ALI V. MUSSA,
Umejibu vema mkuu,
ongezeko la talaka inatokana na wanandoa wenyewe kutokufuata taratibu halisi za ndoa ama kukwepa misingi halisi ya ndoa. Huu ni ukweli kabisa, nakupa tano kwa hilo.
1. Ndoa za siku hizi hazifuati misingi ya ndoa hivyo kupelekea watu kutalikiana hovyo.
2. Ndoa za siku hizi zimejengwa kwenye tamaa ya kukidhi kiu ya ngono kuliko kujenga familia stable. Wanandoa wanaoana ili tu kujaribu kukata kiu ya ngono, hawana mtazamo mwingine kuhusu ndoa, ndio maana UJINGA WA KISASA ni habari za vibamia, mashimo makubwa n.k. Katika hayo yote hakuna msingi wa ndoa.
3. Sijakuelewa unaposema ndoa za kulazimishana kwa sababu ninachoelewa ni kwamba mwanamke na mwanamume wanakuw na consent kisha wanaamua kuwa wanataka kuoana. Hakuna anayemshikia bunduki mwenzake, ni hiari ya moyo. Sasa wawili hawa wakikubaliana wanaamua kuita watu na kuweka ushahidi mbele yao na mnele ya Mungu kwamba wameamua kuungana hivyo mwingine asijaribu kuwaingilia.
Inapotokea wamepishana ama kukorofishana iweje mtu mwingine ahusike hapo? Kwa nini kumnyooshea kidole mtu wa tatu kuwa amewalazimisha kuungana wakati hata hakushiriki kuwapa mashauri waoane?
Ndoa ya kikristo imepaswa ijengwe katika msingi wa kumwamini Mungu. Kwamba umwamini atakupa mke ama mume bora, lakini swali linalowatesa wengi na kuwafanya wabaki kuzini hovyo ni hili:
Je, umemwamini Mungu kiasi cha kufuata maagizo yake na kusubiri akuonyeshe mke au mume wa maisha yako?
Ni wangapi leo wanaweza kusimama na kusema waliingia kwenye ndoa kwa kufuata vigezo vya Mungu? Wengi weru tunaingia kwenye ndoa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na dunia, tunajitwalia wake na waume wa upofu wetu. Mambo yawapo magumu tunatamani tuwaache tutafute wengine, kwa sababu hawa hawakuwahi kuwa wenza wetu hata hivyo. We pre empt God.
Kwa sababu tunaona katika mazingira ya umalaya halafu tunategemea tuishi kwa utakatifu, basi tunajikuta tukitapatapa tu, tuna elimu ya umalaya na ukahaba imeijaza mioyo yetu, halafu tukiingia kwenye ndoa tunataka tuishi kwa elimu ya Mungu ambayo hatuna. Tutajiita wana wa Mungu huku tukimtumikia shetani, kwani kiujazacho moyo wa mtu ndicho kiutokacho.
Suluhu ya hili sio kuoa wake wengi, kwani katika hao pia kama hujafuata misingi ya ndoa bado talaka zitaendelea tu. Misingi ya ndoa ndio jibu kama ulivyobainisha hapo juu. Huwezi kutumikia mabwana wawili, kwa maana utampenda zaidi huyu kuliko mwingine, hata mtume alimpenda zaidi Bi Aisha kuliko wakwze wengine, ni maumbile tu hayo.
Jifunze misingi ya ndoa kabla ya kuingia kwenye ndoa, uli unapooa uoe kwa motive sahihi nawe utampata aliyesahihi kwako. Hivi ndivyo ilivyokuwa tangu kale, watu walioa kwa malengo sahihi kwa kuzingatia misingi ya ndoa, ndipo ndoa nyingi zilidumu.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk