battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,717
- 2,582
Hayati mchungaji Mtikila wa DP aliwahi kuwahimiza sana wapinzani kupigania katiba mpya kwanza kabla ya kukimbilia kushiriki chaguzi mbali mbali kwa katiba iliyopo ambayo imeipa CCM meno ya kufinyanga matokeo ya uchaguzi na ama kuweka wasimamizi wa tume ya uchaguzi makada.
Aliwahimiza wenzake kuwa ni bora tuchelewe lakini tukianza tuwe na uwanja sawa wa ushindani katika siasa.
Neno hilo nalikumbuka tena leo na nimeona niwazindue Vyama husika vyenye nia ya kuleta upinzani wa kweli Tanzania.
Kila kukicha CCM wanabadili sheria angani,kama hivi mwaka uliopita walibadili sheria ya msajili wa vyama na kumuongezea meno msajili ya kuweza kuviingilia vyama na kuvifuta au kuengua viongozi wake.
Nguvu hii aliyopewa msajili inafanana sana na nguvu alizopewa msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kama walivyofanya jaribio hilo la kuwaengua wagombea kwa kisingizio eti hawakutimiza mashariti.
Mwakani katika uchaguzi mkuu yatafanyika makubwa kuliko haya ,maana tayari msajili na tume vinaongezewa meno ili kuhakikisha wapinzani hawafurukuti tena Tanzania.
Nadhani UPINZANI sasa ni wakati muafaka kuzinduka na kujipanga upya .
NB
Mabadiliko haya ya kanuni na sheria yanapofanyika wasiache kuyapitia kwa karibu na kudodosa vipengele vyote vinavyowabana na vile vinavyowatega ili wakosee na wasiwemo kwenye mtanange wa uchaguzi.
Wakati ni huu,not too late.
Wajukuu zetu wanweza kuja faidika matunda ya juhudi zetu zikifanikiwa.lakini tukiwaacha waje kupambana wao watatutimba kwenye makaburi yetu na kututukana kwa ubwege wetu.
Na huenda wao ikawalazimu kuingia msituni badla ya kutumia diplomasia,maana zama zitakuwa zimebadilika.
Nawasilisha