Natamani sana Ndoa za dini ya Kiislamu " Its the best marriage Ever"

Natamani sana Ndoa za dini ya Kiislamu " Its the best marriage Ever"

Nyenyere, Hizi unazozungumzia ni special case, tunazungumzia zile ndoa zilizofungwa kwa misingi ya upendo na sio tamaa tu za mwili ambapo pande zote zipo. Anachoongelea mtoa mada ni kuwa ukiona waislamu wamekaa na kudumu kwenye ndoa jua wanapendana tofauti na sisi unaweza kuona mtu ndani kunafukuta ila hana namna ya kutoka, kifupi kwenye ndoa za kikristo kuna vituko vingi sana....watu wanatutangazia wao ni mume na mke ila ndani wametengana vyumba, eti mume hali chakula kilichopikwa na mkewe hadi ale na watoto kwa hofu ya kuwekewa sumu, kama kungekuwa na talaka haya yasingekuwepo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaza UJINGA ikiwa Kiungo cha mwili wako kinaweza kukatwa kuepusha kuharibu viungo vyengine na kulinda Afya yako Ije iwe ndoa ndo kiwe kitu cha milele na mtu mlie juana ukubwani tu na kila mtu na fikra zake .hapo ndo mmoja anawe kupanga kumuua mwenziwe ili awe huru Kwenye uislamu ndoa Si utumwa ni Maslahi na maelewano kama hamna ruhsa kuepukana nayo ili kila mtu awe huru
Hii ndiyo point tuongeee yote ila ndoa za kikristo zi ashida sana ......mi ni mkristo ila navutiwa na ndoa za kiisilamu hakuna kuzenguana muda wowote ,

Kama mtu anaweza kukatwa kiungo ili kuopesha usalama wa mwili kwa nini kungangania mpk kufa ?

Kwani umezaliwa naye , ndoa nyingi zipo hoi maigizo ni mengi na ni pasua kichwa

Sent using i phone x
 
Hizi unazozungumzia ni special case, tunazungumzia zile ndoa zilizofungwa kwa misingi ya upendo na sio tamaa tu za mwili ambapo pande zote zipo. Anachoongelea mtoa mada ni kuwa ukiona waislamu wamekaa na kudumu kwenye ndoa jua wanapendana tofauti na sisi unaweza kuona mtu ndani kunafukuta ila hana namna ya kutoka, kifupi kwenye ndoa za kikristo kuna vituko vingi sana....watu wanatutangazia wao ni mume na mke ila ndani wametengana vyumba, eti mume hali chakula kilichopikwa na mkewe hadi ale na watoto kwa hofu ya kuwekewa sumu, kama kungekuwa na talaka haya yasingekuwepo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo sio ndoa za kikristo wala kiislamu, huko ni kukwepa msingi wa tatizo. Wengi wanaingia kwenye huo mtego kwa sababu tu hawakuzingatia misingi ya kuingia kwenye ndoa hivyo kujidanganya kuoa na kuacha ndio msimamo mzuri, huo si ukweli.

Ukijua ndoa ni nini utaingia kwa usahihi na utampata mtu sahihi na mataishi kwa furaha maisha yenu yote. Hizi habari za wakristo hawana furaha ni nyimbo za watu wenye tamaa lakini nawajua wakristu wengi tu wenye amani kwenye ndoa zao kama niwajuavyo waislamu wasio na amani kwenye ndoa zao.

Uzoefu wako na ubaki kwako mwenyewe, walio na masikio ya kusikiliza maonyo na maongozo wanaishi kwa amani tu kwenye ndoa zao bila kutii tamaa za mwili kutamani kila kitu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Nyenyere, Nafahamu wapo wakristo wenye ndoa zao nzuri tu, lakini kuna wengine inatokea bahati mbaya wanakosea kuingia na watu ambao sio sahihi...tungepewa na sisi walau nafasi ya kurekebisha makosa [emoji14]....hata moja tu au mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na changamoto mbali mbali za dini ya kiislamu. Baada ya kuchunguza sana nimegundua katika ndoa na mvumo wake ni Ndoa bora zaidi kuliko za Kikristo .

Kama ningeweka katika % basi Ndoa za Kiislamu ni 90% ubora na za Kikristo ni kama 40%

Kwa nini nasema hivi?

Kwanza mimi ni mkristo na nimeoa ndoa ya Kikristo.

Amani - 70% ya ndoa za kikristo hazina amani kabisa ukilinganisha na ndoa za kiislamu zenye amani 80%.

Hii ni kwa sababu ya ile consent (uhiyari wa kuishi katika ndoa).

Upendo - Upendo wa kweli ni 90% kwa waislamu, tofauti na 20% ya ndoa za kikristo (hasa kwa wanawake).

Hii ni kwa sababu ya kupenda au kutokupenda kukaa katika ndoa yenye shida , this means kwa Waislamu aliyepo kwenye ndoa ni yule anayependa kuwa hapo na kama hapendi ndoa hiyo ruksa kuondoa wakati wote. So 100% ndoa za kiislamu wapo kwenye upendo kwa sababu ya uhiyari wa kuwepo au kutokuwepo katika ndoa.

Katika kutafiti kwangu Ile kwamba Mume mmoja na mke mmoja katika ndoa za kikristo ni nadharia tu uhalisia siyo hivyo. Muda mwingi inakuwa ni kujidanganya tu.

(Nimeshuhudia si kwa watu wa kawaida tu hata kwa wachungaji 50% ya ndoa zao ni mbovu)

Nimegundua kwamba Wanaume wa Kiislamu wanatumia ule ubaba wao vibaya na ile ruhusa ya kuoa zaidi ya mke mmoja kama nyanyaso kwa wanawake wengi.

Vile vile nimegundua Wanawake wa kikristo hutumia vibaya ile "pingu za maisha" kufanya wanachotaka wakiwa na bima ya kutokuachika katika ndoa zao na hii imepelekea upendo kupoa na uvunjifu mkubwa wa amani katika ndoa za kikristo.

Kwa ndoa za Waislamu kila kitu kipo wazi watoto, mirathi, kugawana mali na nk.

Katika ndoa za kikristo kila kitu ni giza totoro hakuna utaratibu wala nini. kila kitu vululuvululu.


Mwanamke Alyepo kwenye ndoa za kiislamu ana future anajua sehemu yake na majukumu yake na hata hatma ya watoto wake(this is good).

Kwa waislamu Mume ni master.

Kwa wakristo mume ni partner.

Kwa waislamu kusolve matatizo ya ndoa ni rahisi sana kupitia kwa kadhi.

Kwa wakristo kusuluhisha matatizo ya ndoa ni ngumu sana (kwa maana jambo la hiayari, linafanywa lazima).


Ndoa za kiislamu zimedumu miaka na miaka bila kubadirika - hii ni kutokana na msingi Imara na msimamo wa dini.

Ndoa za kikristo zimebadirika sana na kupindukia. Sasa kuna ndoa za kikristo za mashoga, sasa kuna ndoa za kusagana, sasa kuna ndoa za mikataba.

Kitabu cha dini inayosimamia ndoa za kiislamu hakijabadilishwa (kinasumbuka tu na tafsiri na mafundisho) lakini Content ni ile ile ya kale na kale na hii ndiyo inaweka uimara wa ndoa.

Kitabu cha dini ya Kikristo (Biblia) kimebadishwa sana na sasa baadhi ya maandiko kutokueleweka au kuchanganya na hata mafundisho (theolojia) yake inachanganya sana huyu anafunzisha hivi na yule anafundisha hicho hicho tofauti.

Haya ndio nilivyoyaona katika ndoa hizi.
Mkuu umesema kweli 100/100. Ndoa za kikristo ni NDOANO. Watu tunakufa na tai zetu shingoni ndani ya ndoa. Huwezi kuamini jinsi wanawake wanavyoleta nyodo na ngebe kwa kuwa ndoa zao zina bima ya 'pingu za maisha'. Ushuzi mtupu[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32][emoji777]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika. Wengine wamekubali ndoa tu kwa kuwa waliona umri unaenda na wamepoteza matumaini ya kuolewa. Lakini baada ya kuingia kwenye ndoa wamekuwa vichomi.
Sisi wakristo tunasema mjue sana Mungu ili uwe na amani.

Hiyo Ni Consent niliyoisema, uhuru wa kuishi katika ndoa. tofauti na wanawake wetu wengine siku hizi wanasema aolewe au aoe ili apewe zawadi au ili aondoe mkosi wa kuolewa nk. akiingia katika ndoa anakuwa mwiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
u must have a serious problem ...Kuandika paragraph nying si kipimo cha maarifa ...pia ndoa ni ya wawili kupendana dini ni muongozo tu sjaona umuhimu wa kuleta utofaut wa dini hapa in short ni uzi wa kutetea dini fulani kwa mgongo wa ndoa

ps : naheshimu dini yoyote cha msingi kila mtu Aamini anachoamini Muhimu Amani ,upendo na kutendeana mema ..Mengine ni ww na Mungu Wako
Very true.

Dini yangu ya kikristo ni nzuri sana Ila kuna mafundisho (theolojia) inalazimisha mambo wakati ni hiyari.

Kuoa na kuolewa ni hiyari kama ilivyo kutoa sadaka ni hiyari.

Ninachopigania ile uhiyari wa mtu kuingia katika ndoa na awe na uhiyari wa kutoka katika ndoa.

Kama nilivyosema hapo awali. Mimi nimeoa ndoa ya kikristo, huyu niliye naye ni part ya research yangu, baada ya kuona karibia wote wananfanana ndiyo nimekuja ku conclude kwamba kwenye ndoa hizi za dini hii na ile kuna tofauti kubwa.


Nisamehe kama nimekukwaza but that is true.
 
huo uchunguzi uliufanya wapi? we kama unataka kuoa kiislam nenda tu acha kutafuta justification, hujalazimishwa kukaa kwenye ndoa ya kikristo, badili dini, oa kiislam basi jipe furaha unayoitafuta
 
(Ndoa za kikristo zimebadirika sana na kupindukia. Sasa kuna ndoa za kikristo za mashoga, sasa kuna ndoa za kusagana, sasa kuna ndoa za mikataba). Hizi zipo kwenye biblia gani?
 
Du hiki ni "kifungo cha nje". Yaani hata mtu usichepuko hata mkeo akiwa na mimba? Ut@t0mB@ wapi?[emoji32][emoji32][emoji32]
Mtu akitoka nje ya ndoa anapigwa mawe mpaka afe, hii sheria igekua ndio ya kitaifa mbona watu wangebakia njia kuu, mchepuko usingekua dili.

Mwanamke haruhusiwi akiwa peke yake nyumbani kupata mgeni au kutembelewa na mgeni wa kiume ambae anaweza kumwoa (sio kaka yake, baba yake, mjomba wake), mpaka mume wake awepo. Na mwanaume pia hivo hivo.

Ndoa ya kiisalmu hakuna kugawana mali 50% pindi mkiachana, kila mtu anasepa na alichotafuta (ila huduma kwa watoto ni lazima kwa mwanaume kutoa).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huo uchunguzi uliufanya wapi? we kama unataka kuoa kiislam nenda tu acha kutafuta justification, hujalazimishwa kukaa kwenye ndoa ya kikristo, badili dini, oa kiislam basi jipe furaha unayoitafuta

Ok.

kuna ndoa za mashoga na mikataba na za jinsia moja katika ukristo huu huu ni kwa kitabu gani? ni hii hii biblia au kitabu kingine?.

Hii inaonesha kwamba waalimu wetu wa biblia kuna kitu hawaweki sawa katika mafundisho ya ndoa.
 
Ndio maana huwa nawashangaa sana vijana wadogo wanaotaka kuoa mapema. Kwanini wanataka kujitumbukiza kwenye matatizo ktk umri mdogo?[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32][emoji22][emoji22]
Nafikiri kuna watu wengi hawaelewi maana ya kuoa wake wengi humu na Google hawaitendei haki
Kama hujaelewa kitu ni bora kuuliza tu na kuuliza sio ujinga bali ni kuongeza maarifa tu
Google please


Sent from my iPhone using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ALI V. MUSSA,

Umejibu vema mkuu, ongezeko la talaka inatokana na wanandoa wenyewe kutokufuata taratibu halisi za ndoa ama kukwepa misingi halisi ya ndoa. Huu ni ukweli kabisa, nakupa tano kwa hilo.

1. Ndoa za siku hizi hazifuati misingi ya ndoa hivyo kupelekea watu kutalikiana hovyo.

2. Ndoa za siku hizi zimejengwa kwenye tamaa ya kukidhi kiu ya ngono kuliko kujenga familia stable. Wanandoa wanaoana ili tu kujaribu kukata kiu ya ngono, hawana mtazamo mwingine kuhusu ndoa, ndio maana UJINGA WA KISASA ni habari za vibamia, mashimo makubwa n.k. Katika hayo yote hakuna msingi wa ndoa.

3. Sijakuelewa unaposema ndoa za kulazimishana kwa sababu ninachoelewa ni kwamba mwanamke na mwanamume wanakuw na consent kisha wanaamua kuwa wanataka kuoana. Hakuna anayemshikia bunduki mwenzake, ni hiari ya moyo. Sasa wawili hawa wakikubaliana wanaamua kuita watu na kuweka ushahidi mbele yao na mnele ya Mungu kwamba wameamua kuungana hivyo mwingine asijaribu kuwaingilia.

Inapotokea wamepishana ama kukorofishana iweje mtu mwingine ahusike hapo? Kwa nini kumnyooshea kidole mtu wa tatu kuwa amewalazimisha kuungana wakati hata hakushiriki kuwapa mashauri waoane?

Ndoa ya kikristo imepaswa ijengwe katika msingi wa kumwamini Mungu. Kwamba umwamini atakupa mke ama mume bora, lakini swali linalowatesa wengi na kuwafanya wabaki kuzini hovyo ni hili:

Je, umemwamini Mungu kiasi cha kufuata maagizo yake na kusubiri akuonyeshe mke au mume wa maisha yako?

Ni wangapi leo wanaweza kusimama na kusema waliingia kwenye ndoa kwa kufuata vigezo vya Mungu? Wengi weru tunaingia kwenye ndoa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na dunia, tunajitwalia wake na waume wa upofu wetu. Mambo yawapo magumu tunatamani tuwaache tutafute wengine, kwa sababu hawa hawakuwahi kuwa wenza wetu hata hivyo. We pre empt God.

Kwa sababu tunaona katika mazingira ya umalaya halafu tunategemea tuishi kwa utakatifu, basi tunajikuta tukitapatapa tu, tuna elimu ya umalaya na ukahaba imeijaza mioyo yetu, halafu tukiingia kwenye ndoa tunataka tuishi kwa elimu ya Mungu ambayo hatuna. Tutajiita wana wa Mungu huku tukimtumikia shetani, kwani kiujazacho moyo wa mtu ndicho kiutokacho.

Suluhu ya hili sio kuoa wake wengi, kwani katika hao pia kama hujafuata misingi ya ndoa bado talaka zitaendelea tu. Misingi ya ndoa ndio jibu kama ulivyobainisha hapo juu. Huwezi kutumikia mabwana wawili, kwa maana utampenda zaidi huyu kuliko mwingine, hata mtume alimpenda zaidi Bi Aisha kuliko wakwze wengine, ni maumbile tu hayo.

Jifunze misingi ya ndoa kabla ya kuingia kwenye ndoa, uli unapooa uoe kwa motive sahihi nawe utampata aliyesahihi kwako. Hivi ndivyo ilivyokuwa tangu kale, watu walioa kwa malengo sahihi kwa kuzingatia misingi ya ndoa, ndipo ndoa nyingi zilidumu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Ahsante mkuu na ww nakupa tano kwa ufafanuzi mzuri ndo maana mm sidharau imani ya mwenzangu najua kua Anamafundisho yake tatizo tunatoka nje ya mafundisho kisha tunatafuta mchawi .Maana kosa la Muumini hali haribu Uzuri wa dini .Imam au Padri akizini haimaanishi kua dini zimeruhusu zinaa
 
Nyinyi mnaapa mpaka kifo kitutenganishe sisi hatuna hiyo!!!! Na ndio inawacost

Yes kuachana ni kuzuri

Sasa mf mtu hamuelewani hamna upendo mng’ang’aniane tu kuishi pamoja? Ndio matokeo yake huwa negative

Kama hawa majirani zetu hawana muda na watoto wao , wako busy kukomesha mma akiona baba kaleta vibinti na yy anakamatia vibenten

Sasa kma wote mmeridhiana hamtakani ni heri muachane tu
Hiyo Dini ya kuruhusu kuoa na kuachana ni Dini ya hovyo sana

Si ni bora hiyo ndoa isifungishwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi unazozungumzia ni special case, tunazungumzia zile ndoa zilizofungwa kwa misingi ya upendo na sio tamaa tu za mwili ambapo pande zote zipo. Anachoongelea mtoa mada ni kuwa ukiona waislamu wamekaa na kudumu kwenye ndoa jua wanapendana tofauti na sisi unaweza kuona mtu ndani kunafukuta ila hana namna ya kutoka, kifupi kwenye ndoa za kikristo kuna vituko vingi sana....watu wanatutangazia wao ni mume na mke ila ndani wametengana vyumba, eti mume hali chakula kilichopikwa na mkewe hadi ale na watoto kwa hofu ya kuwekewa sumu, kama kungekuwa na talaka haya yasingekuwepo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umeongea vizuri kabisa nakubaliana nawewe

Swali langu kwako upo teyari kuolewa na kufukuzwa mara ngapi katika maisha yako?
 
Back
Top Bottom