa kote ndiyo maana wajinga bado wengi.
Ile ni kama tiba nyingine tuu kuna kupona, kuna kutopona.. Hizo tiba zingine za kuaminika kama kweli zingekuwa timamu dunia isingeugua
 
Ile ni kama tiba nyingine tuu kuna kupona, kuna kutopona.. Hizo tiba zingine za kuaminika kama kweli zingekuwa timamu dunia isingeugua
Hoja ya kwamba kwakua dunia bado ina magonjwa hivyo inahalalisha unywaji wa kikombe unaiona ni sahihi?
 
Ukiwa mhitaji na ukaambiwa mkojo ni dawa na ukanywa kwa imani unapona! BTW kabla ya tiba za kizungu hatukuwa na tiba zetu? Zilikuwa hazitusaidii?
Kwamba tiba zetu ziliponya watu kwa imani waliyokua nayo. Si ndivyo unamaanisha hapa
 
Hata mimi. Hapa nipo natafuta kakitu ka kuwavuruga wabongo waingie kingi kuwa ni tiba au suluhisho la jambo fulani. Nitaiweka kama marehemu babu huyo. Yani huwezi kuthibitisha kama ni miyeyusho au la. Ukihoji sana nakwambia nimeoteshwa, wewe imani yako tu ndo itakuponya. Kw astaili hii lazima nitakufa nikiwa na furaha. Sitokosa pesa ya pweza na al-kasusu. Sema sijui kwa Mungu nako nitachomoa au atanitaiti, ndo sijui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…