Natamani sana andiko hili la hukumu ya Afande Bageni lisomwe vituo vya Polisi na Makazi yao kwenye Paredi

Natamani sana andiko hili la hukumu ya Afande Bageni lisomwe vituo vya Polisi na Makazi yao kwenye Paredi

NImesikia kweli huyu muuaji namba moja yuko Morogoro Mkambarani. Ila nasikia hali yake ni kama zezeta fulani hivi. Afadhali angefungwa jela angekuwa anajitambua ila hapo alipo sasa mmmmmmmm
Akiwa zezeta basi itakuwa afadhali Sana kwa Usalama wa Umma kwa sababu hatakuwa na uwezo tena wa kurudia kufanya uhalifu mbaya kama huo aliofanya kwa hao Wafanyabiashara aliowaua.
 
Polisi wote Tanzania ni majambazi yenye baraka za serikali,, ukweli usemwe,,
 
Naam! Ukifanya ubaya utalipwa ubaya na ukifanya wema utalipwa wema na ziada ya wema.
 
SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!Na Tumcheni Mungu popote tutakapokuwapo,
 
K
Mwangwi wa sauti ya Wakabing'oko!

SSP Christopher Bageni, atanyongwa hadi kufa! Ndivyo Mahakama ya Rufaa ilivyoamua. Hakika uamuzi wa leo ni wa mwisho katika mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia wala pa kupinga, ni kweli Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Hivyo Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Its over! imeisha!!

Hawezi kukata rufani tena kwa sababu hukumu ya leo ni review, marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo 16 Septemba 2016 ambapo alihukumiwa kunyongwa "hadi kufa" na jopo lile la majaji watatu wakiongozwa naye Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya 'kujadili' tena shauri hilo labda iwe kupitia msamaha wa Rais

View attachment 3243016
Sasa kwao wasiokumbuka, Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi, wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye, akiwa na wenzie, wakiongozwa na aliokua Kaimu RPC Dar Abdallah Zombe, walituhumiwa "kupanga njama" za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro. Sasa A. Zombe anadaiwa kuongoza wenziye kwenye 'mpango' huo baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Hivyo 'wakaikamata' gari waliyokua wameikodi! Na kisha Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Kisha "wakapora" madini pamoja na fedha zote walizokuwa nazo. 'Wakawafunga' vitambaa vyeusi usoni, na hadi pingu mikononi. Wakapigwa risasi za 'kisogoni' na kuuawa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha. Aise!!

Na kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi, yaliyokua yanarushiana tu risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda 'tume' ya Jaji Kipenka kuchunguza jambo hilo. Ikabainika jamaa, hawakuwa Majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa "familia moja". Mama mmoja alipoteza wanae watatu pia watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao. Na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za watumishi wachache!

Zombe alifanikiwa 'Kuchomoka' kwenye kesi hii baada ya kusota "rumande" kwa miaka kadhaa!! Lakini Bageni 'alikutwa' na Hatia! Akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa na akafeli. Akaomba review ya kesi sasa rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA. Yani si kunyongwa tu!

Hakika waliomtuma hawapo nae Segerea. Wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Na Wanaohangaika nae sasa hivi angalau kumfariji ni familia yake, A. Zombe hayupo OCD wake hayupo na hata IGP wa wakati ule hayupo pia. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa pekee!!

Hakika hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo i.e kuteka kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Aliyekutuma hatakuwepo, basi utasimama mwenyewe kutoa hesabu, ya maovu yako. Kama sio hapa duniani basi hata kule mbinguni. Lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo, Wema ni Mbegu. Na Ubaya pia ni mbegu, humea hukomaa na ni lazima uvune! Usijitume wala Kutumwa kwa mabaya, Hukumu ya Mungu ni ya haki. Hakuna jasiri wa kudumu!!

Nchi yangu, Machozi yako, Nchi tamu ya uhuru!
Kwa hiyo huyu bageni ana shati hilo hilo tu. Au hii ndiyo ile ile picha ya mwanzo?
 
Hii ni Habari njema Sana kwa Wapenda HAKI hapa Tanzania.

Ili kulinda maslahi mapana zaidi ya umma katika nchi hii, Rais wa nchi anapaswa ASAINI HATI YA KIFO ya huyu Mtu ili angalau kuanza kurejesha imani iliyopotea miongoni mwa Wananchi dhidi ya vyombo vya Dola, hususani kwa Jeshi la Polisi na Tiss.

Siyo Siri hata kidogo, Wananchi wengi zaidi tayari wamepoteza kabisa Imani dhidi ya Jeshi la Polisi kutokana na vitendo viovu vya uhalifu kama aliofanya huyu Askari Polisi Christopher Bageni.

Siku moja na yaliyomwua Kibao, na kuwapoteza akina soka, nayo yatendewe hivyo hivyo. Hayo ni mashetani yasiyostahili kuonewa huruma. Haya yalitakiwa kuuawa hadharani, tena kwa kuyakata kiungo kimoja kimoja, iwe fundisho kwa mashetani yaliyosalia.
 
Mwangwi wa sauti ya Wakabing'oko!

SSP Christopher Bageni, atanyongwa hadi kufa! Ndivyo Mahakama ya Rufaa ilivyoamua. Hakika uamuzi wa leo ni wa mwisho katika mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia wala pa kupinga, ni kweli Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Hivyo Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Its over! imeisha!!

Hawezi kukata rufani tena kwa sababu hukumu ya leo ni review, marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo 16 Septemba 2016 ambapo alihukumiwa kunyongwa "hadi kufa" na jopo lile la majaji watatu wakiongozwa naye Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya 'kujadili' tena shauri hilo labda iwe kupitia msamaha wa Rais

View attachment 3243016
Sasa kwao wasiokumbuka, Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi, wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye, akiwa na wenzie, wakiongozwa na aliokua Kaimu RPC Dar Abdallah Zombe, walituhumiwa "kupanga njama" za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro. Sasa A. Zombe anadaiwa kuongoza wenziye kwenye 'mpango' huo baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Hivyo 'wakaikamata' gari waliyokua wameikodi! Na kisha Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Kisha "wakapora" madini pamoja na fedha zote walizokuwa nazo. 'Wakawafunga' vitambaa vyeusi usoni, na hadi pingu mikononi. Wakapigwa risasi za 'kisogoni' na kuuawa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha. Aise!!

Na kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi, yaliyokua yanarushiana tu risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda 'tume' ya Jaji Kipenka kuchunguza jambo hilo. Ikabainika jamaa, hawakuwa Majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa "familia moja". Mama mmoja alipoteza wanae watatu pia watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao. Na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za watumishi wachache!

Zombe alifanikiwa 'Kuchomoka' kwenye kesi hii baada ya kusota "rumande" kwa miaka kadhaa!! Lakini Bageni 'alikutwa' na Hatia! Akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa na akafeli. Akaomba review ya kesi sasa rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA. Yani si kunyongwa tu!

Hakika waliomtuma hawapo nae Segerea. Wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Na Wanaohangaika nae sasa hivi angalau kumfariji ni familia yake, A. Zombe hayupo OCD wake hayupo na hata IGP wa wakati ule hayupo pia. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa pekee!!

Hakika hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo i.e kuteka kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Aliyekutuma hatakuwepo, basi utasimama mwenyewe kutoa hesabu, ya maovu yako. Kama sio hapa duniani basi hata kule mbinguni. Lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo, Wema ni Mbegu. Na Ubaya pia ni mbegu, humea hukomaa na ni lazima uvune! Usijitume wala Kutumwa kwa mabaya, Hukumu ya Mungu ni ya haki. Hakuna jasiri wa kudumu!!

Nchi yangu, Machozi yako, Nchi tamu ya uhuru!
Ciciem ni maf💩💩💩 na samia buhiri ni takataka kesi hiyo walitakiwa kinyongwa watu kama 10 hivi ...basi hata huyo atapokea msamaha wa mjambiani mipumbavu
 
Damu Oops
Namuona Mkewe Wakati Mwingine Mo Town
Kwenye Usafiri Lakini Abdala Hoi
 
Baadhi ya Polisi huwa wana akili za ajabu ajabu sana, nina 2 brothers wako huko sioni msaada wao kabisa. Sitaki mazoea kabisa na polisi wa Tanzania

Nilipata wasaa wa kwenda hapo tu jirani Nairobi, aisee polisi wa wenzetu wana maadili ya kwenda mgeni ishu zangu zilikua zinakua sorted bila wenge.

Au issue ya "Fighting For Food Four years" bado ni pending issue kwao na haijapatiwa muarobaini?
 
Back
Top Bottom