Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba namba ya Dr, wa mambo magonjwa ya tumbo toka hiyo hospital tafadhali kama hutojaliAkishindwa nimpe mawasiliano aulize mda wa kuonana na specialist wa ngozi
Wa tumbo Sina maybe nikupe namba ya reception wao watakupaNaomba namba ya Dr, wa mambo magonjwa ya tumbo toka hiyo hospital tafadhali kama hutojali
sawa itashukuruWa tumbo Sina maybe nikupe namba ya reception wao watakupa
unaweza kunisaidia alipoenda kupata hiyo tiba?Ni hivi: kuna mtu wa karibu sana kwangu alikuwa ana tatizo la kuwashwa mwili mzima kama unavyosema. Infact alikuwa anasema siyo kuwashwa bali alikuwa anasikia vitu kama sindano vinachoma choma mwilini. Na hii ilikuwa inatokea kwa muda fulani na inakuja ghafla na kutoweka ghafla. Kwa mfano akifanya kazi mwili ukipata joto kidogo hivyo vitu vinavyochoma vinatokea mwili mzima. Wakati mwingine akitoka kuoga navyo vinachoma. Pia ilifikia hatua macho akienda kulala macho yanakuwa kama mtu kaweka pilipili ndani na machozi yanatoka. Akiamka na kukaa kitako macho yanakuwa sana. Basi akafanya kufanya kipimo akakutwa na inflamation kwenye bowel. Aliambiwa inflamation yake imesababishwa na mwili wake kuingia kwenye kitu kinachoitwa autoimmune, hivyo unatoa ''askari'' wa kujinga na magonjwa na wale ''askari'' wanashambulia mwili wake hivyo kusababisha inflamation. Hivyo alipewa dawa za kuufanya mwili wake usitoe tena wale ''askari'' pasipo sababu. Baada ya kutumia zile dawa ile hali kuwashwa ikaisha.
Mungu akuponye. Nilishawahi kuugua gonjwa baya sana na ambalo lilikuwa linataka kukatisha maisha yangu, nikakata tamaa kabisa, nilichokifanya kwanza ni kutengeneza maisha yangu na Mungu, nikiamini madaktari wanatibu ila Mungu anaponya. Ashukuruwe Mungu aliniponya kabisa hadi madaktari walionipima awali walishangaa imekuwaje nimepona kabla ya operation ya ajabu waliyotaka kunifanyia. hata hivyo, maombi mengi yalifanyika kwa kuomba na kufunga na kumlilia Mungu, naye akaniponya. Mungu huwa anaponya, uwepo wa madaktari haimaanishi Mungu kakabidhi kila kitu kwa madaktari, pale madoctor wanapoishia uwezo wao hapo Mungu ndio anaanza kabisa.Ndugu zangu naombeni ushauri,
Nina tatizo la ajabu linalonitesa kwa muda wa miaka mitatu sasa la mwili wangu kuwa na muwasho mithili ya pilipili hasa ninapolala tu.Ni maumivu makali ambayo yanaanzia katikati ya tumbo na kifua nakusambaa sehemu mbalimbali za mwili,mapajani,mikononi na sasa yanasambaa hadi usoni na kunifanya kila siku nisilale usiku.
Muwasho si wa kujikuna wala kuvimba ila ni WA ndani kwa ndani,kazi yake ni kuvuruga mwili tu na usingizi kupotea.
Nachoshangaa ni kwamba tatizo hili halitokei nikiwa nimeketi wala nikiwa nimesimama,natembea au kufanya chochote,bali nikilala tu na hasa napoanza kupata usingizi huanza kwa ukali!relief yangu ya kwanza huwa ni kuamka na kukaa,ambapo huchukua dakika moja yanapotea.
Nimeshafanya vipimo vingi kwenye Hospitali kubwa hapa Dar ikiwemo Saifei vya damu na Endoscopy, kilichogundulika kilikuwa inflammation bowels pekee (tatizo kwenye utumbo) ambalo sidhani kama ndio chanzo cha muwasho huu kama mtu unavyohisi muwasho wa pilipili halafu si mtumiaji.
Wadau hebu tushare experience ili na Mimi nifurahie usingizi, tatizo hili huja na kuondoka.