Natamani umri wa kustaafu kazi hasa kwenye taasisi za umma ungepunguzwa toka 60 mpaka 55

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,043
Kama maada inavyojieleza ,hii ingesaidia kuwapa fursa zaidi vijana na kuchochea ari ya nguvu kazi na maendeleo zaidi,watu wangejiandaa mapema na kuwaachia vijana Nafasi ,pasi na kuwa na vijana wengi mtaani wasio na ajira rasmi ilhali wana taaluma mbalimbali na kuwa wategemezi zaidi.

Natamani Serikali iliangalie Hilo kwa kina
 
Umri unaendana na uzoefu wa kazi, sana sana serikali itataka kuongeza umri wa kustaafu hadi miaka 65 kama ilivyofanya kwa wahadhiri wa vyuo vikuu.
 
Hii haitokuwa njia mbadala, japo kwa mwanzo litakuwa limepunguza kitu maana litakuwa limesogeza muda wa kustaafu.Lakini baadae mambo yatarudi vilevile.

Kwa sababu ikiwa umri wa kustaafu ni miaka 60, basi atakaye kaa kazini mda mrefu ni yule aliyeingia na umri mdogo, na hapa ndipo penye tatizo.

Mi naona ingekuwa vyema kama limit ingekuwepo katika mambo mawili kwa pamoja.

1- umri wa kustaafu ( mf. miaka 60)
2- muda wa kutumikia( mf. miaka 25)

Hii ingeleta uwiyano katika idadi ya wanaoajiriwa na wanaostaafu.

Kwa mfano mtu ameajiriwa akiwa na miaka 25, basi atatumikia kwa miaka 25 na kustaafu hatakama hajafikisha umri wa kustaafu(yaani 60).
Na atakayeajiriwa na miaka 38, atastaafu akifikisha miaka 60, hatakama hajamaliza muda wake wa kutumikia(yaani miaka 25).

Nadhani mfumo wa namna hii kidgo ungeleta tija.
 
Mkuu uko sahihi 100%. Hata kesho wafanye hivyo, tumshawishi waziri wa kazi, ajira, vijana..... awasilishe mswada maalum Bungeni. Binafsi nitaunga hoja mkono 100%.
 
Hii haitokuwa njia mbadala, japo kwa mwanzo litakuwa limepunguza kitu maana litakuwa limesogeza muda wa kustaafu.Lakini baadae mambo yatarudi vilevile.

Kwa sababu ikiwa umri wa kustaafu ni miaka 60, basi atakaye kaa kazini mda mrefu ni yule aliyeingia na umri mdogo, na hapa ndipo penye tatizo.

Mi naona ingekuwa vyema kama limit ingekuwepo katika mambo mawili kwa pamoja.

1- umri wa kustaafu ( mf. miaka 60)
2- muda wa kutumikia( mf. miaka 25)

Hii ingeleta uwiyano katika idadi ya wanaoajiriwa na wanaostaafu.

Kwa mfano mtu ameajiriwa akiwa na miaka 25, basi atatumikia kwa miaka 25 na kustaafu hatakama hajafikisha umri wa kustaafu(yaani 60).
Na atakayeajiriwa na miaka 38, atastaafu akifikisha miaka 60, hatakama hajamaliza muda wake wa kutumikia(yaani miaka 25).

Nadhani mfumo wa namna hii kidgo ungeleta tija.
Naunga mkono hoja
 
Kama maada inavyojieleza ,hii ingesaidia kuwapa fursa zaidi vijana na kuchochea ari ya nguvu kazi na maendeleo zaidi,watu wangejiandaa mapema na kuwaachia vijana Nafasi ,pasi na kuwa na vijana wengi mtaani wasio na ajira rasmi ilhali wana taaluma mbalimbali na kuwa wategemezi zaidi.

Natamani Serikali iliangalie Hilo kwa kina
Una point mkuu, ila serikali imesogeza 60 kwa hiyari, 65 kwa madakari bingwa na na wahadhiri wa vyuo vikuu!
 
Kama maada inavyojieleza ,hii ingesaidia kuwapa fursa zaidi vijana na kuchochea ari ya nguvu kazi na maendeleo zaidi,watu wangejiandaa mapema na kuwaachia vijana Nafasi ,pasi na kuwa na vijana wengi mtaani wasio na ajira rasmi ilhali wana taaluma mbalimbali na kuwa wategemezi zaidi.

Natamani Serikali iliangalie Hilo kwa kina
Naunga mkono Hoja.
Hii itasaidia vijana wengi waliokosa ajira kupata ajira na uzoefu ili nao wakija kustaafu na 55 waweze kuiendeleza sekta binafsi.
Kutokana na ujuzi na maarifa waliyopata makazini watapelekea kuzalisha ajira zingine nyingi huko sekta binafsi.
 
Hata hivyo bado si suluhisho, kama ni wataalam mbona kila mwa wataalam wanazaliwa kibao tena vitoto vidogo kabisa. Umri Miaka 50 unatosha ili inayo baki 20 kama ipo mtu ujiandaye vema juhitimisha safari. NB. A young man may die, but an old man must die.

Sent from my FIG-LA1 using JamiiForums mobile app
 
kuna wazee wapo zaidi ya miaka 65 hawataki kustaafu, wamejiongezea umri wa kustaafu.
Ifike wakati sasa umri wa kustaafu upunguzwe haswa kwa wafanyakazi wa uma, ili angalau vijana wapate nafasi,
Umri wa kustaafu uwe miaka 45 hiari 55 lazima.
maradhi ni mengi wengi wao wanakufa kabla hata hawajala matunda ya kazi zao
 
Unazo pesa za kuwalipa watu wanaostaafu na miaka 50, kiinua mgongo na pension za kila mwezi hadi mwisho wa uhai wao? hao wanaostaafu na miaka 60 tu mafao yao yameleta shida. Serikali hawawezi kukuruhusu kustaafu na miaka 50 labda uwe na shida nyingine kama ugonjwa wa muda mrefu, wanaweza kukuruhusu na miaka 55 kama huna majukumu makubwa sana.
 
Hata huko 55 ni mbali , 50 tu inatosha
Changamoto tuliyonayo kwa sasa ni kwamba sekta binafsi, ambayo ndiyo yenye uwezo mkubwa wa kuajiri vijana wengi sana kuliko serikalini, imepigwa pini sanaaaaa, yaani inayoshughulikiwa na kufuatwa fuatwa utadhani ni wezi au wauza ngada. Hii sekta binafsi kuanzia NGOs, mashirika ya nje, taasisi binafsi, viwanda, maduka, media industries, private schools, security companies, mashamba ya kilimo, mifugo, green houses, mahoteli, bars & nite clubs etc Huko ndiko kwenye ajira nyingi, sasa hivi kote huko hali Mbaya na wapunguza watu. Yaani nakuhakikishia hata muda wa kustaafu ungekuwa miaka 40 bado isingesaidia kwa sababu serikalini wanaoajiriwa na kustaafu kila mwaka ni wachache mno ukilinganisha na walioko mtaani na wanaoongezeka kila mwaka toka vyuoni.
 
Back
Top Bottom