Nateswa na ugonjwa huu wa ajabu, msaada tafadhali

Nateswa na ugonjwa huu wa ajabu, msaada tafadhali

Ni hivi: kuna mtu wa karibu sana kwangu alikuwa ana tatizo la kuwashwa mwili mzima kama unavyosema. Infact alikuwa anasema siyo kuwashwa bali alikuwa anasikia vitu kama sindano vinachoma choma mwilini. Na hii ilikuwa inatokea kwa muda fulani na inakuja ghafla na kutoweka ghafla. Kwa mfano akifanya kazi mwili ukipata joto kidogo hivyo vitu vinavyochoma vinatokea mwili mzima. Wakati mwingine akitoka kuoga navyo vinachoma. Pia ilifikia hatua macho akienda kulala macho yanakuwa kama mtu kaweka pilipili ndani na machozi yanatoka. Akiamka na kukaa kitako macho yanakuwa sana. Basi akafanya kufanya kipimo akakutwa na inflamation kwenye bowel. Aliambiwa inflamation yake imesababishwa na mwili wake kuingia kwenye kitu kinachoitwa autoimmune, hivyo unatoa ''askari'' wa kujinga na magonjwa na wale ''askari'' wanashambulia mwili wake hivyo kusababisha inflamation. Hivyo alipewa dawa za kuufanya mwili wake usitoe tena wale ''askari'' pasipo sababu. Baada ya kutumia zile dawa ile hali kuwashwa ikaisha.
unaweza kunisaidia alipoenda kupata hiyo tiba?
 
Ndugu zangu naombeni ushauri,

Nina tatizo la ajabu linalonitesa kwa muda wa miaka mitatu sasa la mwili wangu kuwa na muwasho mithili ya pilipili hasa ninapolala tu.Ni maumivu makali ambayo yanaanzia katikati ya tumbo na kifua nakusambaa sehemu mbalimbali za mwili,mapajani,mikononi na sasa yanasambaa hadi usoni na kunifanya kila siku nisilale usiku.

Muwasho si wa kujikuna wala kuvimba ila ni WA ndani kwa ndani,kazi yake ni kuvuruga mwili tu na usingizi kupotea.

Nachoshangaa ni kwamba tatizo hili halitokei nikiwa nimeketi wala nikiwa nimesimama,natembea au kufanya chochote,bali nikilala tu na hasa napoanza kupata usingizi huanza kwa ukali!relief yangu ya kwanza huwa ni kuamka na kukaa,ambapo huchukua dakika moja yanapotea.

Nimeshafanya vipimo vingi kwenye Hospitali kubwa hapa Dar ikiwemo Saifei vya damu na Endoscopy, kilichogundulika kilikuwa inflammation bowels pekee (tatizo kwenye utumbo) ambalo sidhani kama ndio chanzo cha muwasho huu kama mtu unavyohisi muwasho wa pilipili halafu si mtumiaji.

Wadau hebu tushare experience ili na Mimi nifurahie usingizi, tatizo hili huja na kuondoka.
Mungu akuponye. Nilishawahi kuugua gonjwa baya sana na ambalo lilikuwa linataka kukatisha maisha yangu, nikakata tamaa kabisa, nilichokifanya kwanza ni kutengeneza maisha yangu na Mungu, nikiamini madaktari wanatibu ila Mungu anaponya. Ashukuruwe Mungu aliniponya kabisa hadi madaktari walionipima awali walishangaa imekuwaje nimepona kabla ya operation ya ajabu waliyotaka kunifanyia. hata hivyo, maombi mengi yalifanyika kwa kuomba na kufunga na kumlilia Mungu, naye akaniponya. Mungu huwa anaponya, uwepo wa madaktari haimaanishi Mungu kakabidhi kila kitu kwa madaktari, pale madoctor wanapoishia uwezo wao hapo Mungu ndio anaanza kabisa.

hata kama watu hawaamini, ila MUngu huwa anafanay miujiza, huwa anaponya, anaweza kukuponya, kabidhi maisha yako kwake, okoka na umweleze kwamba yeye anasame atakusamehe maovu yako yote na kukuponya magonjwa yako yote na kukuokoa uhai wako na kaburi. tumaili lako liwe kwa Mungu, hao madaktari wengine huwa ni incompetent tu, na wengine wanaingiliwa na shetani na kufanya vitu vya ajabu kabisa bila kutegemea, usione wamevaa hayo magwanda meupe, wengine hapo hawana uwezo wa kukusaidia hata kama ni specialist, na wengine hata kama wanaweza ila shetani anaweza kuwatumia. though wapo wengi pia ambao MUngu huwatumia kutibu ila Mungu ndiye anaponya.

hujiulizi kwanini mtu anatumaini mno kwa daktari, halafu anasahau mkasi kwenye tumbo wakati wa operation, au anafanya makosa makubwa kwenye operation hadi anashitakiwa balaza la madaktari na kufutiwa usajili? na yeye ni daktari mzoefu. weka tumaini kwa Mungu ili basi kama unatibiwa na madaktari hawa Mungu awaongoze na akupe yule asiye na upuuzi. mpe Yesu maisha na atakusaidia katika hili.
 
Back
Top Bottom