Wakuu,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi Kijana wenu Mtiifu na Mwaminifu, ningependa kuuvunja ukimya wangu na kuiweka wazi nia yangu ya kutaka kumchumbia Mwana-Jeiefu mwenzangu, Mrembo wa Ukweli Miss. Shonza.
Tangu nilipoiona Picha yake basi moyo wangu ulisimama kwa sekunde kadhaa na kila nisikiapo ama nionapo jina lake likitamkwa humu (hususani Jukwaa la Siasa) basi huwa mapigo ya moyo yanaongezeka.
Japokuwa nina aleji na Magamba, lakini kwa huyu Bi. Shosti ninauomba radhi Ubongo wangu na kuupa moyo nafasi ya kuamua bila kuingiliwa. Pia ninamuomba radhi Pacha wangu ambaye ameonesha msimamo wa kukataa kata kata kumtambua Shonza kama wifi yake. Pia ninawamba radhi wale wote wanaotajwa kuwa na mahusiano na Shonza na kwa kauli thabiti ninawataka wasitishe mahusiano hayo mara moja!!! Vinginevyo Mabwe Pande inawasubiri.
Kwa sasa niko mbioni kufanya mikakati ya kumfikia ili nimweleze lengo langu kwake, ni matumaini yangu kuwa nitakubaliwa.
Naombeni Mniombee
Mapendo.
TANMO.