FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,956
- 47,046
Leo nimeingiza kumbukumbu mbaya sana katika kichwa changu, na inanitesa sana!
Nilikuwa mjini katika mizunguko ya hapa na pale, ghafla alianza kujongea mtu aliyeonekana kwa haraka haraka kuwa ni wale wanaookota chupa za plastiki ili kujipatia riziki.
Aliposogea karibu zaidi nikagundua kwamba mguu wake mmoja umevimba mno, yaani umekuwa kama wa tembo na ulikuwa na kidonda kikubwa sana.
Aliposogea karibu zaidi nikagundua kwamba anatembea kwa kuburuza ule mguu mmoja tena kwa maumivu makali kupindukia maana usoni alionesha kuwa mtu mwenye maumivu makali yasiomithilika yenye mchanganyiko wa arosto ya unga, njaa na kiu kali ikichanganyika na maumivu makali ya donda kubwa kwenye mguu wake uliovimba.
Aliposogea zaidi nikagundua kiroba chake cha kukusanyia machupa kilikuwa kitupu labda kilikuwa na chupa mbili tatu hivyo bado alikuwa ana shughuli pevu ya kuweza kupata walau kilo mbili akapate hata 500 ya chakula.
Basi akasogea zaidi hadi kwenye msitimu uliokuwa mita chache toka nilipo, huku nikimtazama kwa huruma sana, bila hata yeye kujua kama namfuatilia ile movement yake pale, akainama kuegemea ule msitimu kwa kichwa chake, na hapo ndipo nilipoona machozi yakimtoka, akayafuta na kujaribu kujikaza ila bado yakandelea kummiminika kwa kasi, akawa anajitahidi kuficha maumivu anayopata ila ikashindikana.
Daah, niliumia sana, nikatoa kanoti ka buku mbili nikampa kijana aliyekua jirani yangu ampelekee, yule kijana akapeleka kwa haraka, naye alipoona ona ile noti, kwa kweli alihisi mbingu imemshukia, aliichukua na kufuta machozi, yakafutika na yakapungua kumiminika, akaikunja ile noti vizuri na kuendelea na safari yake kwa mauivu yake yale ya awali.
Sasa kila nikikumbuka ile scenario najilaumu kwanini sikutoa zaidi wakati nilikuwa na bunda mbili za noti mfuko mwingine. Surely ningeweza kutoa zaidi, ila sikutoa, nateseka sana nikikumbuka, ila sehemu jamaa ameinama na anamwagika machozi ya uchungu, nimejikuta machozi yananitoka kila nikikumbuka, najilaumu, kwanini sikumpa zaidi, maana nisingepungukiwa chochote.
Hivi nyie matajiri wa dunia hii, mnawezaje kuishi kifahari huku binadamu wenzenu wanateseke kiasi hiki? Na nyie wauza madawa acheni, mnatesa vijana huku mitaani, aagh!
=====
Ya wadau

Hii inafanana na mimi nilikuwa kwenye pori fulani natembea nipo mwenyewe nimetoka kumtafiti mtu ghafla kwa mbele yangu nikamwona mbibi na babu kwa inavyoonekana ni mtu na mume wake wanaongozana wamebeba viroba vya nguo kabla sijawafikia kwa karibu wakaniuliza wewe kabila gani na unatokea wapi huku ? Nikawajibu.
Baada ya hapo wakaniambia wametokea kwenye msiba kijiji fulani na kijiji walichoniambia ndio nyumbani wanakwenda ni mbali sana maana siku moja kabla nilikuwa huko kikazi na wanarudi nyumbani wameamua kupita njia ya miguu kwasababu hawana nauli na hawakula tokea wametoka msibani kadri nilivyokuwa nawasogelea kwa karibu bibi alikuwa ameshika kiuno mithili ya mtu aliyechoka na safari ndefu wapo chini ya kimvuli wamepumzika.
Babu akaniambia naomba tusaidie shilingi mia tano tu tukanunue mandazi ili tuendelee na safari nikawapa shilingi elfu moja kisha nikawauliza je kutoka hapa mpaka mnapokwenda shilingi ngapi wakanieleza nikampatia kila mmoja nauli na ile mia tano kila mmoja ya kula bibi alivyoona vile alilia sana kisha akachukua zile noti akaziombea akajifuta nazo machozi akanipangusia paji la uso kisha tukaagana ila nami nilijuta baadae sana nilipokuja nikatumiwa shilingi laki mbili jioni yake mpesa sikujua itatumwa baada ya kuachana nikajuta kwanini nisingempa ile akiba niliyokuwa nayo kunitunza hiyo siku