minja mgumu
JF-Expert Member
- May 9, 2017
- 206
- 316
Na ukiona huwezi kutoa 100 kwenye 500 yako jua hata ukiwa na mamilioni hutatoa vile vile, sababu hela haitoshagi kamwe na shida haziishagi.Anza Sasa mgawane hicho kidogo ulichonacho
Kutoa Ni moyo , usisubiri eti nikiwa na uwezo,
Kutoa ni moyo na kuwa nacho pia, huwezi kuwa unao moyo then ukatoa utatoa nini mafua.Anza Sasa mgawane hicho kidogo ulichonacho
Kutoa Ni moyo , usisubiri eti nikiwa na uwezo,
Utakuta viongoz wa dini wanajisahau sna hili unakuta wameelemewa na vya dunia utakuta ktk nyumba ya mungu kiongoz anasema anataka gari la 50,100mill na nyumba ya kuishi yenye thamani kama gharama ya hela ya gari.amesahau kuwa wapo kondoo zake hata mlo 1 ni wakusua sua mbaya zaidi anaenda mbali zaidi hadi kuweka kiwango cha pesa kutoa kama sadaka isipungue kiasi frani je?akiwa hana sadaka asiende kuabudu?na kwanni asifikilie gahari ya gharama Mdogo na kusaidiana kwakile kilichopatikana kwa wenye mahitaji na kuwatembelea kondoo wako uone maisha wanayo ishi.kuna utofauti sna KUMTUMIKIA MUNGU na KUTUMIKIA DINI.mungu atusaidie sna
tena amini nakwambia ukisaidia kwa moyo Mungu hukuongezea ili uwe daraja kwa wengine.Kuna jamaa alikuja dukani kaniomba panadol 2 tu kaniambia anaumwa nimsaide alpo anza kuondoka nikamuita,the way alvokua anatembea hata sura mwili wake ulkua dhaifu sana inaonesha anaumwa sana nikamuulza umekula akajibu hapana kwa kutikisa kichwa nikampa mkate juice na maji daah alivokua anakula akimeza anakunja sura kwa kuonesha kwamba kuna maumivu anapata alposhiba akashukuru nikampa buku nikamwambia abebe na vyakula vyake akasepa zake
ukiamua kusaidia saidia kwa moyo mmoja hujui kesho yako
Duh..Uko tofauti sana dadaUlimuoona maeneo gani? Unaweza kurudi na ukiulizia bodaboda wa hapo ,wauza maduka ,wapiga debe au wafanya biashara hapo.
Jaribu kum-describe wanaweza kukuambia if he is a regular maeneo hayo then acha namba yako wakimuona wakujulishe na uwasiliane nae kupanga umkute hapo umsaidie zaidi
NB: Kama hii issue ni genuine ningependa kusaidia pia.
Barabarani kuna genuine case na kuna nyingine ni miradi. Mimi nafsi yangu in most cases haiwi kunjufu kusaidia wanaoomba na infact sometimes huwa nawaambia wakaokote chupa. Ila zipo nyakati unaona kabisa kuwa unahitaji kusaidia, huwa nasaidia bila hiyana. Ushauri wangu, kama una nafasi na umepima uzito, just help them, ila wa barabarani wengi wao ule ni mradi kama ilivyo miradi mingine.Ukiwa na moyo wa kusaidia barabarani ,basi saidia tu ila hako katabia mi nilishaacha muda mrefu sanaaa. Daslam hapa kuna watu wamefanya swala la kuomba omba kama biashara kuna muda inafikia hujui nani mwenye shida , nani anaigiza.
Utaratibu wangu nikiguswa kutoa ni bora niende kwenye vituo vya watu/watoto wenye uhitaji.
This is the bitter truthNa ukiona huwezi kutoa 100 kwenye 500 yako jua hata ukiwa na mamilioni hutatoa vile vile, sababu hela haitoshagi kamwe na shida haziishagi.
Mkorinto:uko sawandio maana huwa nafikiri na kijiridhisha kabisa kwamba Mungu hatujamuelewa bado.
tulichofanya ni kutengeneza sanamu kwa vile tunavyotaka tuione halafu tukaanza kuisifia kwamba inapendeza.tukaipa na class kwamba si rahisi kuigusa wala kuibusu,na wakati tumeichonga wenyewe.
kwa Mungu wote ni sawa,ndio maana utakufa bila hata sumni wala uzi wa nguo ya gharama uliyonunua.
tunaagizwa kusaidia watu mpaka point ya mwisho,sio ule ujinga wa wema usizidi uwezo,point ya kukosa wewe mwingine apate.
ubinafsi Mungu haupendi,ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano,kuliko TAJIRI(ubinafsi asili yake)kuingia mbinguni.
Dini ya kweli ni ile yenye kusaidia wajane na watoto.
tunyooshe mikono jaman Mungu atatuona.
Ombaomba wa vidonda feki wapo. Kuna mmoja alikuwa anabandika kipande cha ngozi mbichi ya mbuzi au ng'ombe tumboni, ule upande wenye damu unakuwa juu. Alikuwa akija dukani anafunua anasema anaomba fedha ya matibabu kwani kidonda kinazidi kulika. Mtu yeyote anayeona kama ana chochote ni lazima atoe haraka kwa mshtuko anaoupata. Mjini kuna ujanja mwingi. Ila kulingana na maelezo yako inawezekana huyo akawa ni mhanga wa madawa au maisha. Watu kama hao hata kuwapa fedha nyingi wakati mwingine inaweza kuwa kama kuwasukuma waendelee kuwa katika hiyo hali ili wasaidiwe. Njia bora ni kujua undani wake na kumsaidia kwenye kupata matibabu na kitu cha kuingiza kipato kila siku. Kumbuka hata hao wanaobandika ngozi baadhi yao mwanzoni walikuwa na vidonda vya kweli wakawa wanavitumia kuomba fedha lakini walipopona wakabuni njia mbadala ili kuendelea kuchuma.
Ukiwa na moyo wa kusaidia barabarani ,basi saidia tu ila hako katabia mi nilishaacha muda mrefu sanaaa. Daslam hapa kuna watu wamefanya swala la kuomba omba kama biashara kuna muda inafikia hujui nani mwenye shida , nani anaigiza.
Utaratibu wangu nikiguswa kutoa ni bora niende kwenye vituo vya watu/watoto wenye uhitaji.
Kweli kabisa ,pesa haijawahi kutoshaNa ukiona huwezi kutoa 100 kwenye 500 yako jua hata ukiwa na mamilioni hutatoa vile vile, sababu hela haitoshagi kamwe na shida haziishagi.
Binti1,
Its genuine, ilikuwa ile mitaa ya mbele ya jengo la jangwani wanapouza Rim za magari