Natangaza rasmi kuihama Yanga

Natangaza rasmi kuihama Yanga

Sijajua ni kwanini mpaka Leo Yanga Huwa hafanyi Vizuri Mapinduzi..
 
Sio kwa kipigo hiki 4-0 jamani kwel au ndio mwaka mpya,....Sijui nitaweka wapi uso wangu..... Nahama TIMU jaman sio kwa aibu hii Yanga .....Azam mmetumwa na Simba Mahasimu
a5c8ec42f6e9703b57a05ecd86b6e7ba.jpg
 
wewe bure kabisa
Sio mimi Mkuu. Kuna jinga la Mikia ndio lilikuwa linapost huo utumbo. Baadhi nishazifuta. Unajua aliomba laptop na nilikuwa nimecheck keep sign in. Kanikera sana. Hapa ashapata adhabu ambayo hatokuja kuisahau maishani mwake
 
Akili zimewarudia bado mtaleta sahali tu.Iliponyesha mvua waungwana wameshajua panapovuja. Hizo zingine ni kelele tu za debe tupu.4 G imefanya wengi wenye viburi wawe na heshima kama mwali aliyepo unyagoni akisimamiwa na manyakanga. Leo tutapewa kila mifano ya timu kufungwa. Mifano hiyo imeanza leo?Haikuwepo kabla ya mechi ya ARBA?
Sasa kama unajua matokeo hayo siyo mageni, nini sasa kinakuwasha?
 
Unawashwa wewe. Mimi nashangaa mmejua kuna matokeo hayo baada ya kulambishwa koni. Kabla ya hapo lugha za mpira unadunda mlikuwa hamzitumii. Baada ya 4G akili zimewarudia.
 
Januari 7 2012 Azam 3 Yanga 0
Januari 7 2017 Azam 4 Yanga 0
Mbona imeanza kuwa tabia kwenye kombe la Mapinduzi.
 
Huko kusini mwa Tanzania wanasema "chuma chikoli moto "kwa mujibu wa mtangazaji wa Azam TV. Jiji kimyaaa migongo wazi hoiiiii.
 
Back
Top Bottom