Nateseka sana na complicated U.T.I. Naelekea kukata tamaa, nisaidieni niondokane na mateso haya

Mkuu pole sana kwa maradhi yako ya UTI .Kwa dawa za Hospitali huwezi kupona hata kama utatumia mwaka mzima kwani UTı ya siku hizi ni UTI Sugu haisikii kabisa kwa dawa kizungu lakini kwa dawa za Asili ukitibiwa utapona baada ya siku 21 tangu umetumia dawa za Asili huo ndio ushauri wangu.
 
"UTI in men is always considered complicated and treatment should be targeted at the likely bacteria".

Nenda hospital kapime kipimo cha urine culture kujua ni bacteria gani wanakusumbua ili upate dawa sahihi. Pia utaongezea na Doxycyline tabs.
 
Changamoto ni namna ya kupata dawa hiyo ya asili ya kufaa maana siku hizi wauza dawa feki wengi ajabu.
 
"UTI in men is always considered complicated and treatment should be targeted at the likely bacteria".

Nenda hospital kapime kipimo cha urine culture kujua ni bacteria gani wanakusumbua ili upate dawa sahihi. Pia utaongezea na Doxycyline tabs.
Asante sana rafiki.
 
mkuu anza hii dose kuchukua mchaichai mbichi uchemshe kisha uwe unakunywa kwa siku mara 3 glass 1, ingawa inapelesha kiasi ila ni dawa nzuri sana kwa UTI (hapa kiwepesi chemsha mwingi jaza kwenye jagi weka kwa friji.( hii dawa pia ina shusa sana sukari, hivyo kama unasukari ya kushuka usitumie)

Pia kama ukiweza uwe unasaga kitunguu swaumu punje 4 hadi 5 kisha unachanganya na baking soda nusu hadi kijiko kimoja kwenye glass ya maji unakunywa asubuhi na usiku ukitaka kulala! hii asubuhi tu ukikojoa utajua kuna dawa umekunywa kila la kheri !
utaanza sikilizia matokeo baada ya siku 5.
 
Tatizo hujasema uko wapi tukusaidie,kwa hospitali tu utameza hizo antibiotics hadi gunia hakuna kitu,tiba za asili ndio mpango mzima wiki moja utaona badiliko.
 
Asante ndugu
 
Njia ya vumbi na yenyewe husababisha u.t.i sugu..Kama unapenda kupita njia hiyo Basi ukiacha itasaidia sana.kumaliza tatzo


KWA MPALANGE.
 
Maumbile ya mwanamke anapotawaza hakikisha kinyesi kisiingie kwenye k, ukiweza ku control basi u.t.i utapona kabisa
 
Wanaume huwa hawapati UTI kirahisi ila shida inaanza miaka ikienda kama hiyo uliyonayo. Ikitokea umeanza kuwekea mirija ya kukojolea ndiyo tatizo huongezeka zaidi.

Maambukizi kwenye tezi dume (prostatitis) huwa ni kazi sana kuyatoa na mara nyingi husababisha UTI ya kujirudiarudia husababisha hata ukiitibu.
Hapo nashauri ubadilishe dawa. Hizi levofloxacin na wenzake ciprofloxacin zimepata sana na usugu wa wadudu. Jaribu kutumia azithromycin.
 
Unaishi na mke? Je, ulishampeleka kwa madakatar bingwa kupimwa yeye kama ana infections njia us uzaz?


NB: mwanamke anaweza kuwa na infections za hzo UTI bila kuonekana rahis zaid ya mwaka,unajikuta unakarbia kupona,unakutana nae,unawachukua wadudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…