Natamani nikaishi mbali sehemu ambayo sifahamiki na mtu yoyote

Mmh!pole mkuu Kun wakat tunapita katik vilinge vigumu nakutaman hat mambo flan yatokee ndipo huend tutakuwa saw.lakin kinachokosekan hpo ni kimoja t..MUNGU.mshirikishe Mungu kweny nyakat hzo unazopitia atakufnyia wepesi amini hili nakwambia

Amen [emoji120], Asante kwa kunitia moyo [emoji120]🥹
 

Asante kwawkunitia Moyo ndugu,
Naombeni ushauri, nitakapoenda nkifika nichukue hatua gani, maana mimi katika ukuaji wangu nimekulia mazingira ya nyumbani nyumbani tu, wala nlkua sjazoea kuishi mbali na nyumbani, inshort shida nmekua nikiziskia tu, but sasa imefikia tamati naamua kwenda mbali na wazazi na ndugu ili nikaanze kuishi maisha yangu private
 
Kivipi mzee mwenzangu wazazi
Tunakosea wapi Ebu funguka

Wewe kama hujawahi experience hii jambo usiombe likukute. Hakuna kitu kinaumiza kama kuchukiwa na wazazi pasipo na sababu yoyote wala kosa lolote ulilowakosea [emoji17]
 
Ukifika mbali bado utakuja JF au JF nayo utaipptezea?

Nilipata wazo kama hili kuondoka Bongo mazima miaka ya 90, nikahamia mbali na nilikotokea, mpaka leo sina mpango wa kurudi Bongo.
Kuhusu ndugu vipi, unarud nyumbani? Matatizo yakitokea huku bongo si unarud lakini
 

Pole sana kwa magumu unayoyapitia. Bila shaka wewe bado ni kijana. Nimeumia sana moyoni, nikifikiria kama labda ni mtoto wangu angeweza kufikia hatua hiyo!!

Ingekuwa inawezekana, ningependa kujua zaidi: Je, ni nini kimekufanya kufikia hatua hii? Je, ni kuhisi familia na ndugu hawakupendi na kukuthamini? Je, ni ugumu wa maisha? Je, labda umefanya jambo unaloona limekutia sana aibu mbele ya unaowafahamu? Au unalazimishwa kuishi maisha usiyoyataka?

Lakini vyovyote iwavyo, ufahamu kuwa wewe ni mtu mwenye thamani kubwa sana mbele za Muumba wako, na kuna wengi wanakupenda na kukuthamini, japo yawezekana wengine hata huwafahamu. Ufahamu kuwa hata katika magumu, kuna wakati humea mema. Unaweza kupitishwa katika magumu ili akili yako iamke, ufanye uamuzi fulani, na huo uamuzi utakuondoa katika masikitiko, mahangaiko na hali ya kukata tamaa.

Ninachokusifu sana hukukaa na uamuzi wako moyoni, badala yake ukaamua kutushirikisha.

Kiufupi, kama unaona hali uliyofikia ni muhimu kujitenga, basi huna haja ya kufikiria kwenda mbali sana, huna haja ya kwenda Gaza au Burundi, wala Zimbabwe. Nchi hii ni kubwa, waweza kwenda mkoa mwingine, lakini ufanye hivyo kwa umakini, maana usije ukaenda ugenini halafu majuto yakawa magumu zaidi, ukaishia kukata tamaa.

Naomba utusaidie zaidi: upo mkoa gani? Una umri gani? Wewe ni wa jinsia gani? Kazi gani una uwezo wa kuzifanya? Wazazi wako wote wapo hai? Wanafanya shughuli gani? Una ndugu wengine katika familia, kama vile wadogo zako na wakubwa zako? Ni muumini mzuri wa dini (ukristo au uislam)?
 
Kuhusu ndugu vipi, unarud nyumbani? Matatizo yakitokea huku bongo si unarud lakini
Narudi. Ila familia ya karibu wanakuja sana huku kila nikitaka kuja TZ wao wanakuja huku karibu kila mwaka inabidi nikae huku tu.

Huku Marekani kuna kitu kinaitwa Thanksgiving familia nyingi huwa zinakutana kila mwezi wa 11, kukaa na kula pamoja, mshua wangu huwa anakuja kila mwaka bila kukosa awe na watoto na wajukuu wake wote walio US katika Thanksgiving.
 
Nenda mikoa au wilaya ambazo unaweza kufanya kilimo...

Ingia Tukuyu, Njombe, Iringa, Lushoto, Rukwa ndichi ndichi huko...
 
katavi ndani ndani huko utakuwa na amani zote
 
Kama una hela mbona hilo ni jambo jepesi tu! Hata hapa bongo Dar unaweza kujipoteza mwenyewe! Au ukenda mkoa unaojielewa kama Arusha au Mwanza! Au vimji vidogo visivyo na mambo mengi lakini vyenye hela kama Iringa
 

Haya mambo ni ya kuzungumzia PM
 
Kama una hela mbona hilo ni jambo jepesi tu! Hata hapa bongo Dar unaweza kujipoteza mwenyewe! Au ukenda mkoa unaojielewa kama Arusha au Mwanza! Au vimji vidogo visivyo na mambo mengi lakini vyenye hela kama Iringa

Ushauri mzuri sana, ( kuhusu pesa yote nliyokua nkitunza ilichukuliwa na mzazi wangu nkidhani kuwa atanirudishia skujua kuwa ndo ilikua mbinu yake ya kunirudisha nyuma kimaendeleo, kazi amenifukuzaw, na pesa yangu amebaki nayo)[emoji119][emoji856][emoji30]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…