Nateswa na ugonjwa huu wa ajabu, msaada tafadhali

unaweza kunisaidia alipoenda kupata hiyo tiba?
 
Mungu akuponye. Nilishawahi kuugua gonjwa baya sana na ambalo lilikuwa linataka kukatisha maisha yangu, nikakata tamaa kabisa, nilichokifanya kwanza ni kutengeneza maisha yangu na Mungu, nikiamini madaktari wanatibu ila Mungu anaponya. Ashukuruwe Mungu aliniponya kabisa hadi madaktari walionipima awali walishangaa imekuwaje nimepona kabla ya operation ya ajabu waliyotaka kunifanyia. hata hivyo, maombi mengi yalifanyika kwa kuomba na kufunga na kumlilia Mungu, naye akaniponya. Mungu huwa anaponya, uwepo wa madaktari haimaanishi Mungu kakabidhi kila kitu kwa madaktari, pale madoctor wanapoishia uwezo wao hapo Mungu ndio anaanza kabisa.

hata kama watu hawaamini, ila MUngu huwa anafanay miujiza, huwa anaponya, anaweza kukuponya, kabidhi maisha yako kwake, okoka na umweleze kwamba yeye anasame atakusamehe maovu yako yote na kukuponya magonjwa yako yote na kukuokoa uhai wako na kaburi. tumaili lako liwe kwa Mungu, hao madaktari wengine huwa ni incompetent tu, na wengine wanaingiliwa na shetani na kufanya vitu vya ajabu kabisa bila kutegemea, usione wamevaa hayo magwanda meupe, wengine hapo hawana uwezo wa kukusaidia hata kama ni specialist, na wengine hata kama wanaweza ila shetani anaweza kuwatumia. though wapo wengi pia ambao MUngu huwatumia kutibu ila Mungu ndiye anaponya.

hujiulizi kwanini mtu anatumaini mno kwa daktari, halafu anasahau mkasi kwenye tumbo wakati wa operation, au anafanya makosa makubwa kwenye operation hadi anashitakiwa balaza la madaktari na kufutiwa usajili? na yeye ni daktari mzoefu. weka tumaini kwa Mungu ili basi kama unatibiwa na madaktari hawa Mungu awaongoze na akupe yule asiye na upuuzi. mpe Yesu maisha na atakusaidia katika hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…