Natamani sana Ndoa za dini ya Kiislamu " Its the best marriage Ever"

Natamani sana Ndoa za dini ya Kiislamu " Its the best marriage Ever"

malisoka

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Posts
1,860
Reaction score
2,636
Pamoja na changamoto mbali mbali za dini ya kiislamu. Baada ya kuchunguza sana nimegundua katika ndoa na mfumo wake ni Ndoa bora zaidi kuliko za Kikristo .

Kama ningeweka katika % basi Ndoa za Kiislamu ni 90% ubora na za Kikristo ni kama 40%

Kwa nini nasema hivi?

Kwanza mimi ni mkristo na nimeoa ndoa ya Kikristo.

Amani - 70% ya ndoa za kikristo hazina amani kabisa ukilinganisha na ndoa za kiislamu zenye amani 80%.

Hii ni kwa sababu ya ile consent (uhiyari wa kuishi katika ndoa).

Upendo - Upendo wa kweli ni 90% kwa waislamu, tofauti na 20% ya ndoa za kikristo (hasa kwa wanawake).

Hii ni kwa sababu ya kupenda au kutokupenda kukaa katika ndoa yenye shida , this means kwa Waislamu aliyepo kwenye ndoa ni yule anayependa kuwa hapo na kama hapendi ndoa hiyo ruksa kuondoa wakati wote. So 100% ndoa za kiislamu wapo kwenye upendo kwa sababu ya uhiyari wa kuwepo au kutokuwepo katika ndoa.

Katika kutafiti kwangu Ile kwamba Mume mmoja na mke mmoja katika ndoa za kikristo ni nadharia tu uhalisia siyo hivyo. Muda mwingi inakuwa ni kujidanganya tu.

(Nimeshuhudia si kwa watu wa kawaida tu hata kwa wachungaji 50% ya ndoa zao ni mbovu)

Nimegundua kwamba Wanaume wa Kiislamu wanatumia ule ubaba wao vibaya na ile ruhusa ya kuoa zaidi ya mke mmoja kama nyanyaso kwa wanawake wengi.

Vile vile nimegundua Wanawake wa kikristo hutumia vibaya ile "pingu za maisha" kufanya wanachotaka wakiwa na bima ya kutokuachika katika ndoa zao na hii imepelekea upendo kupoa na uvunjifu mkubwa wa amani katika ndoa za kikristo.

Kwa ndoa za Waislamu kila kitu kipo wazi watoto, mirathi, kugawana mali na nk.

Katika ndoa za kikristo kila kitu ni giza totoro hakuna utaratibu wala nini. kila kitu vululuvululu.


Mwanamke Alyepo kwenye ndoa za kiislamu ana future anajua sehemu yake na majukumu yake na hata hatma ya watoto wake(this is good).

Kwa waislamu Mume ni master.

Kwa wakristo mume ni partner.

Kwa waislamu kusolve matatizo ya ndoa ni rahisi sana kupitia kwa kadhi.

Kwa wakristo kusuluhisha matatizo ya ndoa ni ngumu sana (kwa maana jambo la hiayari, linafanywa lazima).


Ndoa za kiislamu zimedumu miaka na miaka bila kubadirika - hii ni kutokana na msingi Imara na msimamo wa dini.

Ndoa za kikristo zimebadirika sana na kupindukia. Sasa kuna ndoa za kikristo za mashoga, sasa kuna ndoa za kusagana, sasa kuna ndoa za mikataba.

Kitabu cha dini inayosimamia ndoa za kiislamu hakijabadilishwa (kinasumbuka tu na tafsiri na mafundisho) lakini Content ni ile ile ya kale na kale na hii ndiyo inaweka uimara wa ndoa.

Kitabu cha dini ya Kikristo (Biblia) kimebadishwa sana na sasa baadhi ya maandiko kutokueleweka au kuchanganya na hata mafundisho (theolojia) yake inachanganya sana huyu anafunzisha hivi na yule anafundisha hicho hicho tofauti.

Haya ndio nilivyoyaona katika ndoa hizi.
 
Nenda visiwani kuna watu wana vyuo mpaka 6. Halafu ana miaka 25 tu..
Msichana akikuambia nina vyuo vitatu ujue kaolewa na kuachika mara 3.

Sisi wakristo tunasema mjue sana Mungu ili uwe na amani.

Hiyo Ni Consent niliyoisema, uhuru wa kuishi katika ndoa. tofauti na wanawake wetu wengine siku hizi wanasema aolewe au aoe ili apewe zawadi au ili aondoe mkosi wa kuolewa nk. akiingia katika ndoa anakuwa mwiba.
 
Mtu akitoka nje ya ndoa anapigwa mawe mpaka afe, hii sheria igekua ndio ya kitaifa mbona watu wangebakia njia kuu, mchepuko usingekua dili.

Mwanamke haruhusiwi akiwa peke yake nyumbani kupata mgeni au kutembelewa na mgeni wa kiume ambae anaweza kumwoa (sio kaka yake, baba yake, mjomba wake), mpaka mume wake awepo. Na mwanaume pia hivo hivo.

Ndoa ya kiisalmu hakuna kugawana mali 50% pindi mkiachana, kila mtu anasepa na alichotafuta (ila huduma kwa watoto ni lazima kwa mwanaume kutoa).
 
Nenda visiwani kuna watu wana vyuo mpaka 6. Halafu ana miaka 25 tu..
Msichana akikuambia nina vyuo vitatu ujue kaolewa na kuachika mara 3.
Na wengi hujisifia kuolewa Mara nyingi kuwa Ni sifa kuwa yeye soko lake liko juu.Vyuo vikiwa vingi Ni sifa kwa wanawake wenzie kuwa usimuone yule kiboko yule sasa hivi chuo Cha nane
 
Nenda visiwani kuna watu wana vyuo mpaka 6. Halafu ana miaka 25 tu..
Msichana akikuambia nina vyuo vitatu ujue kaolewa na kuachika mara 3.

Ndio uzuri moja wapo huo sio mtu upendo hamna basi mnaishi tu kama simba na chui’ upendo ukiisha na kutokufikia muafaka basi mnapeana talaka kila mmoja anafanya yake
Hata akiwa na vyuo20 kinachotakiwa ni uhalal tu[emoji1419]

Nina majirani zetu huu ni mwaka wa 15 wanaishi pamoja ila kila mtu na chumba chake’ kila mtu analeta watu wake (wapenzi) Yan wanakomeshana ilihali ni mume na mke kwa ndoa takatifu

Sasa shida yote ya nn??? Ndoa za kiislamu ni nzuri bisha ubishavyo ila ukweli ndo huo
 
Wooooooohh!!
IMG_20200114_124355.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uislamu ni dini ya ajabu inayoendana na binadamu.

Ruhusa ya mume kuoa wake wengi jambo ambalo ni maumbile ya mwanaume.na uislamu haukujali kuwa mwanamke atapata wivu kwa sababu wivu ni sehemu ya mwanamke.

Uislamu umeruhusu mwanamke kujivua kwenye ndoa kwa sharti ya kulipa mahari ikiwa mwanamke huyo ametokea kumchukia mumewe ghafla kwa sababu ya tabia zake mbovu au imetokea tu amemchukia moyoni mwake.

Hapa mwanamke amepewa uhuru pia na uislamu kwenye ndoa mana mume anaweza kuwa tafrani mbaya mbaya kwa tabia alafu unaambiwa ni pingu za maisha kwani ndoa ni kosa mpaka iwe pingu za maisha..?

Uislamu bwana unaruhusu mwanamke kuvunja ndoa kwa kadhi ikiwa mume ana tabia mbovu.. malisoka,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa tamu ukipata mtu sasa mimi muislam sijawah kuwa mkristo so ya kikristo siyajui vizuri lakini huku kwetu ukipata mke alisoma dini na upendo upo hata kuchepuka huwezi, kuna usafi flani hivi amaizing, ila ukichochora ukaoa muislam jina ama na wewe una mambo yako meusi mbona utafurai na roho yako itakuwa ya moto kama unaishi jehannam ndogo
 
Kwanza Kuna limit wake 4 tu sio zaidi

Tamaa ya mwanaume sio 4 tu ila zaidi yaani idadi haieleweki.

Nikujifariji tu, fanyeni research muone kama wanaume huridhika wakifikisha wake 4 ndo baasi.

Akipita mnene macho kodo

Mrefu macho kodo

Mwembamba macho kodo

Mwenye nywele nzuri macho kodo

Mwenye kiuno kizuri macho kodo

Mwenye sauti na mwanya mzuri macho kodo

Nafsi zetu huwa zinaficha mengi na midomo yetu bila aibu hunena unafiki uliotukuka.
 
Naona una experience mbovu katika ndoa mkuu na unajaribu kuzilinganisha na za wengine ambazo unazoziona kwa nje. Si ajabu kuna mtu anakuangalia na kukuona role model wake katika ndoa ila siri unayo moyoni
 
Mwizi ni mwizi, huwa hatosheki akiiba laki tatu, usijidanganye kwamba ukimpa milioni atatulia.

Malaya ni malaya tu usijidanganye atatulizwa na wake wa nne. Hiyo ni silka ama hulka ya mtu. Na behaviour not easy to manage.

Nimeishi mikoa mingi hapa Tanzania machungu na vichomi vya masahibu ya ndoa yameenea kote. Sio bara wala visiwani, sio mbeya wa bukoba

Ndoa ni zaidi ya kanisani

Ndoa ni zaidi ya msikitini

Bora kubishana...bishana lakini chungu na tamu kwa kila ndoa ...
Wanaoelewa ni wanandoa wenyewe.
 
Back
Top Bottom