Nateswa sana na jini mahaba

Tambua kwamba mwili wako si nyumba ya mashetani na majini mwili wako ni hekalu la Mungu,usi deal na huyo jini wala shetani gani deal na mwili wako,safisha hekalu la Mungu,unajua unaweza lalamika kwanini Mende hawaishi ndani kwako na kila siku unaweka dawa? shida sio dawa

unazoweka zakuzuia mende,shida ni CHANZO kinachosababsha mende kuja ndani kwako Yawezekana jikoni ndani kwako kuna uchafu na masalia ya vyakula kila iitwapo LEO kamwe mende hawawezi isha nyumbani kwako,utatumia kila dawa ila Mende waturudi tu,KWANINI? kwasababu uchafu ndio misingi ya nyumba yako.

SASA BASI achana kudeal na majini au mashetani Tuanze na jambo 1 tu ambalo kufanya usafi wa hekalu la bwana (huo mwili wako) Acha kila kitu unachotumia kisichompendeza Mungu.

Jisafishe,Jitakase kuwa serious katika hili,Kwenye maombi yako usitamke "Mungu namkataa huyu jini" nk nk wewe wakati unaomba mwambie "Mungu safisha mwili wangu,hili ni hekalu lako" mahali pako pa kupumzikia, nisafishe BABA nitakase..

Omba toba,omba utakaso,omba roho mtakatifu aingie ndani yako (yani fanya kama humjui jini) wewe deal na mwili wako komaa eneo hilo,Ukishampokea roho mtakatifu akakushukia maana yake Utakua safi.

sasa baada ya kumpokea roho mtakatifu,Dunda na Mia zako tuone huyo jini mahaba ataingia nyumba ipi wakati mwenye nyumba yupo ndani anatawala,Ajaribu bahati yake aone kitachomkuta.

Brother unapambana vita ya kiroho sio ya kimwili,lazima ukubali kuacha kila takataka ya dunia ili alie juu (roho mtakatifu) aweze kukushukia akusaidie, vita sio vyetu vita ni vya alie juu.

Ndio mana nimekwambia hata kwenye maombi usimpe kiki kwa kumtaja "jini mahaba sijui" usimpe showtime kabisa komaa na maombi ya utakaso,jiweke safi Nakuhakikishia ukishakua safi Hayo mengine unayoyataka yatakua Automaticaly tu.

Hamnaga Mende nyumba safi,hamnaga Panya nyumba safi ukiona hao viumbe jua kuna shida mahali shda si wao shda ni "wewe" na hata ktk hili mimi nina ujasiri kukwambia shda sio "jini mahaba" shida ni wewe. Badilika chukua hatua.
 
Halafu Kiranga atakuja kubisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikupe ushauri utakaomaliza shida yako, majini, mapepo na roho zote za shetani huwatesa watu pale wanapokuwa nauhalali. Dhambi humpa uhalali pepo kumtesa mtu.
Ukimwamini Yesu, unasamehewa dhambi zako na zaidi unapewa uwezo wa kuishi maisha matakatifu (uwezo wa kushinda dhambi).
Unapoombewa, jini hutoka na kwenda mahali kwa muda, baadae huja kuangalia kama bado kuna njia (mlango) wa kukuingia tena. Na kama kuna mlango huingia tena, na ikibidi huja na majini wengine kukaa humo.

Suluhisho ni kumwamini Yesu, akuokoe. Halafu ufanyiwe maombi ya ukombozi (kufunguliwa). Halafu acha dhambi.

Soma 1Yohana 3:8.
 
Katka maisha yangu sitokuja kisahau hawa viumbe walivyonitesa. Miaka ya 2016 Nilikuwa naamka saa tisa ya usiku naenda kanisani kuimba mapambio, kamwe sitokuja kusahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe muumini wa dini yoyote? Au dhehebu gani?
Ni huruma ya Mwenyezi Mungu pekee ndio inayo sambaratisha mashetani. Sio kuloga
 
Sipingi unachokiamini bt nahc hujakutwa na tatizo la hko kiumbe pia mshukuru sir god kwa hvyo ulivyo.
 
Uko sahihi kabisa. Shetani, jini nk ni wewe mwenyewe na mawazo yako unaeviumba. Kiuhalisia havipo.
 
Ushauri mzuri sana
 
Unajichanganya kwa waganga na kwenye maombi, hata ningekua mimi jini sikuachi maana ni vuguvugu huelewi umesimama wapi, kama umeamua kumuamini Mungu simama upande huohuo usijichanganye, hao waganga wa kienyeji wanazidi kukuongezea majini na kuweka madhabahu za kipepo ndani ya mwili wako zinazompa huyo jini uhalali wa kuweka makazi yake ndani yako.

Kuna jambo moja ukilizingatia litakusaidia, huyo jini ana uhalali wa kukaa ndani ya mwili wako, ukiweza kupata maombi ya kuvunja hiyo madhabahu yake basi hatakua na mahali pa kukaa na ataondoka, unahitaji maombi ya deliverance tena yanayoambatana na sadaka, na baada ya hapo uache njia mbaya zote uishi katika njia zinazompendeza Mungu
 
Nafikir wewe ndo giza,lenyewe sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…