Natatizwa na BBC kuhusu Kiswahili

Natatizwa na BBC kuhusu Kiswahili

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Wakuu, hivi sasa BBC Swahili inaadhimisha miaka kama sikosei 67 ya kuanzishwa kwake. Tatizo nimeliona ni mtangazaji aliyejikita Zanzibar akisema Kiswahili ndipo kilipoanzia.

Mie, natambua Kiswahili chimbuko lake ni Lamu nchini Kenya sasa kama ni mwendelezo wa upotoshaji unaoendelea ni hatari tena kwa mtangazaji aliyepo kwenye chombo cha habari kikubwa kama hicho.
 
Ata mie huwa nakerekwa sana na hawa wana habari walioko BBC swahili... hasa hawa wa kenya yaan wana tumia kiswahili cha ovyooo, ifike muda sasa BBC watuletee hidhaya ya kiswahili cha Kenya na cha Tanzania
 
Halafu kuna reporter mmoja kutoka Uganda nadhani; maneno "kulalamika" au "kukosoa" anatumia neno "kukashifu", miaka nenda rudi, sasa halafu na wenye mamlaka kwenye chombo ambacho huwa anaripotia, wamemwachia tu.
 
Wakenya watu wa fursa!! BBC kama ilivyo vyombo vingi vya magharibi maudhui yamejikita katika propaganda na bad news kwa third world countries,,Mtu makini anayetafuta kweli na ulimwengu/dunia inakwendaje hawezi kukitilia manani chombo hiki.
 
Back
Top Bottom